Si nasikia huko sifa zao kuu n hizi
Uwe na tako
Uwe na mwonekano
Elimu walau ujue kusoma kuandika s muhimu Sana
Kwa mwanaume uwe handsome.
Nyingne n sifa za ziada tu
MKuu hivo vigezo vya urembo hata huko majuu pia hua vinapewa kipaumbele
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Si nasikia huko sifa zao kuu n hizi
Uwe na tako
Uwe na mwonekano
Elimu walau ujue kusoma kuandika s muhimu Sana
Kwa mwanaume uwe handsome.
Nyingne n sifa za ziada tu
Uliwahi kusoma chuo Mkuu?
Hivi unajua chuoni kuna kila aina ya fani? Kila aina ya watu?
Unadhani chuoni hakuna wenye vipaji vya kuigiza, kuimba, kucheza n.k?
Nayaelewa yote hayo mkuu, ila ninacho maanisha ni kua aliepasi vizuri darasani haimaanishi kuwa yeye ndie atakua bora, au alisoma chou haimanishi kua lazima yeye ndie atakua bora.
Hii falsafa ya kuamini Msomi wa chou kikuu ndio bora kwenye kila mahali fikra mbovu za kiafrica tunazokaririshwa. Kwa mantiki kama hiyo Tanzania tungekua katika nchi zilizoendelea duniani mana katika kila nafasi za uongozi zimejaa Maprofesa na Ma PHD, ila ndio wanaozidi kutuzamisha tu.
Naendelea kunukuu haya maneno
Ni muhimu kuheshimu UWEZO,hapa simaanishi elimu tu. Prof Kabudi ni zao la utafiti mzuri kuwa elimu bila akili ni sawa na choo bila mlango.
Anadhani Priyanka aliishia darasa la nane kama dada zake anaofanya nao kazi, hapo anataka kumfananisha Priyanka na Wema Sepetu kisa wote walikua maMiss, anashindwa kuangalia education backgrounds zao.
Industry ya Bongo haijawahi kufanya vizuri Budah, sema zipo baadhi ya Movie zilijitahidi, na hiyo ni kutokana na sababu kuwa kipindi hicho jamii ilikuwa gizani, wenye elimu walikuwa wachache, wenye Tv walikuwa wachache, Hapakuwa na Smartphone ambazo zingelinganisha kazi zetu na za kigeni.
Huoni mambo yamebadilika sasa, wewe darasa la pili utaigiza jambo gani kuifundisha jamii hii ya utandawazi zaidi ya vichekesho vyako?
Bila shule hakuna utakachoigiza cha maana kwenye ulimwengu wa sasa zaidi ya vichekesho, futuhi, na vioja.
Wewe unataja Movie zenye bajeti kubwa wakati kuna filamu za kizungu zenye bajeti ndogo kabisa zinafanya vizuri, angalia filamu za kifilipino hakuna bajeti ya kutisha lakini zinachezwa kitaalamu, angalia filamu za kikorea zipo nyingi tuu zina bajeti ndogo, na vifaa visivyogharimu pesa nyingi.
Kwa hiyo hao wanaofatilia ndio wameamua kuigiza utopolo licha ya kuwa wafuatiliaji?
Mkuu tunachozungumzia hapa, ni kuwa hata huo uwekezaji mdogo uliofanywa mbona hatuoni la maana?
Ndio nikasema shida shule ndogo kwa wasanii wengi na wahusika wa filamu.
Filamu nyingi zimelenga mambo ya kitoto.
Yaani Watu wazima wanaigiza kama watoto, kimama mama na kibaba baba bhana!!!!!!!!!!!!
Unaona usivyo na akili nzuri. Hivi kama mmeweza kuigiza filamu mnashindwa vipi kuajiri maafisa masoko wakuwasaidieni kutafuta soko, mnashindwa kuandaa hata matamasha ya bei rahisi kwa kuingia mikataba na wanamuziki?
Haya mmeshindwa kuanzisha YOUTUBE CHANNEL Maalumu kwa kutangaza movie zenu, mmeshindwa kuanzisha page maalumu kwa kazi hizo?
Mnashindwa na watafsiri Movie hamjiulizi wanasambazaje?
Kitu kikiwa bora huwezi pata shida kukisambaza, lakini kikiwa kibaya lazima uone shida kukisambaza.
Serikali unataka iwe sirius ili watu wapoteze vitumbua vyao?
Serikali ikiitambua Fani ya uigizaji itaweka vigezo lazima uwe na Diploma au degree moja unafikiri wangapi watabaki hapo?
Kisha watu wapewe leseni
Kuna yule mama anaact kama waziri, khaa yale ndio maisha ya waziri kweli? Si bora hata wangesema ni mfanyabiashara mkubwa basi ikatosha,
Wanasingizia bajeti, lakini wanakopeshana pesa hadi kutukanana matusi mazito mazito,
Hayo madanga wanayopasiana wanashindwa kuwaomba wawafadhili wafanye movie moja matata yenye story nzuri ya kusisimua,
Shida directors wao, producers wao, Editors wao, halafu ushikaji mwingi wanafanya kazi kimazoea sana.
Hapo ndio mnakosea, kuna muda sinema inatakiwa ikae sokoni lakini wewe kila miezi 3 unatoa filamu hapo unategemea nini
Ulisikia industry gani duniani kama kigezo cha uigizaji uwe na Diploma au Degree? ulsikia wapi duniani kuwa actor lazima uwe na leseni ? mbona unazungumza mambo ya ajabu mkuu?
Mkuu unazungumza vitu ambabyo wewe mwenye huvielewi, Huko majuu kuna watu wanatoa hata filamu 3 mpaka 4 kwa mwaka. Fatilia Nigeria na India utaelewa.
Wakamuangalie jamaa mmoja anaitwa hwang jeong min wa korea. Kuna kipindi mshikaji mpaka akawa anaulizwa mbona unaigiza filam nyingi kwani ugomvi?
Ilikuwa ni back to back. I don't know why people think muigizaji akitoa filamu nyingi sio sahihi
😂😂😂 Nilicheka sana kumbe na ww uliona kuwa actor lazima uwe na leseni
Nilichoona hapa wengi hawajui jinsi ambavyo movie industry za mataifa nyingine zinafanya kazi. Kabisa mtu anasema eti watu watengeneze movie waweke youtube 😂😂
Bila shule hakuna utakachoigiza cha maana kwenye ulimwengu wa sasa zaidi ya vichekesho, futuhi, na vioja.
Wewe ndio huelewi, filamu zenu mnakurupuka hamfanyi tafiti zozote, hamjui kuhusu masoko ya sinema zenu ndio maana mnatoa sababu zisizo na kichwa wala miguuMkuu unazungumza vitu ambabyo wewe mwenye huvielewi, Huko majuu kuna watu wanatoa hata filamu 3 mpaka 4 kwa mwaka. Fatilia Nigeria na India utaelewa.