Bora kuolewa na mzee aliyejipanga kimaisha kuliko kuolewa na kijana maskini mwenzio

Hizi kauli zipo miaka dahali iliyopita lkn tinashuhudia ndoa zikiingia shimoni kila siku.

Njaa ya tumboni hupofusha akili, upendo na imani (jisomee kuhusu hili. Utanishukuru).
 
K Lyn yamemtokea yapi!!!?? Nnachofahamu ni ule wosia aliodai ni wa marehemu ndo umekataliwa ila urithi wa wanae upo pale pale kwa kuzingatia mgao sawa kwa wote.
Ndiyo ushangae Sasa. Kuna wasiofuatilia mambo humu wanasema ametoka bila bila.
 
Bustani ya Eden iliyokuwa na kila kitu.
Kwani bustani ilikuwa yake? Mbona walifukuzwa sasa!?
Eva na Adamu walianza mwanzo kabisa wakiwa hawana kitu na hata baada ya kufukuzwa bustanini walienda huko duniani kuyaanza maisha upya wakiwa pamoja.
 
Ilikuwa yake ni ujinga wake tu ndio ulimponza, hivyo ikabidi apambane na hali yake.
 
Vipi na wanaume tukiweka mgomo wa kuoa wanawake maskini, mtatoboa kweli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…