Bora kuufuta kwanza mkataba wote wa bandari na DP World kuliko kujaribu kurekebisha chochote ili ufae

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
11,550
Reaction score
40,697
Tanzania tupo kwenye mjadala mzito unaohusu bandari na waarabu wa Dubai (DP world), na kiini cha mjadala wote ni kuhusu dosari za kimsingi zinazounguka mkataba wenye.

Jambo moja la wazi linalokubalika na pande zote katika mjadala huu ni kuwa, sote (serikali na wakosoaji) tunakubali kuwa mkataba una dosari za msingi zenye kuhitaji marekebisho kabla ya kwenda hatua yoyote nyingine mbele.

Nikiwa kama mtanzania, mwenye kuipenda nchi yangu na kuwapenda watanzania wenzangu wote, ninatoa pendekezo hili.

Serikali itangaze mara moja kusitisha mkataba wote(makubaliano yote) ili kuanza upya mchakato mzima utaoweza kuzingatia ushauri, maoni na mapendekezo kutoka kwa wadau mbalimbali.

Tuwe wakweli, mjadala kuhusu huu mkataba umetugawa vibaya watanzania, una hatarisha amani yetu, unamchafua rais wetu mpendwa wa Tanzania mama Samia Suluhu, unatupotezea muda sana, unatumia pesa nyingi kujaribu kuutetea au kuukosoa na hautoi taswira njema huko tuendako.

Mkataa pema pabaya panamwita...
Mficha maradhi mauti yatamuumbua....
Heri nusu shari kuliko shari kamili...
Dalili ya mvua ni mawingu...
Samaki mkunje angali mbichi...
 
Ule mkataba haufai, na bahati mbaya hata kama wakitaka kuuvunja mwarabu hawezi kukubali tena, zile terms za kinyonyaji zinazomfaidisha vile hawezi kuziachia kirahisi.

Mimi nasema potelea mbali, kama kukosea wameshakosea, afadhali kuwa tayari kulipa fidia ili kulinda heshima yetu, na uhuru wa mipaka yetu, kuliko kuiogopa fidia huku tukuendelea kuwa watumwa ndani ya nchi yetu.
 
Kwani unamakosa ganiiii. Ebu zungumzaaa acha unoko weka uzalendooo
 
Ule mkataba haufai, na bahati mbaya hata kama wakitaka kuuvunja mwarabu hawezi kukubali tena, zile terms za kinyonyaji zinazomfaidisha vile hawezi kuziachia kirahisi.

Mimi nasema potelea, kama kukosea wameshakosea, afadhali kuwa tayari kulipa fidia ili kulinda heshima yetu, na uhuru wa mipaka yetu, kuliko kuiogopa fidia huku tukuendelea kuwa watumwa ndani ya nchi yetu.
Mkuu ila wabunge wa ccm wana roho ngumu sana!
 
Tanzania tupo kwenye mjadala mzito unaohusu bandari na waarabu wa Dubai (DP world), na kiini cha mjadala wote ni kuhusu dosari za kimsingi zinazounguka mkataba wenye.

Jambo moja la wazi linalokubalika na pande zote katika mjadala huu ni kuwa, sote (serikali na wakosoaji) tunakubali kuwa mkataba una dosari za msingi zenye kuhitaji marekebisho kabla ya kwenda hatua yoyote nyingine mbele.

Nikiwa kama mtanzania, mwenye kuipenda nchi yangu na kuwapenda watanzania wenzangu wote, ninatoa pendekezo hili.

Serikali itangaze mara moja kusitisha mkataba wote(makubaliano yote) ili kuanza upya mchakato mzima utaoweza kuzingatia ushauri, maoni na mapendekezo kutoka kwa wadau mbalimbali.

Tuwe wakweli, mjadala kuhusu huu mkataba umetugawa vibaya watanzania, una hatarisha amani yetu, unamchafua rais wetu mpendwa wa Tanzania mama Samia Suluhu, unatupotezea muda sana, unatumia pesa nyingi kujaribu kuutetea au kuukosoa na hautoi taswira njema huko tuendako.

Mkataa pema pabaya panamwita...
Mficha maradhi mauti yatamuumbua....
Heri nusu shari kuliko shari kamili...
Dalili ya mvua ni mawingu...
Samaki mkunje angali mbichi...
Una nia mbaya na taifa hili weye.
 
Mkataba upi sasa ?
 
Nakumbuka mitihani ya kidato cha nne /sita >> paper 1 / paper 2
Kulikuwa kunaandaliwa nakala kadhaa, hili likivuja unaleta nyingine nk
huenda kuna siku mkataba halisi utatolewa hadharani
 
Ule mkataba haufai, na bahati mbaya hata kama wakitaka kuuvunja mwarabu hawezi kukubali tena, zile terms za kinyonyaji zinazomfaidisha vile hawezi kuziachia kirahisi.

