Awali ya yote,nichukue nafasi hii kuwapa pole nyngi watu wa arusha pole kwa masahibu ya wanayoyapitia kwa siku za karibuni.Siwapi pole kwa kuwa tu ndo nyumbani kwetu nilipozaliwa ila ni kwa sababu wanastahili na mtanzania yeyote mpenda amani atafanya hivyo,MUngu azilaze pema peponi roho za marehemu.Nirudi kwenye hoja yangu ya msingi,hili ni tukio la pili la mlipuko wa bomu kwenye mkusanyiko wa watu huko arusha baada ya lile la kanisani,nachojiuliza ni je,polisi na taasisi za usalama hawakuchukua taadhari yeyote wakati ni hivi karibuni tu limetokea janga kama hilo?pili,hivi haya mabomu yanatengenezwa wapi?tayari walikuwa na pa kuanzia kwa tukio la kanisani,sasa iweje tukio la aina ileile eneo lilelile lijirudie bila upinzani wa vyombo husika?wananchi kwa kweli tunabaki dilema,je ni ugaidi,siasa chafu au ni wahujumu wa amani yetu?kwa hili,serikali itupe majibu kama wameshindwa watuambie pia,inachosha na kuhuzunisha kupoteza roho za wenzetu wasio na hatia hivihivi