Bongo Movies kumshitaki DJ Mark (Anayetafsiri movies za nje)

Bongo Movies kumshitaki DJ Mark (Anayetafsiri movies za nje)

Kwani akina Mlela wanapoweka maneno ya kiingereza, yayotafasili kiswahili kilichotumika kwenye movie zao huwa wanataka nini ?
Waache ujinga,anayetakiwa kumshitaki huyo DJ ni Wamiliki wa hizo movie zinazotafasiliwa siyo akina Mlela na wenzake.
Mlela kavurugwa na njaa kali
 
Sasa hapa najiuliza hao bongo muvi wanachukia kwa sababu gani?

Ingekuwa jamaaa anatafsiri mamuvi yao kwa lugha nyingine kweli ,sasa muvi wacheze wengine halafu wao waje kukasirika hii inaingia akilini kweli?

Hapo wenye haki ni hao ni wenye muvi zao kama vile wahindi ,wazungu wakorea nk na sio hao vikaragosi vya bongo muvi.
Wanamshitaki kwa niaba yao
 
Hao wacha wapigike na bado wataendelea kupigika hadi akili itakavyowarudia maana na laana za watanzania kwa jinsi walivyoegemea ccm kipindi cha uchaguzi
Kwani watanzania wote ni wapinzani wa ccm
 
Hivi kuna mtu mzima anaweza kuangalia huo up....zi unaoitwa BONGO MOVIES? Wanatafuta wa kumlaumu tu. Wakae chini wajipange ila siwezi kupoteza muda wangu kungalia hayo maigizo yao artificial!!! Bora wacheze kiduku na kuvaa sare za nyinyiemu ndo watapata mkate wao wa kila siku tu!!!!
 
Akiongea kwenye E-News ya East Africa Yusuph Mlela amesema Bongo Movies wameanza taratibu za kumshitaki jamaa maarufu anaetafsiri movies za nje maarufu kama Dj Mark na wengine wote wanaotafsiri movies za nje na kuwaharibia soko la Bongo Movies.

Mlela, "Tumeanza taratibu za kumshtaki jamaa sisi tunataka movies za nje zifuate taratibu kama sisi tunavyofuata ili kuwe sawa".

Bongo movies wameamua.
Waache njaa wanashindwa kufanya kazi nzuri zenye ubunifu wanahangaika na watu wanaotafuta ridhiki mara walalamikie wamachinga. BONGO MOVE NA BADO MPAKA MPATE AKILI .....USAWA HU HABEBWI MTU hakuna cha mutoto ya ng'ombe wala ndama
 
Back
Top Bottom