Boniface Jacob: Bunge limedanganya kuhusu elimu ya Nape Nnauye

Boniface Jacob: Bunge limedanganya kuhusu elimu ya Nape Nnauye

Hawa wanasiasa wa CCM, ni nani anafanya vizuri katika siasa? Goli la mkono ndiko kufanya vizuri katika siasa.

Tunaongozwa na failures na majizi ndiyo maana nchi haiendi popote.
Kama ni rahisi na wewe funga Goli la mkono 😄
 
Butimba TTC

Kuna wakati mama Gaudensia Kabaka Mwenyekiti mstaafu wa UWT alikuwa mkuu wa Chuo pale

Private Candidate hufanya Mitihani popote pale usiteseke sana Boniyai [emoji23]
Sasa na wewe unapocomenti uwe na uhakika kama alifanya kama Private Candidate au School Candidate na kama ni Private Candidate je Butimba imesajiliwa na NECTA kama PC Centre? Yaani uwe na jibu linaloeleweka kama huna katafiti kwanza mkuu
 
NAPE KALIDANGANYA BUNGE KUHUSU ELIMU YAKE.

Katika kufanya Utafiti wangu kuhusu mapitio (background) ya elimu ya Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya habari Bw.Nape Moses Nnauye

Nimeshtuka kuona Bunge linatangaza Waziri Nape Moses Nnauye amepata Elimu ya ADVANCED CERTIFICATE OF SECONDARY SCHOOL katika shule ya BUTIMBA TCC mwaka 1998 hadi mwaka 2000.

Nimelazimika kuwatafuta Walimu wenzangu waliosoma na kufanya kazi BUTIMBA TCC (Butimba teacher's college).

Wameshangaa na kushtushwa na taarifa ya Bunge inayohusu elimu ya Waziri Nape Moses Nnauye.

Ukweli ni kwamba BUTIMBA TCC haijawahi kuwa na shule ya Sekondari mwaka 1998 wala katika tovuti ya Baraza la Mitihani Tanzania alijawahi kusajili Shule ya Sekondari na kuipa mitihani mwaka 1998 hadi 2000 kwa Jina la "BUTIMBA TCC SECONDARY SCHOOL"

BUTIMBA TCC (Butimba teacher's college) ilianzishwa mwaka 1939 na wakoloni na Kujengwa shule ya msingi ya mazoezi (Teaching Practice) na wakoloni wenyewe kwa ajili ya mafunzo kwa Vitendo kwa Wanafunzi wa Ualimu.

Hata hivyo 28 January 2000 serikali ilianzisha shule mpya ya sekondari (Kutwa) ya BUTIMBA SEKONDARI SCHOOL (BUTIMBA DAY) ambayo kidacho cha Kwanza waliingia mwaka 2000 na Kumaliza mwaka 2003 kidato cha nne.

Ambapo kwa mujibu wa tovuti ya Bunge Nape alikuwa ameshamaliza kidato cha 6 Mwaka 2000 latika Shule ya Sekondari ya BUTIMBA TCC.

Lakini kubwa zaidi inaonyesha Nape Moses Nnauye hakusoma BUTIMBA TCC elimu ya kidato cha kwanza hadi cha nne bali alisoma kidato cha tano na cha sita katika Shule ambayo haipo wala haijawahi kuwepo.

Pichani ni tovuti ya Bunge kuhusu elimu ya Nape Moses Nnauye,Picha ya Pili ni kuhusu usajili wa Sekondari wa Butimba Day mwaka 2000.

Naomba kuwasilisha.

NAMALIZIA UTAFITI kuhusu Shahada ya Sheria pale OPEN UNIVERSITY OF TANZANIA anayosoma Nape Moses Nnauye.

Imewezekanaje mwanafunzi aliyekosa qualificayion za Direct Entry za
1."Principal mbili" za ADVANCED CERTIFICATE OF SECONDARY SCHOOL ..?

2. Credit mbili za O-level ( History na English language Kusoma Sheria kinyume na Kanuni za TCU..?

3. au Mwanafunzi aliyekosa Equivalent qualifications za Diploma yenye G.P.A yenye 3.0 and above anawezaje kujiunga na Shahada ya sheria..?

Au mtafuta kuwapa lawama LAW SCHOOL OF TANZANIA..,

( Kaka ana madiploma Mengiiiiiiiii lakini hayana uzito)

4. au Bachelor degree kutoka Chuo kinachotambulika na TCU...? Siyo kama BANGALORE UNIVERSITY YA INDIA 😂😂😂

La sivyo TCU mtuambie mtu akiwa CCM au Kiongozi wa Serikali Vigezo vya Kujiunga na elimu ya Juu kwake havizingatiwi sawa na Watanzania Wengine..?
View attachment 2841228View attachment 2841229
Screenshot_20231213_130924_Samsung Internet.jpg



Nashauri
Ya kwanza iungwe isome moja kwa moja kwenye mifumo ya TCU
Ya pili isome kwenye mifumo ya NACTE
Ya tatu isome kweny system za NECTA
 
Tatizo chadema ni wajinga sana. PC wamefanya pale mitihani, kuna kituo cha mitihani. Wakati tunasoma pale chuo na Mh Waziri Mkuu Majaliwa, wapo watu walikuwa wanafanya mitihani pale ya ACSEE. Aache ujinga, huo muda akafanye mazoezi apungue.
 
Maisha ya hapa duniani hayana kanuni unakuta MTU mwenye CV kubwa yupo mtaani ni bodaboda na kilaza yupo kwenye V8 anakula maisha.
Sometimes hakuna haja ya kuumiza Sana kichwa juu ya maisha ya wengine
 
Sasa na wewe unapocomenti uwe na uhakika kama alifanya kama Private Candidate au School Candidate na kama ni Private Candidate je Butimba imesajiliwa na NECTA kama PC Centre? Yaani uwe na jibu linaloeleweka kama huna katafiti kwanza mkuu
Boniyai ndio amfanyie Utafiti

Very simple 😂
 
Tunajiumiza vichwa bure! Utaratibu wa Chama chetu, ni kuwa, sifa mojawapo ya kugombea U Rais, ni lazima uwe na japo Digirii moja. Na hiyo sifa, ilimkimbiza mzee wa Kiraracha, Mrema.
Sasa jee, huyu Rais wetu, wakati anaukwaa U Rais, alikuwa na Elimu hiyo?
Gari linakwenda, tushukuru tunasafiri salama tu!
Sifa ya mgombea uraisi kuwa na degree ipo kwenye latina au kitu gani? Ni sheria gani hiyo inayomtaka mgombea uraisi awe na degree?
 
Tatizo chadema ni wajinga sana. PC wamefanya pale mitihani, kuna kituo cha mitihani. Wakati tunasoma pale chuo na Mh Waziri Mkuu Majaliwa, wapo watu walikuwa wanafanya mitihani pale ya ACSEE. Aache ujinga, huo muda akafanye mazoezi apungue.
Mkuu hebu acha uongo bhna nimefanya kazi maeneo hayo ya Butimba Miaka hiyo Nape anayosema kulikuwa na Secondary..Kiukweli ilikuwepo Shule ya Msingi Butimba ambayo ilikuwa ikitumika kama shule ya mazoezi ya Walimu..

Secondary imeanzishwa mwaka 2000 ..
 
Back
Top Bottom