Bongo aliyenunua gari na kujenga nyumba anajiona ametoboa maisha

Nunua gari na ujenge uache majungu shekhe🤣
 
Kwani ni uongo?.Kwa Tz ukijenga nyumba,unabiashara ambayo inakupatia kipato na unausafiri ambao utakusaidia kukupeleka unakotaka ndiyo maisha menyewe.Au wewe mleta mada una Nini Cha ziada ambacho unaona Hivyo havifai kuitwa mtu amefanikiwa?Au wewe mleta mada una mradi wa kwenda kuishi sayari ya mars kama Wa kina Elon musk?
 
gari ni kitu kizuri sana kwa maisha, linarahisisha kazi, linaharakisha utendaji kazi na utafutaji wako. lakini gari ni kitu hatari sana kwa afya yako. walionielewa wamenielewa. wengi wetu leo hii ukisema tutembee vituo viwili vya basi kwa mguu, au tupande daladala, inatuwia vigumu sana. kilichobaki ni kulipia gym na kuhangaika kujenga afya jambo ambalo yule anayepanda daladala na kutembea kwa mguu alipata bure kabisa. wanaotembea kwa mguu au daladala kwa shida wanapata afya njema sana ila wao tu hawajui.
 
Maelezo ya mafanikio yanatofautiana kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine. Huku kwangu mwenye mafanikio hayo ameona bora akazae nje huko kwasababu sasa anaweza hudumia-NIMEMTIMUA akaanze upya na familia mpya, vya huku aache huku ha ha haaa....maana mafanikio yake ni kuwa na gari + kuwa na nyumba
 
Wew una wivu. binafsi nahitaji nifikie hapo niwe na nyumba na niwe na gari kama Toyota Prius au Subaru impreza
Ndugu yangu mmoja alikua km wewe na akili za kindezi bi mkubwa akamuita chini akamshauri usiingie kwenye mikopo ndugu alivyo mjinga kasikiliza ushauri wa mkewe kadharau ushauri wa bi mkubwa kaenda bank katia saini M200 miezi 6 imekata yote nyumba kamaliza gari alikua anatembelea Alphard white ndio ilikua gari yake pendwa alienda kula mzinga k/koo gari ikafumuka mbele aliingia chini ya lori, bank kila mwisho wa mwezi wanakomba ½ na ¼ ya mshahara wake mpaka kichwa kikaanza kumuwaka moto watoto anasomeshwa shule za gharama mpaka akaanza kuwarudisha kayumba mmoja mmoja, usiombee yakukute
 
Siyo kweli kuwa wenye magari wote wamekopa.
 
Acha uzwazwa ninaishi na mzee mwenye magari ila namshangaa mara kwa mara kwanini anatembelea miguu na gari anazo zimepark nyumbani na mbaya zaidi muda mwingine anajichanganya kwenye usafiri wa umma na nyumbani kaacha magari yake hata watoto wake hawatembelei magari ni boda bajaji public transportation kila nikijiuliza kwanini yule mzee sipati majibu
 
Kibongo bongo kapunguza mishale mingi hapo ye anatafuta pesa kula na familia tu
 
sasa mbona unanitukana wakati unaongea kile kile nilichokiongea mimi? kwanini mzee anaacha magari na kutembea kwa mguu? kutembea kwa mguu sio kitu rahisi kama umezoea gari ndugu, labda kama hauna experience hiyo. ndio maana mida ya jioni badala ya kuoga na kupumzika utakuta watu wanakimbia riadha au kutembea kwa mguu, wanacompensate kitu hicho, ama la afya yako inaweza haribika sana.
 
😂 Puzzle ya maisha kila mtu ana ya kwake ambacho kinatakiwa ni kujaza jigsaw yako ili kufikia mafanikio.

Si kwa unafiki ila Blueprint ya waliotoboa maisha bongo ni walioweza kuushinda mtihani wa kodi ya mwenye nyumba kwa maana kuweza kujenga kiota chako haijalishi ni kibanda au ghorofa. Maisha ya mafanikio huanzia hapo maana uhuru wa kufanya chochote ikiwamo kuoa na kumiliki extras kama magari na vinginevyo.
 
Mbona unatoa povu? Kwa hali ya kibongo kumiliki gari na nyumba si jambo rahis. Japokuwa hao sitowaita matajiri bado ni uchumi wa kati. Acha wajipokengeze kufikia hapo si kazi rahisi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…