Bongo Movies kumshitaki DJ Mark (Anayetafsiri movies za nje)

Bongo Movies kumshitaki DJ Mark (Anayetafsiri movies za nje)

Ata wakimshitaki hatutaangalia movie zao kwa upumbavu kama huu
6a5253fc4b1a254e6890064148e33f55.jpg
Ahahahaaaa
 
Kujipanga ni pamoja na kupambana na soko la haki
Soko la haki kivipi? Bidhaa ikiwa sokoni mteja anaangalia kilicho bora. Tasinia ya filamu inahitaji uwekezaji mkubwa, billions of money. Hii tasinia imevamiwa na wahuni na wauza sura wasio na vipaji.
 
Hiyo siyo inayotakiwa kwenye swala la movie zinatajiwa sticker maalum kwa kila CD inauzwa shs 300 halafu inatakiwa ikakaguliwe bodi ya filamu kwa shs 500000 na wao wafanye hivyo kabla ya kuuza dukani.

Kama mnalipishwa isivyo mnapaswa muilalamikie serikali kuhusu hayo malipo bila kuwahusisha wasiohusika, mathalani hiyo ya kodi na laki 5 kwa bodi ya filamu.

Na mngefanya hivyo yawezekana mpaka sasa hayo malipo yangeishaondolewa au kupunguzwa.

Badala yake, nyie mnaangaika kucreate matatizo mengine.Serikali yoyote makini haiwezi kukubali kukosana na machinga nchi nzima wanaoishi kwa hizo CD za nje kwa sababu ambazo hazina mahusiano ya moja kwa moja na ya kimantiki.

Mjitafakari upya.
 
Katika kero yangu kubwa kwenye mabasi ni yale ma-tv yao hakika yananikera na utadhani wamerogwa maigizo ulioyaona Dar Lux utayakuta Shabiby,jana nimeamua kupanda Sai baba toka Dar–Sumbawanga kwa kua nilijua hawana tv wala redio ingawa scania imechoka ila nilikua na amani kwa kua kero ya bongo movie nilijua haipo.
Hahhhh Safi sana.ila mkuu zimefungiwa dar 2.
 
Duuh...labda wafunge na website za kudownload...wateja hawalazimishw kununua bidhaa,wateja wanachagua wanachokiona ni bora kwao,wateja wanaangalia prefferences and taste
 
Wawafungulie mashitaka na wenye ma-bus hasa ya safari ndefu kwa kuonyesha bongo movie bila ridhaa yao,watusaidie maana kuangalia ushuzi wa Bongo movie kutoka Dar–Mwanza ni zaidi ya kero nishagombana sana na makondakta.
Uwa wanankera kwel
 
Kweli hawa ndo bongo movie, wanaendelea ku act movies.....
hahahahahaha ngoja niishie kucheka tu kuptia comment zenu maana cna cha kuongezea kila kitu mmekisema ngoja niendelee kula popcorn huku nikiangalia series ya DEFENDANT. 😛😛
 
Hapana,tayari kuna regulations za kutosha kuratibu masuala ya sanaa na movie.Tupo kwenye ulimwengu wa utandawazi, kuwa na bodi inayohakiki video za nje ni kutofahamu wakati tuliopo.Ukienda hapo inabidi uunde na tume ya kusimamia habari za TV za nje, miziki ya nje, na habari za mitandao ya nje inayoonekana Tanzania, sasa jiulize tukifanya yote haya tutafika?hatuwezi kuwa kisiwa.

Wao wangelalamika kuwa Basata haina maana kuwepo wangekuwa na hoja,tujiulize kwani Nigeria nao kabla hawajatoa movie uwa inapitiwa na bodi kama Basata?India wana bodi kama Basata?Marekani wana bodi kama Basata?Basata ina umuhimu gani kuwepo kwenye dunia ya sasa wakati haiwezi kucontrol soko kwenye dunia ya utandawazi?kwanin jukumu la kuangalia movie inafaa au haifai lisibaki kwa soko na local TV?

Kingine wangelalamika kwanin walipe kodi kwa CD kabla ya kuuza wakati kama biashara au kampuni (kama wanazo), mwisho wa siku watalipa kodi kwa mapato waliyoyapata?kwanini wao walipe before lakin biashara zingine viwanda vikiwepo wanalipa baada ya kuuza au kupata mapato?na je hii sio double taxation?

Bongo Movie wanachokosa ni ubora wa kazi zao na kukosa watu wa kuwaongoza.Wajitathmini kwa ukweli,wajue walaji wanataka nini,wafanye hayo.
Noted
 
Teh
Hawa wauza sura wafanye kazi waache maneno... Watu wanapiga kazi toka enzi za Lufufu Leo anakuja na sura yake ya mapenzi na kuanza kuleta blah blah blah.
Shenzi porini.
hahahahahhahahaha SHIKAMOO tena kwa herufi kubwa sio kwa kunichekesha huko
 
Hii mibongo movie mijinga sijawahi kuona, eti think tank wao ni Bashite.............Duuuh.
 
Wengine walipe kodi pia
kwani wakilipa kodi ndio kazi zenu zitakuwa nzuri? kazi zenu mbayaaaaa tumewachoka tena mnavyozidi kufanya ujinga huu ndivyo mnavyozidi kuwaudhi watu
 
Back
Top Bottom