Nimeona wengi wakitaka kustaafu haraka wapate pesa zao 'Wakafanye kazi.' Wengi sana.
Mkuu hao huwaga hawana pa kutokea na barua zao za maombi yao ya kuongeza mkataba wa nyongeza kupigwa chini.
Maana mtumishi ukifika mchakato wake wa kustaafishwa kwa umri, kuna kada zingine huwa favor watumishi kwa kuwaongezea miaka miwili ya nyongeza.
Utaratibu huo inatakiwa mtumishi aandike barua kuomba kuongezewa, hapo kuna mawili, kukubaliwa ama kukataliwa kutokana na umuhimu wake, hasa ndicho waajiri wanachojali kubakisha mtumishi.
Sasa barua ikishagonga mwamba, ndiyo utasikia mtu akisema; "aaargh kazi yenyewe shachoka mie, waharakishe tu mafao yangu nikaanze shughuli zangu za maana".
Lakini kiuhalisia watumishi wengi hawatamani kustaafu kutokana na mazingira mabovu wanayokumbana nayo wastaafu bada ya kuwa nje ya mfumo.
Na hakuna mtu yeyote hata bungeni anayethubutu kuongelea madhila ya wastaafu na pensheni take home per month zao zilivyo kiduchu, haziwezi kuwakidhi hata maisha ya wiki moja.
Sasa hapo kwanini mtu asigwaye kustaafu na akistaafu lazima apige kazi kuziba mapengo?