Bongo Movies wengi ni vilaza, si ajabu wameilaza sanaa ya uigizaji. Wasomi ingieni huko

Bongo Movies wengi ni vilaza, si ajabu wameilaza sanaa ya uigizaji. Wasomi ingieni huko

Si nasikia huko sifa zao kuu n hizi

Uwe na tako

Uwe na mwonekano

Elimu walau ujue kusoma kuandika s muhimu Sana

Kwa mwanaume uwe handsome.

Nyingne n sifa za ziada tu

MKuu hivo vigezo vya urembo hata huko majuu pia hua vinapewa kipaumbele
 
Uliwahi kusoma chuo Mkuu?

Hivi unajua chuoni kuna kila aina ya fani? Kila aina ya watu?
Unadhani chuoni hakuna wenye vipaji vya kuigiza, kuimba, kucheza n.k?

Nayaelewa yote hayo mkuu, ila ninacho maanisha ni kua aliepasi vizuri darasani haimaanishi kuwa yeye ndie atakua bora, au alisoma chou haimanishi kua lazima yeye ndie atakua bora.
Hii falsafa ya kuamini Msomi wa chou kikuu ndio bora kwenye kila mahali fikra mbovu za kiafrica tunazokaririshwa. Kwa mantiki kama hiyo Tanzania tungekua katika nchi zilizoendelea duniani mana katika kila nafasi za uongozi zimejaa Maprofesa na Ma PHD, ila ndio wanaozidi kutuzamisha tu.

Naendelea kunukuu haya maneno

Ni muhimu kuheshimu UWEZO,hapa simaanishi elimu tu. Prof Kabudi ni zao la utafiti mzuri kuwa elimu bila akili ni sawa na choo bila mlango.
 
Bila shule hakuna utakachoigiza cha maana kwenye ulimwengu wa sasa zaidi ya vichekesho, futuhi, na vioja.
 
Anadhani Priyanka aliishia darasa la nane kama dada zake anaofanya nao kazi, hapo anataka kumfananisha Priyanka na Wema Sepetu kisa wote walikua maMiss, anashindwa kuangalia education backgrounds zao.

Usibadilishe mada. Wote hawajasomea filamu full stop na wamefanya vizuri.

Wewe unajua education background ya wema sepetu?
 
Industry ya Bongo haijawahi kufanya vizuri Budah, sema zipo baadhi ya Movie zilijitahidi, na hiyo ni kutokana na sababu kuwa kipindi hicho jamii ilikuwa gizani, wenye elimu walikuwa wachache, wenye Tv walikuwa wachache, Hapakuwa na Smartphone ambazo zingelinganisha kazi zetu na za kigeni.

Huoni mambo yamebadilika sasa, wewe darasa la pili utaigiza jambo gani kuifundisha jamii hii ya utandawazi zaidi ya vichekesho vyako?

mkuu muigizaji anatakiwa kufata script na maelekezo ya director kwenye kuigiza, sio kuelimisha jamii, kwahiyo udarasa la pili wake sio point kabisa hapo, Hayo ni masuala ya watunzi wa filamu.

Na sio kila filamu lazima ielimishe jamii, Zipo nyengine kwa ajili ya kuburudisha na nyengine kwa ajili ya kuonyesha uhalisia wa mazingira ya kijamii. Hayo masuala yenu ya fasihi hayana uhalisia kabisa kwenye mazingira ya filamu.
 
Bila shule hakuna utakachoigiza cha maana kwenye ulimwengu wa sasa zaidi ya vichekesho, futuhi, na vioja.

Tatizo lako linaanzia mbali sana, fikra zako ni kuwa muigizaji ndie mtengenezaji wa filamu. FIlamu haitengenezwi na muigizaji, muigizaji kazi yake ni kuigiza tu wanaomsimamia ndio wanaitengeneza filamu. kwahiovyeti vyke vya elimu sio nguzo muhimu kabisa kwenye kazi yake.
 
