Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Habari Wakuu!
Mwakinyoni mpiganaji mzuri lakini moja ya udhaifu wake ni majivuno ambayo hayana manaa yoyote kwenye kazi yake. Kwenye masumbwi yapo majivuno yenye maana katika ubondia lakini Kwa mwakinyo majivuno yake nayaona Kama hayana maana kwani hayamsaidii lolote.
Siku za nyuma Mwakinyo aliwahi kuponda mabondia wenzake akimlenga zaidi Twaha kiduku, Kwa kupigana kisa Gari Aina ya Crown, alisema yeye ni mpiganaji Mkubwa wakimataifa ambaye anapigana kupata mikanda na sio vizawadi mshenzi Kama vigari.
Alijitamba kuwa yeye anamagari mengi na mazuri hiyo hana uhitaji tena wa magari.
Nilimuelewa lakini kama ningeambiwa nimshauri ningemshauri vinginevyo!
Mwakinyo katoka Familia Masikini,
Mwakinyo yupo nchi Masikini!
Mwakinyo yupo kwenye Fani ambayo bado ipo chini na bado inaumasikini Mkubwa wa wafuasi.
Mwakinyo kujishaua na kukataa baadhi ya mapambano ndani ya nchi yake ni Dalili ya kuonyesha hayupo Sirius, na haijui nchi yake, na hajui vizuri watu wa nchi yake.
Hapa Tanzania Sanaa na mchezo wenye wafuasi wengi ni Muziki wa bongo Fleva, Hiphop kidogo na Muziki wa injili.
Mpira nao unawafuasi wengi hasa kwenye timu ya Simba, Yanga, na Azam.
Mchezo wa Masumbwi hauna wafuasi wengi hapa nchini kumaanisha bado sio biashara nzuri Kwa wawekezaji. Hilo lazima mwakinyo alijue.
Kama angekuwa analijua hilo asingejifanya kutaka dau kubwa lisiloendana na uhalisia wa Biashara ya mchezo wa Masumbwi hapa nchini.
Unataka milioni 100 wakati Pambano likiitishwa watu watakaoingia hawafikishi hiyo milioni Mia moja unategemea nini hapo.
Mwakinyo aache kujilinganisha na mabondia wa nchi za nje zilizojijenga katika mchezo huo.
Ni Sawa na Mchezaji wa mpira wa Tanzania achezaye Simba au Yanga stake kulipwa Sawa na mchezaji wa Mpira wa Mamelody ya Afrika Kusini. Hiyo ataonekana hamnazo!
Sasa Mwakinyo amegeuke tena! Anasema Mkanda ni zawadi tuu haumuongezee chochote, baada ya kunyang'anywa, anachotaka ni pesa. Inashangaza Sana.
Mwakinyo ninakushauri, jua umetoka familia Masikini, upo nchi Masikini, na upo kwenye mchezo wenye umasikini WA wafuasi.
Kiufupi wewe na wenzako bado mnajenga msingi wa mchezo wa masumbwi hivyo msitarajie makuuubwa Sana kama wenzenu wa BongoFleva!
Lazima muongeze wafuasi katika mchezo wenu huo ili ifikie hatua Pambano likitangazwa basi uwanja wa taifa unajaa au nusu ya uwanja kukaa!
Embu jiulize Mwakinyo, hivi Pambano lako likitangazwa unauwezo wa kujaza uwanja wa taifa au nusu yake?
Au hata vile viwanja vya mpira vya jamhuri Kama Morogoro, CCM kirumba ya Mwanza, au Sokoine ya Mbeya?
Jina linaweza kuwa kubwa lakini lisiwe biashara yenye faida kubwa!
Mfano, Sanaa ya stand comedy ndio Kwanza ni changa, inavijana wadogo Masikini, kwenye nchi Masikini, yenye umasikini WA wafuasi bao ndio wateja.
Kijana Kama Coy Mzungu ajifanye anataka malipo makubwa ilhali hana wafuasi wengi wanaoweza kutoa pesa kupata Huduma yake.
Ndio maana Coy yeye anapambana kuhakikisha anajenga msingi na kuimarisha wapenzi wa Sanaa hiyo.
Mwakinyo anawadharau Vijana wenzake wanaopigana mapambano mpaka ya Mbuzi asijue wenzake ndio wanajenga msingi wa mchezo wao ndani ya nchi.
Hawawezi kujidanganya kuwa wao ni Masikini Kama ulivyo wewe, wengi wenu elimu zenu ni duni katika nchi Masikini, mchezo wenu bado haujakubalika kivile ndani ya jamii hivyo ni jukumu Lenu kuifanya jamii iukubali. Na sio kulilia maslahi!
Mwisho, Mwakinyo unapaswa ujifunze pia Mazingira zaidi ya mchezo wenu, wafuasi wako, sio uishie kujifunza Kucheza Ringi pekeake!
Kuwa kama Diamond, hajaishia kujikita kwenye kuimba tuu studio na Jukwaani Bali amejifunza Mazingira ya nchi yetu, watu wake wakoje na wanapenda nini hasa Vijana, ambao ndio wateja wake.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Dar es salaam