Mimi nasema potelea, kama kukosea wameshakosea, afadhali kuwa tayari kulipa fidia ili kulinda heshima yetu, na uhuru wa mipaka yetu, kuliko kuiogopa fidia huku tukuendelea kuwa watumwa ndani ya nchi yetu.
Tuilipe hiyo fidai, lakini wote waliohusika wawajibishwe. Na pia iundwe kamati ndogo ya kuwachunguzwa waliopokea rushwa toka DP. Maana fidia tutakayolipa inahusisha pia pesa ambazo DP ilitumia kuwahonga watanzania wenzetu. Waliopokea hongo wafilisiwe, ili wapunguze mzigo wa fidia tutakayolipa DP.
 
Tanzania tupo kwenye mjadala mzito unaohusu bandari na waarabu wa Dubai (DP world), na kiini cha mjadala wote ni kuhusu dosari za kimsingi zinazounguka mkataba wenye.

Jambo moja la wazi linalokubalika na pande zote katika mjadala huu ni kuwa, sote (serikali na wakosoaji) tunakubali kuwa mkataba una dosari za msingi zenye kuhitaji marekebisho kabla ya kwenda hatua yoyote nyingine mbele.

Nikiwa kama mtanzania, mwenye kuipenda nchi yangu na kuwapenda watanzania wenzangu wote, ninatoa pendekezo hili.

Serikali itangaze mara moja kusitisha mkataba wote(makubaliano yote) ili kuanza upya mchakato mzima utaoweza kuzingatia ushauri, maoni na mapendekezo kutoka kwa wadau mbalimbali.

Tuwe wakweli, mjadala kuhusu huu mkataba umetugawa vibaya watanzania, una hatarisha amani yetu, unamchafua rais wetu mpendwa wa Tanzania mama Samia Suluhu, unatupotezea muda sana, unatumia pesa nyingi kujaribu kuutetea au kuukosoa na hautoi taswira njema huko tuendako.

Mkataa pema pabaya panamwita...
Mficha maradhi mauti yatamuumbua....
Heri nusu shari kuliko shari kamili...
Dalili ya mvua ni mawingu...
Samaki mkunje angali mbichi...
Hureeh👏👏
...umetoa ushauri mzuri sana. Kuna mtu alisema mfalme wa dubai eti ni mtu muungwana sana. Basi tukubaliane mkataba umekufa na wasije kutushitaki uingereza kwa kuvunja mkataba.
Saa hizi sahihi zote zimewekwa na wabunge kwa ujinga wao wamepitisha bomu kwa kufikiri wao hawatalipuka kwa kua washakula chao toka dubai.
Mungu tunusuru na hawa wahuni.
 
Tanzania tupo kwenye mjadala mzito unaohusu bandari na waarabu wa Dubai (DP world), na kiini cha mjadala wote ni kuhusu dosari za kimsingi zinazounguka mkataba wenye.

Jambo moja la wazi linalokubalika na pande zote katika mjadala huu ni kuwa, sote (serikali na wakosoaji) tunakubali kuwa mkataba una dosari za msingi zenye kuhitaji marekebisho kabla ya kwenda hatua yoyote nyingine mbele.

Nikiwa kama mtanzania, mwenye kuipenda nchi yangu na kuwapenda watanzania wenzangu wote, ninatoa pendekezo hili.

Serikali itangaze mara moja kusitisha mkataba wote(makubaliano yote) ili kuanza upya mchakato mzima utaoweza kuzingatia ushauri, maoni na mapendekezo kutoka kwa wadau mbalimbali.

Tuwe wakweli, mjadala kuhusu huu mkataba umetugawa vibaya watanzania, una hatarisha amani yetu, unamchafua rais wetu mpendwa wa Tanzania mama Samia Suluhu, unatupotezea muda sana, unatumia pesa nyingi kujaribu kuutetea au kuukosoa na hautoi taswira njema huko tuendako.

Mkataa pema pabaya panamwita...
Mficha maradhi mauti yatamuumbua....
Heri nusu shari kuliko shari kamili...
Dalili ya mvua ni mawingu...
Samaki mkunje angali mbichi...
Ni wewe kweli umetoa huu ushauri??!?!!
 
Kwa maoni yangu nafikiri ingekuwa vyema mikataba yooote kwa sasa iende TLS kwa mapitio badala ya Bungeni kwani imani na hawa 'watu' wa ccm imetutoka kabisa
Uko sahihi kwani maccm yanaweka uchama mbele ili waendelee kutawala badala ya kutanguliza Utaifa kwanza. Bunge hili linakiuka ibara ya 63 (2) ya Katiba ya JMT inayosema :'Sehemu ya pili ya Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka,kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii.'

