Bora kuufuta kwanza mkataba wote wa bandari na DP World kuliko kujaribu kurekebisha chochote ili ufae

Kwa kifupi maneno ya ndungai yametimia.
 
Kwani aliyetoa saini hakusoma mkataba????
 
Ufutwe tu
 
Hakuna fidia yoyote, mkataba uliosainiwa ulikuwa kati ya nchi na nchi wala sio DPW mikataba ya dpw ndio hiyo wanaita HGA, hizo HGA bado kusainiwa labda tu kama wanatuzuga tu kumbe walishamaliza kila kitu, kwahiyo tukijichomoa sasaivi hakuna wakushitaki mwenzio.
 
Mkuu usitegemee jambo la maana kwa serikali hii.

Tuhesabu maumivu tu.
 
Hivi Rais akivunja katiba, huwajibishwaje?

Na vyombo vingine kwa mfano Mkuu wa majeshi (Cdf) na Mwanasheria mkuu wa Serikali, pamoja na genge lote linalokula viapo vya kuilinda Katiba wateuliwapo nyadhifa zao kwa viapo vyao vya: ..."Nitailinda, kuihifadhi na kuitumikia katiba ya JMT"... humaanisha kuilinda kwa namna gani, na wakiona imevunjwa ama mtu yeyote anaivunja, hutakiwa kufanyaje ili kuonekana wametekeleza viapo vyao?

Na je wakikaa kimya kumezea uvunjwaji huo, na baadaye kuja kubainika kisheria kuwa Katiba ilivunjwa wakati wao wakiwa kwenye mamlaka, ni hatua gani madhubuti wanazostahili kuchukuliwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…