Bora kuolewa na mzee aliyejipanga kimaisha kuliko kuolewa na kijana maskini mwenzio

Bora kuolewa na mzee aliyejipanga kimaisha kuliko kuolewa na kijana maskini mwenzio

Maisha yetu ni mafupi sana hapa duniani, hivyo tunapaswa kufurahia maisha muda wote. Hii habari ya kuoana na mtu eti mchume wote baadaye mtafurahia maisha haikubaliki. Maana hakuna aliye na mkataba na Mungu, unaweza ukafa the next morning.

Na kwa taarifa yako furaha na umaskini havikai pamoja, ni kama maji na moto. Ukiolewa na maskini maana yake ni kwamba umeipiga teke furaha ktk maisha yako. Asikwambie mtu, pesa ndiyo sabuni ya roho.

Kama huna hela utalala sehemu yenye uvundo kama banda la beberu la mbuzi. Huyo mume wako maskini anakuwa amelala huku akikoroma maana amechoka utadhani yuko ICU (ndiyo maana ya mlalahoi). Mate
yanamtoka na kulowesha godoro unaweza kudhani kakojolea.

Utajikuta tu unaamka na kuanza kulia kwa uchungu huku ukimuuliza Mungu; why me? Maisha haya mpk lini?

Na kuna ndharia mpya kuwa maskini hatauona ufalme wa Mungu. Kwasabb kila siku anatenda dhambi ya manung'uniko. Maskini hana shukurani kwa Mungu wake. Kila siku akijisogeza mbele za mola wake anaorodhesha maombi zaidi ya mahitaji yake kwa Mungu. Lkn tajiri kila siku anamtukuza na kumshukuru kwa hatua aliyopiga. Ndiyo maana hisikii tajiri akiangushwa na pepo wachafu.

Umaskini ni ugonjwa. Kwann ? Umaskini husababisha magonjwa ya kizembe na kupelekea mtu kufa kizembe.

Usikubali kuolewa na maskini.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] poleni sana watoto wa kike, wewe ni tajiri au masikini???? Ulisikia wapi tajiri akawa na masikini wakaoana, mnakutana wapi???
Alafu acha kudanga umri umeenda tafuta kijana mwenzio olewa mpambanie maisha yenu.....!!!! Tofauti na ivyo jiandae kuteseka
 
Mtu anaeongea haya baba yake na uzee wote hajatoboa maisha anataka aolewe na kijana wa 28 akiwa ana mafanikio akili za kuwazia tundu la buza.
Alitakiwa aseme bora kuolewa na mume wa mtu mwenye pesa kuliko kijana hasiye na pesa, sasa anavyosema mzee hakuna mzee mwenye pesa akawa hana mke wala watoto

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Kipindi unawaza hivyo, ukiacha papuchi, ni value gani unaenda kuadd kwenye hiyo ndoa/mahusiano?
Na papuchi yenyewe unaweza kuta ni marapurapu kama utumbo wa mafungu pale vingunguti
 
Subiri wanaume maskini waje wakupopoe ukome.

Pesa sio kila kitu ila muhakikishe zipo za hapa na pale.
Na zikizidi pia mtashindwa jicontrol .

Pesa ya mboga, usafiri na mavazi isiwapige chenga. Mbona burudani tu.
Mtu anadate na kazee wanakutania mafichoni kwa kuogopa macho ya watu, ya nini hayo aisee.
 
Wazee wanaojua kutunza na hawana papara. Tatizo ni kwamba wewe msichana kama ulishazoea vijana ni lazima utakuwa na kijana wa pembeni ili akufikishe unapotaka.
 
FB_IMG_16652657087554332.jpg

Watu wanatoka mbali Nyie mnowaza life zuri kishamba shamba. Achume uje ule kizembe. Mwisho wa siku kila my atabaki peke yake.
 
Mwanamke mwenye mawazo kama huyu hata kama ukiwa na mali ukaoa atakufilisi na kukuacha, usioe tu kwa sababu mwanamke mzuri angalia anayepambana siku ukiyumba akupambanie
 
Maisha yetu ni mafupi sana hapa duniani, hivyo tunapaswa kufurahia maisha muda wote. Hii habari ya kuoana na mtu eti mchume wote baadaye mtafurahia maisha haikubaliki. Maana hakuna aliye na mkataba na Mungu, unaweza ukafa the next morning.

Na kwa taarifa yako furaha na umaskini havikai pamoja, ni kama maji na moto. Ukiolewa na maskini maana yake ni kwamba umeipiga teke furaha ktk maisha yako. Asikwambie mtu, pesa ndiyo sabuni ya roho.

Kama huna hela utalala sehemu yenye uvundo kama banda la beberu la mbuzi. Huyo mume wako maskini anakuwa amelala huku akikoroma maana amechoka utadhani yuko ICU (ndiyo maana ya mlalahoi). Mate
yanamtoka na kulowesha godoro unaweza kudhani kakojolea.

Utajikuta tu unaamka na kuanza kulia kwa uchungu huku ukimuuliza Mungu; why me? Maisha haya mpk lini?

Na kuna ndharia mpya kuwa maskini hatauona ufalme wa Mungu. Kwasabb kila siku anatenda dhambi ya manung'uniko. Maskini hana shukurani kwa Mungu wake. Kila siku akijisogeza mbele za mola wake anaorodhesha maombi zaidi ya mahitaji yake kwa Mungu. Lkn tajiri kila siku anamtukuza na kumshukuru kwa hatua aliyopiga. Ndiyo maana hisikii tajiri akiangushwa na pepo wachafu.

Umaskini ni ugonjwa. Kwann ? Umaskini husababisha magonjwa ya kizembe na kupelekea mtu kufa kizembe.

Usikubali kuolewa na maskini.
Na sisi hatukubali kuoa wanawake masikini dadangu!!!!Wala hakuna shida
 
Back
Top Bottom