Hapana,tayari kuna regulations za kutosha kuratibu masuala ya sanaa na movie.Tupo kwenye ulimwengu wa utandawazi, kuwa na bodi inayohakiki video za nje ni kutofahamu wakati tuliopo.Ukienda hapo inabidi uunde na tume ya kusimamia habari za TV za nje, miziki ya nje, na habari za mitandao ya nje inayoonekana Tanzania, sasa jiulize tukifanya yote haya tutafika?hatuwezi kuwa kisiwa.
Wao wangelalamika kuwa Basata haina maana kuwepo wangekuwa na hoja,tujiulize kwani Nigeria nao kabla hawajatoa movie uwa inapitiwa na bodi kama Basata?India wana bodi kama Basata?Marekani wana bodi kama Basata?Basata ina umuhimu gani kuwepo kwenye dunia ya sasa wakati haiwezi kucontrol soko kwenye dunia ya utandawazi?kwanin jukumu la kuangalia movie inafaa au haifai lisibaki kwa soko na local TV?
Kingine wangelalamika kwanin walipe kodi kwa CD kabla ya kuuza wakati kama biashara au kampuni (kama wanazo), mwisho wa siku watalipa kodi kwa mapato waliyoyapata?kwanini wao walipe before lakin biashara zingine viwanda vikiwepo wanalipa baada ya kuuza au kupata mapato?na je hii sio double taxation?
Bongo Movie wanachokosa ni ubora wa kazi zao na kukosa watu wa kuwaongoza.Wajitathmini kwa ukweli,wajue walaji wanataka nini,wafanye hayo.