Bongo Movies kumshitaki DJ Mark (Anayetafsiri movies za nje)

Bongo Movies kumshitaki DJ Mark (Anayetafsiri movies za nje)

Tunachozungumzia sisi ni wao kulipa kodi TRA kwa biashara wanayofanya so ukienda kwa ofisi utakuta wamebandika lessen na TIN no
Hiyo siyo inayotakiwa kwenye swala la movie zinatajiwa sticker maalum kwa kila CD inauzwa shs 300 halafu inatakiwa ikakaguliwe bodi ya filamu kwa shs 500000 na wao wafanye hivyo kabla ya kuuza dukani.
 
Wawafungulie mashitaka na wenye ma-bus hasa ya safari ndefu kwa kuonyesha bongo movie bila ridhaa yao,watusaidie maana kuangalia ushuzi wa Bongo movie kutoka Dar–Mwanza ni zaidi ya kero nishagombana sana na makondakta.
[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3]
 
Yusuf Mlela hajui kuigiza kimeo tu. Hakuna hata movie 1 aliyofanya yenye jambo la maana.
Wafe njaa tu kama wafanyakazi wa umma waliofukuzwa na Magu.
DJ Mark aka Kidume.....wanakuja afu anatia kale kamluzi kake raha sana kumsikiliza kama unapenda mamovie yaliyotafsiriwa. Wakikushtaki tutakutetea....sheria imelala hapa.

Bongo movie ni uchafu tu kama uchafu mwingine wowote.
 
Hakuna uchafu nisiyoupenda kama bongo muvi!
Kudadeki!
 
Zifuate utaratibu ikiwemo kulipa kodi
Nyie mmekuwa TRA?acheni TRA ifanye kazi yake.Inaijua vizuri.

Huku kuingilia yasiyowahusu kunazidi kuichonganisha Bongo Movie na wapenzi wa Movie.Kumbukeni mnawahitaji sana wapenzi wa movie kuliko wao wanavyowahitaji ninyi.Enendeni kwa akili.
 
Kuna season inaitwa Merlin hivi utaniambia niache kuingalia Merlin niangalie jini anavuka barabara anaangalia kushoto Na kulia kisha ndo avuke barabara...hahahaha
 
Uzalendo hautafutwi kwa kulazimisha,kinachotakiwa wao bongo movie kuishauri serikali kupitia wizara husika kuunda bodi chini ya Basata kuratibu filamu na sanaa nchini.
Miongoni mwa majukumu ya bodi yao iwe ni kuhakiki,kusajili na kufuta sanaa/filamu/films zisizokidhi viwango.
Kusajili films/filamu za nje na kutoa utambulisha wa wanaotafsiri kwa ufasahaa.
Hapana,tayari kuna regulations za kutosha kuratibu masuala ya sanaa na movie.Tupo kwenye ulimwengu wa utandawazi, kuwa na bodi inayohakiki video za nje ni kutofahamu wakati tuliopo.Ukienda hapo inabidi uunde na tume ya kusimamia habari za TV za nje, miziki ya nje, na habari za mitandao ya nje inayoonekana Tanzania, sasa jiulize tukifanya yote haya tutafika?hatuwezi kuwa kisiwa.

Wao wangelalamika kuwa Basata haina maana kuwepo wangekuwa na hoja,tujiulize kwani Nigeria nao kabla hawajatoa movie uwa inapitiwa na bodi kama Basata?India wana bodi kama Basata?Marekani wana bodi kama Basata?Basata ina umuhimu gani kuwepo kwenye dunia ya sasa wakati haiwezi kucontrol soko kwenye dunia ya utandawazi?kwanin jukumu la kuangalia movie inafaa au haifai lisibaki kwa soko na local TV?

Kingine wangelalamika kwanin walipe kodi kwa CD kabla ya kuuza wakati kama biashara au kampuni (kama wanazo), mwisho wa siku watalipa kodi kwa mapato waliyoyapata?kwanini wao walipe before lakin biashara zingine viwanda vikiwepo wanalipa baada ya kuuza au kupata mapato?na je hii sio double taxation?

Bongo Movie wanachokosa ni ubora wa kazi zao na kukosa watu wa kuwaongoza.Wajitathmini kwa ukweli,wajue walaji wanataka nini,wafanye hayo.
 
Bongo movie wameishiwa swagga, sasa kwa mfano jamaa (Dj Murphy) akafuata taratibu za kulipa kodi na taratibu zote halafu akaendelea kutafsiri, watakuja na swagga gani tena?
DJ Murphy alivyoitendea haki udaaan wamshitakije jamii haitakuelewa
 
Ata wakimshitaki hatutaangalia movie zao kwa upumbavu kama huu
6a5253fc4b1a254e6890064148e33f55.jpg
Hizo subtitles ni balaa
 
Hawajapata kibali halali wanachakachua kupitia vibali vya kuuza accessories/ stationeries halafu wanatumia kuBurn movies kitu ambacho TRA hawakubali ndio maana kila mara wanakimbizwa na tra. Kupata kibali cha kuuza movie ya mtu ni mpaka movie ifikishe miaka 50.
duh...kwa hiyo na hawa wanaouza bongo movie kwenye maduka wanafanya makosa...maana hakuna bongo movie hata moja iliyofikisha miaka 50
 
Duuh ...bongo movie wakiingia humu wanazimia na haya matusi
 
Back
Top Bottom