Boniface Mwabukusi ashinda kesi dhidi ya Tanganyika Law Society. Ruksa kugombea Urais wa Chama hicho

Boniface Mwabukusi ashinda kesi dhidi ya Tanganyika Law Society. Ruksa kugombea Urais wa Chama hicho

Huyu Jamaa ni mzalendo wa kweli Tanzania sema watu kama hawa hawatakiwi wanatakiwa wale wahuni wahuni mara leo utasikia tutashinda hata kwa goli la mkono..
 
Pollonium,hata kwa eti?

Polonium (High radioactivity, high lethality) is a highly radioactive heavy metal. It is arguably the most lethal known material. Although it has some minor industrial uses it is best known for links with possible assassinations. It is also used to produce neutrons in the core of nuclear weapons.
 
Wadau washindwa kujizuia kufanya Shamrashamra na sura nyingi zilizojaa tabasamu baada ya mfumo onevu uliojikita ndani ya TLS kushindwa kumnyima haki mgombea kupitia hukumu iliyosomwa leo na jaji wa mahakama kuu....
 
Kesi ya Boniface AK Mwabukusi kupinga kukatwa kwenye Uchaguzi wa Rais wa Tanganyika Law Society kutolewa hukumu leo pale Mahakama kuu ya Tanzania

Jumaa Mubarak 😃

----
Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam leo, Ijumaa Julai 26.2024 imetoa hukumu ya kesi iliyokuwa imefunguliwa na Wakili wa kujitegemea Boniface Mwabukusi dhidi ya TLS (Chama cha Mawakili Tanganyika) ambapo Wakili Mwabukusi alikuwa anapinga maamuzi ya kamati ya rufani kumuengua kugombea nafasi ya Rais wa chama hicho katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mapema mwezi ujao.

Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili Mahakama imeridhika na hoja zilizotolewa na upande wa Mwabukusi ambapo sasa rasmi imetengua maamuzi ya kamati ya rufani ya TLS, hivyo kwa sasa Wakili Mwabukusi amerejeshwa kugombea nafasi ya Rais wa TLS.

Pia soma
Kuna watu wanalindwa na MUNGU Ila CCM haishindwi kwenye hizi sarakasi & vice versa is True
 
1000028361.jpg
 
Back
Top Bottom