Hongera sana Mwaisa Mwabukusi kwa ushindi huu mnene. Mungu akubariki sana na akuongoze kwenye kazi yako ya kuwatumikia watanzania.Wakili Mwabukusi aapishwa rasmi kuwa Rais wa chama cha Wanasheria Tanganyika.
View attachment 3060504
Wakili Boniface Mwabukusi ataendesha chama cha Wanasheria Tanganyika kwa Miaka mitatu.
Uapisho huo umefanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.
Wakili Boniface Mwabukusi alitangazwa kuwa Mshindi wa Urais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) akiwashinda Wanasheria wengine watano waliokuwa wakiwania nafasi hiyo
View attachment 3060503
Mwabukusi alishinda kwa Kura 1,274 huku Sweetbert Nkuba aliyekuwa akipewa nafasi kubwa ya kushinda akifuatia kwa Kura 807. Kwa matokeo hayo, Mwabukusi anakwenda kukiongoza Chama hicho cha Wanasheria kwa kipindi cha miaka mitatu.
View attachment 3060509
Mawakili wengine waliokuwa wakiwania nafasi hiyo ni Kapt. Ibrahim Bendera aliyepata Kura 58, Paul Kaunda aliyepata Kura 51, Emmanuel Muga aliyepata Kura 18 na Revocatus Kuuli aliyepata Kura 7
Pia, soma; Wakili Sweetbert Nkuba kupinga ushinda wa Wakili Boniface Mwabukusi kuwa Rais wa TLS
Hilo ni pandikizi la CHADEMA huko TLS. Huo ndo uchaguzi pekee intelijensia ya CHADEMA imeshinda.Mungu mbariki mtu huyu
Mawakili wanajitambua.
Kishaliwa huyoSasa yule aliekwenda mahakamani itakuwaje😂
Kuna Siku moja TANGANYIKA itarudi kwetukumbe ni chama cha Wanasheria Tanganyika. na siyo Tanzania
We unawaza kiu dini dini tu nyakati zote? Uko sawa kweli mkuu, au changamoto afya ya akili?!.KAKAMATA NINI MKONO WA KUSHOTO?
Wanajua muda si muda jamaa atawafurusha ulaji wao.Mbona waapishaji kama hawajachangamka??
Umma haujawahi kushindwa kitu chochote kile pale unapoamua jambo lake.Pamoja na figisu zote, bado ameshinda!! Pongezi nyingi kwake.
Rufaa yake itaendelea kama kawaida ili wajuba wazipige hela zake zisizokuwa na kazi ya maana.Kwa kuwa ameapishwa yule msukuma wakili Nkuba rufaa yake ya kupinga matokeo itakuwaje sasa?
Akapige kazi, aanzie na suala la Upatikanaji wa Katiba Mpya hapa Tanzania.
Well hawajafika mahali, this time wame plan vibaya. Even state makes mistakesThe state imempata mtu wao kwa strong hold aka push ajenda ya katiba mpya ambayo aliepewa jukumu hilo kaweka mpira kwapani kwa kutaka kuchaguliwa tena!
Kudos the state!