MBINGU ZIMENIRUHUSU KUSEMA
Baada ya kimya cha muda mrefu, hatimaye ibada ya Sabato ya leo nimesikia sauti ya ujumbe wa Mungu ikisema;
"Fili mi loqui ad salvandum populum meum"
(Mwanangu zungumza watu wangu wapone..)
Hivyo kesho, Jumapili, saa 6 :00 mchana, natarajia kuzungumza na viongozi wa CHADEMA Kanda ya Pwani pamoja na vyombo vya habari kuhusu hali ya siasa ndani ya chama na nje ya chama.
Waandishi wa habari wote mnakaribishwa. Mkutano utakuwa mubashara (live) kupitia akaunti za mitandao ya kijamii na YouTube pia.
"Hufunua mambo ya ndani ya gizani, na kuyaleta nuruni yale yaliyositirika sana." - Ayubu 12:22