Bora kuolewa na mzee aliyejipanga kimaisha kuliko kuolewa na kijana maskini mwenzio

Bora kuolewa na mzee aliyejipanga kimaisha kuliko kuolewa na kijana maskini mwenzio

Unaweza kumpata mwenye hizo pesa na zikawa chungu kuliko shubiri.

Bora umpate anayekupenda.

Anayekupenda atakuvumilia, hata hesabu mabaya yako, atakuamini na haya ni muhimu sana.

Kumtegemea mtu mwingine kiuchumi hata kama ni mume wako ni jambo baya mno.
Hizi kauli zipo miaka dahali iliyopita lkn tinashuhudia ndoa zikiingia shimoni kila siku.

Njaa ya tumboni hupofusha akili, upendo na imani (jisomee kuhusu hili. Utanishukuru).
 
K Lyn yamemtokea yapi!!!?? Nnachofahamu ni ule wosia aliodai ni wa marehemu ndo umekataliwa ila urithi wa wanae upo pale pale kwa kuzingatia mgao sawa kwa wote.
Ndiyo ushangae Sasa. Kuna wasiofuatilia mambo humu wanasema ametoka bila bila.
 
Bustani ya Eden iliyokuwa na kila kitu.
Kwani bustani ilikuwa yake? Mbona walifukuzwa sasa!?
Eva na Adamu walianza mwanzo kabisa wakiwa hawana kitu na hata baada ya kufukuzwa bustanini walienda huko duniani kuyaanza maisha upya wakiwa pamoja.
 
Kwani bustani ilikuwa yake? Mbona walifukuzwa sasa!?
Eva na Adamu walianza mwanzo kabisa wakiwa hawana kitu na hata baada ya kufukuzwa bustanini walienda huko duniani kuyaanza maisha upya wakiwa pamoja.
Ilikuwa yake ni ujinga wake tu ndio ulimponza, hivyo ikabidi apambane na hali yake.
 
Maisha yetu ni mafupi sana hapa duniani, hivyo tunapaswa kufurahia maisha muda wote. Hii habari ya kuoana na mtu eti mchume wote baadaye mtafurahia maisha haikubaliki. Maana hakuna aliye na mkataba na Mungu, unaweza ukafa the next morning.

Na kwa taarifa yako furaha na umaskini havikai pamoja, ni kama maji na moto. Ukiolewa na maskini maana yake ni kwamba umeipiga teke furaha ktk maisha yako. Asikwambie mtu, pesa ndiyo sabuni ya roho.

Kama huna hela utalala sehemu yenye uvundo kama banda la beberu la mbuzi. Huyo mume wako maskini anakuwa amelala huku akikoroma maana amechoka utadhani yuko ICU (ndiyo maana ya mlalahoi). Mate
yanamtoka na kulowesha godoro unaweza kudhani kakojolea.

Utajikuta tu unaamka na kuanza kulia kwa uchungu huku ukimuuliza Mungu; why me? Maisha haya mpk lini?

Na kuna ndharia mpya kuwa maskini hatauona ufalme wa Mungu. Kwasabb kila siku anatenda dhambi ya manung'uniko. Maskini hana shukurani kwa Mungu wake. Kila siku akijisogeza mbele za mola wake anaorodhesha maombi zaidi ya mahitaji yake kwa Mungu. Lkn tajiri kila siku anamtukuza na kumshukuru kwa hatua aliyopiga. Ndiyo maana hisikii tajiri akiangushwa na pepo wachafu.

Umaskini ni ugonjwa. Kwann ? Umaskini husababisha magonjwa ya kizembe na kupelekea mtu kufa kizembe.

Usikubali kuolewa na maskini.
Vipi na wanaume tukiweka mgomo wa kuoa wanawake maskini, mtatoboa kweli?
 
Back
Top Bottom