Mkataba wa DPW unaipeleka nchi katika utumwa kwa taarifa yako! Ebu nikupe dondoo za mkataba wenyewe kama ulikuwa ufahamu: unahusisha bandari zoote za bahari, maziwa na mito; unahusisha na ardhi zilipo hizo bandari; unahusisha njia za usafirishaji wa mizigo kutoka na kuingia bandari hizo ikiwa na maana SGR, barabara, Meli, na viwanja vya ndege (all transit corridors); inaitaka serikali ihakikishe usalama wa DPW katika nyanja zoote kisiasa, kiulinzi, na kiuchumi bila kumuingilia. Serikali haitakiwi kuhoji uendeshwaji na mapato ya DPW bila ridhaa ya DPW, nk,nk.
Kwa hali hii kama serikali bado haijaufuta na kuuondoa huo mkataba, baasi! Tanganyika ni koloni la DPW! Cha kushangaza DPW sio nchi! Yaani, DPW ni kifupi cha Dubai Port World! Chakushangaza, serikali (Rais, mkuu wa nchi) anaingia Mikataba ya kuuza nchi kwa taasisi (DPW) ambaye mkuu wake sio Rais! Ndo maana tunapigwa na butwaa inakuwaje Rais wa nchi kubwa yenye wasomi na wanasheria wanaenda kuingia mkataba wa kuuza nchi kwa taasisi (sijui kampuni)???