Boniface Jacob: Rais Samia tunaomba Afande Mafwele anayetuhumiwa kumteka Sativa achunguzwe

bro nakuelewa taarifa zako zinatosha kumhukumu
 
Ataendaje underground na ameshaumia sana.

Na Waziri Masauni kasema wenye ushahidi wa kutosha juu ya matukio wapeleke.

Na hii ndio njia sahihi.

Akienda Undergound atapotea tena. Lakini sasa akipotea tutajua nani mhusika na kwanini.
Waziri Masuni kasema wenye ushahidi wa kutosha juu ya matukio wapeleke ati?

Kuna watu wamesomea na wana ubobezi wa kufanya kazi hii.
Akiyetekwa na kunusuruka kuuawa uchunguzi hautofanyika hadi mtu mwenye ushahidi apeleke?

Lisssu alishambuliwa akaambiwa àende akalisaidie jeshi kwenye uchunguzi, mzee huyu aliyetekwa na kuuliwa Masauni anatamani kama askari wake amwambie marehemu aende akasaidie upelelezi, kama wenye dhamana wameshindwa
 
Mbali na copy and paste huwezi kusema chochote mkuu britanicca kuhusiana na huyo mtu ?
Hata mwaka 2017 kwenye kesi ya Bilionea MSUYA shahidu Shaibu Said (Mredii), alidai mahakamani kuwa alipelekwa Kituo cha Polisi kinachoitwa Guantamano, nje kidogo ya Jiji la Arusha na kuteswa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani.

Shahidi Mwingine alisema alifungwa tofari sehemu za siri kwa amri ya Mafwele
 
Huyo jamaa inaelekea ni katili sana kwenye uhai wa watu
 
Dah!...Tz pia kuna Guantanamo?
 
Mi nahisi hata huyu anayeitwa shetani ni huyu huyu Mafwele sema hatujuagi tu...
 
Duuu huko mbinguni sijui atakuwa na nafasi ipi. Atakuwa ameua watu wengi sana kama hii taarifa ni ya ukweli.
Unaongelea mbinguni..muulize watoto na ndugu zake wako salama vipi kwa kazi hizi anazofanya? Binadamu mwenye akili ya kawaida kabisa ukimtoa Mungu wanaofuatia kwenye umuhimu ni watoto na wazazi..inakuwaje huwezi tambua matendo yako yana direct connection na future ya unaoamini ndio wanakufanya unahangaika wapate maisha mazuri?
 
Kijnaa amekubali kupambna na mtu anaye tuhumiwa kuua na kuteka Watu ajulikanae kama Mafwele, dogo ameamua kumrarua na kumjeuza kama chapati bwana Mafwele, sativa anajuwa na NKutambua kuwa Mafwele ndie aliye mteka na kumuumiza vibaya

Hyo ni email iliyo kwenda chuo anacho soma bint ake faith j mafwele
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…