Boniface Mwabukusi aapishwa kuwa Rais wa TLS. Aanza kazi rasmi

Boniface Mwabukusi aapishwa kuwa Rais wa TLS. Aanza kazi rasmi

Kongole sana wakili msomi Boniface Mwabukusi kwa kuchaguliwa kuwa rais wa TLS kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2024 hadi 2027

Kuchaguliwa kwako wakili Boniface Mwabukusi kunaendana pia na TLS kuwa mdau mkubwa kuwa mtazamaji (observer) wa chaguzi za Serikali za Mitaa na Vijiji 2024 na uchaguzi mkuu wa 2025 ambapo TLS itahakiki mchakato mzima wa chaguzi hizo za kitaifa 2024 / 2025 ziwe huru, za kidemokrasia na haki kwa wote Tanzania .
 
Wakili Mwabukusi aapishwa rasmi kuwa Rais wa chama cha Wanasheria Tanganyika.
View attachment 3060504
Wakili Boniface Mwabukusi ataendesha chama cha Wanasheria Tanganyika kwa Miaka mitatu.

Uapisho huo umefanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.

Wakili Boniface Mwabukusi alitangazwa kuwa Mshindi wa Urais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) akiwashinda Wanasheria wengine watano waliokuwa wakiwania nafasi hiyo
View attachment 3060503
Mwabukusi alishinda kwa Kura 1,274 huku Sweetbert Nkuba aliyekuwa akipewa nafasi kubwa ya kushinda akifuatia kwa Kura 807. Kwa matokeo hayo, Mwabukusi anakwenda kukiongoza Chama hicho cha Wanasheria kwa kipindi cha miaka mitatu.
View attachment 3060509
Mawakili wengine waliokuwa wakiwania nafasi hiyo ni Kapt. Ibrahim Bendera aliyepata Kura 58, Paul Kaunda aliyepata Kura 51, Emmanuel Muga aliyepata Kura 18 na Revocatus Kuuli aliyepata Kura 7

Pia, soma; Wakili Sweetbert Nkuba kupinga ushinda wa Wakili Boniface Mwabukusi kuwa Rais wa TLS
Hongera sana Mwaisa Mwabukusi kwa ushindi huu mnene. Mungu akubariki sana na akuongoze kwenye kazi yako ya kuwatumikia watanzania.
 
Hivi walishabadilisha mda wa kuongoza TLS kutoka mwaka mmoja mpka mitatu?
 
The state imempata mtu wao kwa strong hold aka push ajenda ya katiba mpya ambayo aliepewa jukumu hilo kaweka mpira kwapani kwa kutaka kuchaguliwa tena!

Kudos the state!
 
Kuna mtu saa hizi vitu vinagonga chupi vinarudi ndani maana Watanganyika wachache tu wameonesha mfano huo, je wale wengi nao siku yao ya kufanya maamuzi ikifika itakuwaje? Mungu ibariki Tanganyika.
 
Kula la kheer.. Simamia kwenye haki na maadili. Msimamo wako usiyumbe kama baadhi ya walio pita...
 
The state imempata mtu wao kwa strong hold aka push ajenda ya katiba mpya ambayo aliepewa jukumu hilo kaweka mpira kwapani kwa kutaka kuchaguliwa tena!

Kudos the state!
Well hawajafika mahali, this time wame plan vibaya. Even state makes mistakes
 
Back
Top Bottom