Bongo mtu akistaafu ndiyo anaanza kufanya kazi

Bongo mtu akistaafu ndiyo anaanza kufanya kazi

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Tanzania tuna utaratibu wa kushangaza. Mtu akistaafu ndiyo anaanza kufanya kazi, tena kwa bidii na maarifa zaidi. Huko ughaibuni mtu akistaafu anaanza kusafiri kutalii. Anatulia akiburudika na michezo au hobby mbalimbali. Huku kwetu hali tofauti kabisa. Mtu akistaafu ndiyo kazi inaanza. Tena anakuwa anatamani astaafu haraka ili apige kazi kisawasawa.

Huu utaratibu una shida yeyote? Kuna haja ya kubadilika?
 
Mimi paka leo na shangaa akili za wtzania walio wengi, hawapendi kufanya kazi during their 'productive age' wa naona kukuepa kazi ni ujanja, mtu mzima kabisa ana kuambia bora niajiliwe serikalini kule ni kuzuri hamna kazi ni kukaa tu na kusubilia mshahara na marupurupu ya bure mengi, mtumishi anaingia ofisi anaacha koti lake kwenye kiti af anatokomea bar paka saa 8 mchana.

Wakati amesahau kwamba huo mda wakurelax bila kazi atakuja kuufidia tena kwa gharama kubwa, mimi mstaafu wa serikali hata akiangaika je simuonee huruma kabisa.
 
Nimeona wengi wakitaka kustaafu haraka wapate pesa zao 'Wakafanye kazi.' Wengi sana.

Basi unaishi bongo tofauti na hii tunaijua sisi, ukiona mtu kastaafishwa ujue kafanya kila namna imeshindikana kuendelea.

Matatizo ya kiafya ndo hustaafisha wengi kwa hiari.
 
Tanzania tuna utaratibu wa kushangaza. Mtu akistaafu ndiyo anaanza kufanya kazi, tena kwa bidii na maarifa zaidi. Huko ughaibuni mtu akistaafu anaanza kusafiri kutalii. Anatulia akiburudika na michezo au hobby mbalimbali. Huku kwetu hali tofauti kabisa. Mtu akistaafu ndiyo kazi inaanza. Tena anakuwa anatamani astaafu haraka ili apige kazi kisawasawa.

Huu utaratibu una shida yeyote? Kuna haja ya kubadilika?
Ukistaajabu ya wastaafu kufanya kazi kwa bidii utaona ya uteuzi. Hapa Bongo kuna watu wanastaafu na kisha kupata teuzi za kuongoza Bodi za Mashirika ya Umma.
 
Basi unaishi bongo tofauti na hii tunaijua sisi, ukiona mtu kastaafishwa ujue kafanya kila namna imeshindikana kuendelea.

Matatizo ya kiafya ndo hustaafisha wengi kwa hiari.
Sijui bongo uliyopo wewe. Lakini bongo hii wengi sana sikuhizi wanaopt 55yrs. Wengi wanasubiria kwa hamu kustaafu kwao.
 
Sijui bongo uliyopo wewe. Lakini bongo hii wengi sana sikuhizi wanaopt 55yrs. Wengi wanasubiria kwa hamu kustaafu kwao.

Kumbe unaongelea watarajiwa, hao wanaosubiria kwa hamu ni ile kudhani watakwapua fuba la mafao…. ila kiuhalisia wakishastaafu wengi hugundua kuwa hawakujiandaa kustaafu.

Mafao hayatoshi na huisha ghafla, ndo hao sasa unaona wanafanya kazi kwa bidii ili kubangaiza maisha yaliyobaki.
 
Social security za kibongo ni miserable yaani ndiomaana mtu akistaafu tu hachukui round anakufa, anakuwa na frustration, maisha duni, kuzungushwa hata kwa ile haki yake ambayo alitakiwa aipate nk.nk.nk. .kuna jamaa aliwahi kusema kustaafu bongo ni death penalt ndio maana kwenye maofisi vimajaa vibabu vilivyoongopa umri havitaki kustaafu. Kuna ofisi nilipita enzi zile kabla sijahama nchi yaani ni disaster mtu anayeambiwa hajastaafu ukimwangalia mpaka unamuonea huruma hata kutembea shida , bora angeongopa padogo basi loh mtu hadi amepinda.
 
Mimi hushangaa zaidi pale Luteni kanali mstaafu anapokuja kuteuliwa kuwa balozi wa tz marekani!....na wahitimu vyuoni wapo wengi wanasugua benchi mitaani na degree na masters zao,tena wengine wamehitimu pale chuo cha diplomasia...
 
