Bookworms of JF, what's your favorite book (s) and why?

Paula Paul, nyumba ya kuishi ni liability, lakini hiyo haimaanishi kwamba watu wasiwe na nyumba za kuishi.

Shida ya masikini tuliowengi ni kuwa tunatumia jasho na damu kununua luxuries na liabilities... Ili upige bao fasta unatakiwa kutumia assets kununua luxuries.

Your job is not an asset kwa hiyo kutumia mshahara kujenga nyumba ya kuishi sio sahihi, Wengi huwa wanapinga hili..

Swali lako kwamba unafamilia na kupanga utajibana, unaanzaje kujenga nyumba ya kupangisha sijalijibu, kwa sababu inategemea na hali ya mhusika, kipato, ukubwa wa familia na mazingira mengine...

Lakini naomba nikujibu kifupi tu, jenga hiyo nyumba ya kuishi, kama ulivyosema kidogo kidogo huku tayari umeshamia ili kukwepa gharama ya pango, ikishakamilika, hama halafu ipangishe, wewe nenda kapange, si tayari unakuwa umeshaweza?

Mimi nadhani ni rahisi tu, lakini wengi tunataka ule ufahari kwamba, NINATOKEA KWANGU, ninaishi kwenye nyumba yangu, hata kama hakuna tija yeyote..

Mkuu kama kuna hoja nimesahau kuijadili nikumbushe..
 
Nimemwelewa sana alipose sisi wanaume we are sexual by nature and you are emotional by nature. She says a woman is a woman. You are different but inside you operate the same.

Hicho cha why men love bitches sijakisoma nippasie ukikipata.
Bila shaka hakifundishi wanawake wote waanze kufanya kama .... Ili wapendwe.
Nikimaliza ninachokisoma sasa hivi nitakuwa nasoma hiki page 5 kila siku hadi kiishe.
 

Attachments

Ni kweli kuna vitabu ukinunua ukivisoma unaweza usimalize au ukimaliza usitamani kuvitizama tena.

Nadhani miongoni mwa hobbies zangu Kusoma vitabu ni namba moja.
Kuangalia movies ni namba mbili.
Kusikiliza music ni namba tatu.
Asante kama umeona vinachangamsha akili Nowonmai.
 
Nimecheka😊😊😊.
Mwenye power yake haitumii vizuri, hadi anakupa muda wa kusoma vitabu hadi nyumbani?

ASOIAF ipo hadi book ngapi? Hivi ni vizuri kusoma kabla ya kuwatch show au baada?
Wewe umesoma wakati gani?
Nasikia kina mambo ambayo kwenye show hayapo lakini kwenye vitabu hapo.
Nilisoma book one nikaweka kando. Nishawishi na Mimi.
 
Hahahaahaaa!
wanataka kuwa Kalumekenge au sio?

Kabla sijasahau, umesema asilimia kubwa ya waliopitia shule wana vipato vikubwa na wengi wanalipwa mishahara mikubwa, hapa ndio tatizo lilipo:

Wanalipwa mishahara mikubwa na kipato kikubwa lakini bado wana struggle financially, why? Ndio ubovu wa hiyo formal education.

Mtu kafanya kazi muda mrefu lakini akitumbuliwa anataka kujinyonga, why? Ndio ubovu wa formal education.

Mtu kafanya kazi hadi umri wa kustaafu umefika lakini anaomba kuendelea kufanya kazi, why? Ndio ubovu wa formal education.

Mtu kafanya kazi hadi kastaafu, lakini ana maisha magumu na pensheni yake wanamzungusha tu, why?

Kama wewe unapenda kuwa muajiriwa maisha yako yote hadi uzeeni unaamka asubuhi kwenda kazini, formal education inakufaa,

Kama ni vinginevyo, ongezea na mengine nje ya syllabus.
 
Asante Mjuni.
Nivumilie kidogo.
Kipindi nimesoma chuo nilisoma haya mambo.
1. Namna ya kuandaa business plan.
2. Namna ya kuchagua Business Idea.
3. How to start a business.
4. Namna ya kupata startup capital
5. Kuikuza biashara hapa nilisoma naweza nikatumia (loan/debt au Equity Capital).
6. Kufanya research ya eneo ninalotaka kufungua hiyo biashara, ili kujua wateja wangu watakuwa ni wakina nani.
7.
8.
9
10.
Ni mengi ambayo siwezi kuelezea.

