Bongo Movies kumshitaki DJ Mark (Anayetafsiri movies za nje)

Bongo Movies kumshitaki DJ Mark (Anayetafsiri movies za nje)

Mimi Ndio huwa siziangaliagi kabisa Hakuna jipya zaidi ya mapenzi tu. Na mavazi ya ajabuajabu. Hazina maadili kwawatoto.
 
wao walikurupukia mkorogo na kutoga masikio, halafu dharau nyingi mtaani wakati hao wanao wadharau ndio mabosi wao...wabadili tu njia ya kujiingizia kipato, wajiunge TOT kufanya maigizo huenda wakafikiriwa posho na chama tawala.
 
Kuna season inaitwa Merlin hivi utaniambia niache kuingalia Merlin niangalie jini anavuka barabara anaangalia kushoto Na kulia kisha ndo avuke barabara...hahahaha
Hahahahh jambazi anaingia ndan kuiba anavua viatu nje.
 
Ata wakimshitaki hatutaangalia movie zao kwa upumbavu kama huu
6a5253fc4b1a254e6890064148e33f55.jpg
[emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13]
 
Bongo movie wameishiwa swagga, sasa kwa mfano jamaa (Dj Murphy) akafuata taratibu za kulipa kodi na taratibu zote halafu akaendelea kutafsiri, watakuja na swagga gani tena?
wao bongo movies watamshitaki jamaa kama nani ?
 
Siasa tamu sana kwani wao siku hizi wanafanya move..................... Waende kuongea a mama ongea na mwanao wavumilie kama upinzani mpk mwaka 2020 ili na wao wapate kazi maana ndio wanayoiweza zaidi OVA
 
Wawafungulie mashitaka na wenye ma-bus hasa ya safari ndefu kwa kuonyesha bongo movie bila ridhaa yao,watusaidie maana kuangalia ushuzi wa Bongo movie kutoka Dar–Mwanza ni zaidi ya kero nishagombana sana na makondakta.
Mkuu umeua. Mimi nikajua ushuzi ni hewa na harufu kumbe wenzetu man macho makali hata hewa mnaiona. Ha...ha...haa.. Kusema ukweli bongo Mimi ni upuuzi
 
Nchini Kenya yupo DJ flani hivi jamaa anajiita 'DJ Afro'.Ukitazama movies zilizotafsiriwa na huyu DJ hautakuja kuangalia bongo movies milele,jamaa ametafsir movie nyingi sana kama vle Brothers Grimsby, Viral factor,fast and furious zote,movies zote za Dolph Lundgren,Movies za Michael Dudikoff,Prisoners of war the escape (P.O.W),Escape from Surbibor, Many ways to die in the west, movies za Keny Koshugi (mtoto wa Shokoshugi),Yankee the Zulu.Pia ukifuatilia kpind cha Churchill show huwa wanapenda kumualika,huyu DJ yuko very talented na huwa napenda movies zake kwa kuwa huwa anatafsiri tukio na cyo maneno.Kwa fikra hizi wanazokujanazo ndugu zetu wa bongo movies wanapaswa kujipanga.
DJ afro movie zake online zipo?
 
Kati ya matatizo ya hii tasnia ni hilo la kila kitu kuratibiwa na Wasanii.

Nadhani Tasnia/serikali ina vyombo vyenye mamlaka za kisheria kufuatilia uhalifu wa aina hii.

Na wala hapa sio suala la Bongo movie kutaka kazi zao zipate nafasi sokoni bali ni swala la kufuata sheria na suala la haki miliki zaidi, na huo ni uzembe wa serikali kuacha raia wake kuvunja sheria waziwazi mpaka kupelekea jamii kudhani kinachofanyika ni halali/haki.

Kukopi/kuhariri kazi ya Wengine ni uhalifu kama uhalifu mwingine wa kughushi hati, risiti, cheti n.k.

Kazi za kuhariri hufanywa kwa makubaliano kati ya Mzalishaji na anayetaka kuhariri...sasa ni wapi hawa watia sauti wetu wanawashirikisha wenye kazi zao? na jamii inawashangilia kana kwamba kifanyikacho ni haki.

Wasanii hamna haja ya kujiingiza kwenye migogoro isiyowahusu na kulumbana na jamii bila sababu, nyie himizeni tu vyombo vinavyohusika vifanye kazi zao.

Hata kama sio kwa ajili ya Bongo movie bado hakuna uhalali wowote wa kinachofanyika.
 
Bongo movie wameishiwa swagga, sasa kwa mfano jamaa (Dj Murphy) akafuata taratibu za kulipa kodi na taratibu zote halafu akaendelea kutafsiri, watakuja na swagga gani tena?
Hicho ndio cha kufanya na sio KUIBA.

Na usidhani kupata hizo haki ni kazi rahisi....we imagine kazi inayoandaliwa kwa milioni mia tano uende kuomba haki ya kutafsiri hiyo tozo yake itakuwaje? na hawatakubali bila kuhakiki kiwango cha ubora wa kinachotaka kufanyika.....hiyo ni pamoja na kuridhika na studio inayofanyia kazi hiyo pamoja na utaalamu wa 'sound', weledi wa watendaji n.k.

WATU WANAFANYA KAZI KWA BIDII KUPATA WANACHOTAKA...wenzetu Wazungu huwa wanahimiza sana huu ujumbe kwa Watoto ili wasije kufikiria kwamba waendako kuna njia za mkato za kupata mafanikio....sasa sisi Wabongo ni kuendekeza ushabiki tu hata kwenye mambo yanayohitaji kuelimishana.
 
Haah huyo jamaa inaonekana kunamovie anaandaa movie kwahiyo anatafuta tention ya watu ametoka kwa ney ameenda kwa DJ haingii hakilini atakm akimshitaki yule jamaa km hawatakuwa wabunifu hakuna atakae angalia movie zao
 
Mnachekesha kweli. Ninyi hamna Haki ya kunshtaki huyo anayetafsiri. Ninyi sio makampuni yenye haki miliki ya kazi hizo wala ninyi sio mamlaka husika za serikali mfano COSoTa.

Anaachoongea Mlela ni ujinga tu.
Afuate tu
 
Bac na wazungu wawashtaki bongo movie kwa kutumia subtitle za kiingereza. Maana hata sielew point yao. Kwa dj murphy akiweka subtitle za kiswahili kwenye movie za kiingereza haitokuwa offence?
 
Back
Top Bottom