Wewe unataja Movie zenye bajeti kubwa wakati kuna filamu za kizungu zenye bajeti ndogo kabisa zinafanya vizuri, angalia filamu za kifilipino hakuna bajeti ya kutisha lakini zinachezwa kitaalamu, angalia filamu za kikorea zipo nyingi tuu zina bajeti ndogo, na vifaa visivyogharimu pesa nyingi.

Kwa hiyo hao wanaofatilia ndio wameamua kuigiza utopolo licha ya kuwa wafuatiliaji?

Acha "kuhisi" mkuy. Do your homework na ufanye research it seems ukiona movie unadhani ni actors na washika camera tu

Nitajie hapa movie za kizungu zilizofanya vizuri kwenye box office au kushinda golden globes au oscars alafu zina bajeti ndogo kama ya bongo movie!

Anza kugoogle I'll wait.
 
Mkuu tunachozungumzia hapa, ni kuwa hata huo uwekezaji mdogo uliofanywa mbona hatuoni la maana?
Ndio nikasema shida shule ndogo kwa wasanii wengi na wahusika wa filamu.

Filamu nyingi zimelenga mambo ya kitoto.

Yaani Watu wazima wanaigiza kama watoto, kimama mama na kibaba baba bhana!!!!!!!!!!!!

Mkuu hata hizo filamu za mambo ya kitoto nchi za wenzetu zipo na zinapiga hela. Na kama umekua mfatiliaji mzuri wa filamu za kimataifa utagundua hili, Filamu nyingi zinazofanya vizuri kibiashara sio zile zilizotengenezwa kiubora kabisa, hua ni zile zilizotengenezwa ki formula au kijanja kwa kukamata hisia za watazamaji, mana watazamaji wengi na wapenzi wa filamu hua wapo kimihemko Zaidi.
 
Unaona usivyo na akili nzuri. Hivi kama mmeweza kuigiza filamu mnashindwa vipi kuajiri maafisa masoko wakuwasaidieni kutafuta soko, mnashindwa kuandaa hata matamasha ya bei rahisi kwa kuingia mikataba na wanamuziki?
Haya mmeshindwa kuanzisha YOUTUBE CHANNEL Maalumu kwa kutangaza movie zenu, mmeshindwa kuanzisha page maalumu kwa kazi hizo?

Mnashindwa na watafsiri Movie hamjiulizi wanasambazaje?

Kitu kikiwa bora huwezi pata shida kukisambaza, lakini kikiwa kibaya lazima uone shida kukisambaza.

We jamaa yaani utengeneze movie kwa gharama kubwa kisha uweke youtube? Kwamba wakina ray, JB, marvel, universal pictures wote ni wajinga wale hawajaona youtube? Unajua malipo ya youtube? 😂😂

Alafu watafsiri movie si wanatumia mb tu kudownload wanaingiza sauti wanasambaza unaweza kulinganisha na film makers wenye crew zaidi ya 100?

Acheni akili za kimotivational speaker. Maisha sio rahisi hivo.

Ntaishia hapa nakwambia tena nenda kasome how film industry works ndo uje kuongea huu utumbo hapa.

Umenisikitisha sana movie? you tube?
Hahahaha.
 
Serikali unataka iwe sirius ili watu wapoteze vitumbua vyao?

Serikali ikiitambua Fani ya uigizaji itaweka vigezo lazima uwe na Diploma au degree moja unafikiri wangapi watabaki hapo?
Kisha watu wapewe leseni

Ulisikia industry gani duniani kama kigezo cha uigizaji uwe na Diploma au Degree? ulsikia wapi duniani kuwa actor lazima uwe na leseni ? mbona unazungumza mambo ya ajabu mkuu?
 
Kuna yule mama anaact kama waziri, khaa yale ndio maisha ya waziri kweli? Si bora hata wangesema ni mfanyabiashara mkubwa basi ikatosha,

Wanasingizia bajeti, lakini wanakopeshana pesa hadi kutukanana matusi mazito mazito,
Hayo madanga wanayopasiana wanashindwa kuwaomba wawafadhili wafanye movie moja matata yenye story nzuri ya kusisimua,

Shida directors wao, producers wao, Editors wao, halafu ushikaji mwingi wanafanya kazi kimazoea sana.