Ain't these enough kufungua biashara yangu mwenyewe?

Nikasoma pia namna ya kumanage hiyo biashara.
Mambo ya accounting.
Mambo yote ambayo nimeyasoma kwenye vitabu nimeyasoma darasani.

Sasa kama nimefundishwa kwanzia kuwa na business idea, kuandaa business plan, hadi sehemu ninayoweza kupata capital, na pia namna ya kuwa na nidhamu ya fedha kweli haya yote wameniandaa ili ni ajiriwe?.
Ni kitu gani au elimu gani tena nahitaji ili kuanzisha biashara yangu mwenyewe? Capital?

Hebu nieleweshe zaidi Mjuni, natamani kuelewa sana.
 
Ukitaka kutekeleza hayo mambo uliyofundishwa, utajikuta umekwama kwenye "analysis paralysis" bila kuchukua hatua yeyote,

Na ukija kufanikiwa kuchukua hatua, utafail, utakimbia na kusema biashara ni ngumu, utaenda kutafuta ajira.
Sasa hivi nakuja kuelezea ni kwa nini.
 
Kalumekenge ni nini Nowonmai?
Hapa Mjuni ndio aelezee vizuri kwa sababu mimi ni naamini kama wewe. Kwamba elimu ni kila kitu.
Unaweza kuwa na hela pia ukahitaji ma expert wakufanyie kazi zako na watakwambia kaa kimya Mimi ndio nina ujuzi na hili.
Lakini hili pia " this Kiyosaki " anaona pia ni sawa na kutishia kwamba waliofeli shule ndio wanaajiri waliofaulu.
Yupo mtu mmoja humu kama sijakosea anaitwa "Khan " alisema huyu Robert Kiyosaki anaweza kukufanya ukaidharau degree yako.
Na ndivo vijana wanavofanya, wa natamani ada waliolipia shule wangepewa wafungue biashara.
Lakini jee, Kiyosaki hajasoma ?
Reginald Mengi haja soma?
Bilget haja soma?
 
Hapana haujasahau hoja yoyote.
Na nashukuru kwa namna unavyoelezea kwa moyo wote. Na ninakiri kuelewa.

😊😊Mimi ni miongoni mwa watu tunapenda title ya "mama mwenye nyumba'' nadhani hii concept ya huyu jamaa hainifai.

Asante Sana Mjuni nakiri kuelewa.
 
Paula Paul, naendelea kujadili post yako namba 836.

Pale juu nilisema kuwa darasani inakosekana financial education,

Financial education ni pana sana kushinda formal education, kwa maana ya academic na professional(can you believe this?)



Elimu imegawanyika ktk makundi makuu manne, yaani inatakiwa kucover sehemu kuu nne:
1)physical
2)mental
3)emotional
4)spiritual

Formal education ina deal na namba 2) tu, mental, ilihali financial inatakiwa emotional na spiritual,

kwa hiyo iĺi uweze kupata financial education, lazima uwe prepared emotionally na spiritually, otherwise utakimbia tu.

Hii mada ina mambo mengi sana, hadi hapa inabidi nistop, ili nione kama sijapuyanga nje ya hoja.
 
Asante, nasubiri sababu kwa hamu.
 
You are appreciated Mjuni..
Nilikuwa nataka niongeze maswali ila pia kwa tuliyoyajadili I am grateful.
Nina imani kuna siku tutakutana hapa na nitakuwa maswali yangu. Nimeweka alama tulipoishia.

Hats off to you.!
 
Asante, nasubiri sababu kwa hamu.
#842 inaendelea,

Mwanzo kabisa ulisema kampuni za kiyosaki zilifirisika, hiyo ndio emotional na spiritual(mtaniwia radhi, sijui kufundisha, hadi mwenyewe nimejicheka).

Shuleni tunafundishwa kuwa kufail ni jambo baya na unachapwa ukifail, huku kwenye bussness kufail siyo jambo baya, ni ni vizuri ukifail, there is a saying in aviation "you havent crushed until you have crushed, until then, keep flying the plane"

Wakuu kesho, naona kabisa sieleweki, sijui usingizi!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…