Watu wanafanya kazi lakini hawashiki pesa, hela yote inabaki serikalini kama mafao yao ya uzeeni,yani haka kautaratbu kaserikali n kama ka mwajiri anaemlipa mfanyakazi Nusu ya mshahara ili aendelee kubaki kufanya kazi kwake maana hakuna mfanyakazi ataeacha kazi akat anakudai mshahara.

Mafao ni pesa ambayo ulidunduliza enzi za utendji kazi wako,ukija pewa zile hela unapewa zote kwa mkupuo Paap kama ni Mil.200 mzigo wote unapewa,mtu tangu anazaliwa hajawahi shika milioni 1 ya pamoja leo hii anapewa burungutu la 200M ,Kwann asianze kazi Upyaaa.

Wazee wengi hutimiza ndoto zao uzeeni ndio mana wenye pesa ma don wengi n wazee ktk nchi zetu hizi,chakufanya kuondokana na hili waajiriwa wangeondolewa hii ya NSSF sijui kila mtu akipewa chake apewe mzigo wake kama ulivyo 2m mpe mtu 2m yake nzima nzima,mambo ya kukatana katana haya ndio hupelekea haya ma vitu.
 
Na bado jiwe likataka kudhulumu mafao ya wastaafu.

Asante Sana Mungu.
 
Kibongobongo ukiona mtu anahangaika wakati wa kustaafu

1. Alikuwa anaponda starehe bila saving

2. Alikuwa mtumishi mtiifu kwa jamhuri yaani hana magendo ya kumpa pesa zaidi ya kutegemea mshahara

3. Alikuwa na majukumu mazito aidha ndio mkombozi wa ukoo au ndio wale wana watoto na wake kila mtaa hata saving ni shida

lakini hiyo akili ya kufanya kazi extra au kuwa na biashara unayoisema wengi huwajia wakishastaafu. Kinachotegemewa ni ajira
 
Elimu ya Msingi ingefupishwa,darasa la 7 hivi miaka 7 unasoma nini hapo shule, ishu ingeishia darasa la 5 Tu baada ya hapo mtu anadandia sec ambapo anapga 1 to 3 akitoka 3 anaruka Chuo anapgwa kule 3yrs Akmaliza hapo bado kijana mdogo anaanza kazi mapema anakusanya vyake kufika 40yrs anafunga hesabu maisha safi.

Ila hii ya kurefushiana elimu hiii kwanza tu unazeeekea darasani usiposhtuka kuwa elimu ya TZ inapoteza muda utatengeneza mitoto itayoanza kushika 1M ikiwa na miaka 35 ndio anamiliki 1m yake ya Kwanza.

Kuondoa hii kwanza elimu ifupshwe,ajira zitolewe kwa vijana watu kustaafu kazini mwisho iwe miaka 40 Kama n mafao apewe vyake afanye yake ila hii kupeana ajira wazeee ndio yale mtu anatumbuliwa ana miaka 65 anaanza leta Thread JF namna ya Kufuga kuku wa Mayai Hapo ana 65yrs,sijui hao kuku anawafugaje fugaje na miaka yake hiyo kuku wakifa wote bandani kazee ka watu kanajiparalaizia kenyewe tunaanza singizia n walio mtumbua kumbe shda n shock ya kuku wake wamekufa ghafla.
 
Kuna kizee kimestaafu kimekuja nunua kiwanja kule kwangu heka kama 20, kachimba kisima cha mashine,kajenga nyumba yake kubwa ya kuishi (in a month tu) maband ya mifugo yanaendelea kujengwa Hapa yupo analeta Kuku wake afuge yote hayo anahangaika mwenyewe hadi najiuliza Mshua hana watoto au hata mchepuko asimamie shoo zote hizo.

Hela za Uzeeni hizi mbaya sana,mafundi ni wanamwibia hadi sio poa maana kuna team ya mafundi sio chini ya 30 plus vibarua, kazi zinapgwa hapoo mzee ikifika jioni huyooo anajisepea huku nyuma watu n wanauza tu matofali kwa majirani Ila siku huyu mzee akijua matofali yake ndio yanajenga na kwangu Asipo paralaizi basi atajifia anajiona.

Hapo anakwambia nimestaafu nataka kupumzika zangu sasa, najiuliza we mzeee umestaafu unakuja nunua viwanja huku hata hatujapimiwa Siku MAMA aseme tusepe tutafute chocho mzee si utazezeteka wewe na mate juuu...
 
Back
Top Bottom