Waziri kama shangingi[emoji23][emoji23], hata mimi nilishangaa, Tatizo hawafanyi research maisha ya waziri yanakuaje akiwa nyumbani , the way wanavyoongea Yan utadhan mmama anayeuza wanawake malaya
 
Hapo ndio mnakosea, kuna muda sinema inatakiwa ikae sokoni lakini wewe kila miezi 3 unatoa filamu hapo unategemea nini

Mkuu unazungumza vitu ambabyo wewe mwenye huvielewi, Huko majuu kuna watu wanatoa hata filamu 3 mpaka 4 kwa mwaka. Fatilia Nigeria na India utaelewa.
 
Ulisikia industry gani duniani kama kigezo cha uigizaji uwe na Diploma au Degree? ulsikia wapi duniani kuwa actor lazima uwe na leseni ? mbona unazungumza mambo ya ajabu mkuu?

😂😂😂 Nilicheka sana kumbe na ww uliona kuwa actor lazima uwe na leseni

Nilichoona hapa wengi hawajui jinsi ambavyo movie industry za mataifa nyingine zinafanya kazi. Kabisa mtu anasema eti watu watengeneze movie waweke youtube 😂😂
 
Mkuu unazungumza vitu ambabyo wewe mwenye huvielewi, Huko majuu kuna watu wanatoa hata filamu 3 mpaka 4 kwa mwaka. Fatilia Nigeria na India utaelewa.

Wakamuangalie jamaa mmoja anaitwa hwang jeong min wa korea. Kuna kipindi mshikaji mpaka akawa anaulizwa mbona unaigiza filam nyingi kwani ugomvi?

Ilikuwa ni back to back. I don't know why people think muigizaji akitoa filamu nyingi sio sahihi
 
Tatizo la wabongo kila wanachokiona kinafanywa na wazungu wao wanahisi ndio u coolness, sasa Hollywood mtu akiekti filamu moja analipwa 30m $ ajichoshe kwa kipi kuekti mafilamu mengi?
 
😂😂😂 Nilicheka sana kumbe na ww uliona kuwa actor lazima uwe na leseni

Nilichoona hapa wengi hawajui jinsi ambavyo movie industry za mataifa nyingine zinafanya kazi. Kabisa mtu anasema eti watu watengeneze movie waweke youtube 😂😂

Wewe ndio huna ujuacho kuhusu filamu, huko Zile zinazowekwaga Youtube Netflix ni nini yako?
Nimeshakuambia wekeni mfumo Youtube wa kurusha matangazo ya filamu zenu, mnazubaa zubaa kwa ukilaza wenu
 
Bila shule hakuna utakachoigiza cha maana kwenye ulimwengu wa sasa zaidi ya vichekesho, futuhi, na vioja.

Labda useme ujuzi ndo watakuelewa ukisema Elimu what comes in their mind is bachelor degrees. Unaweza tu kujifunza mambo ya film kupitia platform mbali mbali kuongeza ujuzi, tasnia ya uigizaji inahitaji akili zisizo za kawaida
 
NI HITIMISHE KWA KUSEMA,
WAIGIZAJI VILAZA WANA ANDAA MUVI KWA AJILI YA VILAZA WENZAO. NI VIGUMU WASOMI KUINGIA HUKO KWANI WATALAZIMISHWA KUSHABIKIA CHAMA CHAO

99.jpg
 
Mkuu unazungumza vitu ambabyo wewe mwenye huvielewi, Huko majuu kuna watu wanatoa hata filamu 3 mpaka 4 kwa mwaka. Fatilia Nigeria na India utaelewa.
Wewe ndio huelewi, filamu zenu mnakurupuka hamfanyi tafiti zozote, hamjui kuhusu masoko ya sinema zenu ndio maana mnatoa sababu zisizo na kichwa wala miguu
 
Back
Top Bottom