Katika sakata hili tunaona wazi kuwa serikali ndiyo inaliagiza bunge nini cha kufanya. Wabunge wamepelekwa Dubai ili kuandaliwa kuja kupitisha mkataba(wenyewe wanaita makubaliano) wa kimangungo ambao serikali ilishaingia na DP World kitambo sana,kifupi Bunge limetumika kama muhuri tu wa serikali hii. Huu ni uvunjajaji mkubwa wa Katiba yetu hivyo hakuna sababu tena ya kuwaamini watu wanaovunja Katiba ya nchi ili kukidhi njaa ya matumbo yao na matamanio yao ya kuona chama chao kinabaki madarakani milele. Tumeona hata jinsi Spika alivyoendesha kikao kile kishabiki kabisa kama mshabiki oya oya wa Simba au Yanga ambaye yuko tayari kujivua utu wake ili tu kushangilia timu yake hata kama inaboronga.
 
Ule mkataba haufai, na bahati mbaya hata kama wakitaka kuuvunja mwarabu hawezi kukubali tena, zile terms za kinyonyaji zinazomfaidisha vile hawezi kuziachia kirahisi.

Mimi nasema potelea mbali, kama kukosea wameshakosea, afadhali kuwa tayari kulipa fidia ili kulinda heshima yetu, na uhuru wa mipaka yetu, kuliko kuiogopa fidia huku tukuendelea kuwa watumwa ndani ya nchi yetu.
Nani alipe?

Tukiweka pembeni uchawa na maslah binafsi, mkataba una njia nyingi kuuvunja.

Njia mojawapo ni kumkamata musu kumama na kumshitaki na kumfunga Kwa kupokea RUSHWA, unavunjika.

Pili ni njia ya KATIBA yetu, Katiba imetaja, mkataba au makubaliano yoyote yaliyo juu ya KATIBA ni BATILI. Hivyo mkataba unavunjika.

Tatu ni CCCCCM kuondolewa madarakani, wanaingia Serikali ingine, vinawekwa vichwa Hasa vifukue madudu yote, unavunjika.

Nne, KATIBA mpya, KATIBA mpya, unavunjika.

NB: THERE IS NO EVIL PLAN WITHOUT A MISTAKE.

Mungu ibariki TANZANIA.

Amen
 
Kufuta tu haitoshi, hatua kali za kisheria zichukuliwe kwa wahusika. This was a deliberate attack on our sovereignty.

Wote walipokea fedha za mwarabu wachukuliwe hatua kali, AG, Spika, Waziri wa miundombinu, Johari na wengine waachie nafasi zao.
 
DP WORLD wanatumika tu kama cover. Ila kuna Watanzania wenzetu ndio wanaotaka kutupiga, na huo mkataba wameutengeneza wao
 
Mkataba wa DPW unaipeleka nchi katika utumwa kwa taarifa yako! Ebu nikupe dondoo za mkataba wenyewe kama ulikuwa ufahamu: unahusisha bandari zoote za bahari, maziwa na mito; unahusisha na ardhi zilipo hizo bandari; unahusisha njia za usafirishaji wa mizigo kutoka na kuingia bandari hizo ikiwa na maana SGR, barabara, Meli, na viwanja vya ndege (all transit corridors); inaitaka serikali ihakikishe usalama wa DPW katika nyanja zoote kisiasa, kiulinzi, na kiuchumi bila kumuingilia. Serikali haitakiwi kuhoji uendeshwaji na mapato ya DPW bila ridhaa ya DPW, nk,nk.

Kwa hali hii kama serikali bado haijaufuta na kuuondoa huo mkataba, baasi! Tanganyika ni koloni la DPW! Cha kushangaza DPW sio nchi! Yaani, DPW ni kifupi cha Dubai Port World! Chakushangaza, serikali (Rais, mkuu wa nchi) anaingia Mikataba ya kuuza nchi kwa taasisi (DPW) ambaye mkuu wake sio Rais! Ndo maana tunapigwa na butwaa inakuwaje Rais wa nchi kubwa yenye wasomi na wanasheria wanaenda kuingia mkataba wa kuuza nchi kwa taasisi (sijui kampuni)???
 
I see! Next time nafasi ya umakamu wa Rais kiwe ni kigezo cha kumdisqualify mgombea wa kiti cha Urais! Tulikuwa tunachukulia poa eti umakamu rais anaweza kukaa mtu yeyote! Ona sasa!
 
Back
Top Bottom