BoT yakataza rasmi kampuni za mikopo mitandaoni kuchukua mawasiliano ya wateja ili kuwadhalilisha. Yatoa mwongozo mpya!

BoT yakataza rasmi kampuni za mikopo mitandaoni kuchukua mawasiliano ya wateja ili kuwadhalilisha. Yatoa mwongozo mpya!

Screenshot_20241021-110957_1.jpg

Hawa wanaitwa Bahari pesa
 
Mimi niliwatukana matusi makubwa makubwa sijapata kuona hadi wakaniblock. Baadaye akanipigia mtu aliyejitambulisha kuwa ni mhasibu wao ndio tukaongea lugha inayoeleweka tukamalizana.
 
Hebu cheki wanavyochafua watu. Na saizi hawaandiki jina la kampuni makusudi ili wasishtakiwe. Hawa wafungiwe tu
IMG-20241021-WA0031 (1).jpg
IMG-20241021-WA0031 (1).jpg
 
Kwanini ukakope vikampuni uchwara?

Una shida Ela ya chap, kakope kwenye mabenki na taasisi zinazoeleweka

Juzi kati nmevuta laki 5 na 55 benki ya nmb, riba elfu 68 Kwa siku 14

Deadline Yao tar 5 mwezi huu na sijapigiwa simu au sms yoyote ya vitisho.
Sasa ungekua umekopa kwenye online apps hiyo laki 5 ungelipa laki 8 tena kwa wiki moja, na ungekula matusi na vitisho juu
 
Hebu cheki wanavyochafua watu. Na saizi hawaandiki jina la kampuni makusudi ili wasishtakiwe. Hawa wafungiwe tu
View attachment 3131608View attachment 3131608
Wanaposema katumia taarifa za watu binafs, wanamanisha nini kama huyu ni mkopaji?

Makampuni ya mikopo ndio yanayotumia taarifa binafs kudhalilisha watu. Sass huyu yeye katumiaje hizo taarifa kudhalilisha watu?

Kama wanandai, basi watakuwa wameamua tu kumchafua baada ya kushindwa kulipa deni lao ndio wameamua kusambaza picha yake.

Au alkkopa kwa kutumia majina na taarifa za watu wengine?
 
Wanaposema katumia taarifa za watu binafs, wanamanisha nini kama huyu ni mkopaji?

Makampuni ya mikopo ndio yanayotumia taarifa binafs kudhalilisha watu. Sass huyu yeye katumiaje hizo taarifa kudhalilisha watu?

Kama wanandai, basi watakuwa wameamua tu kumchafua baada ya kushindwa kulipa deni lao ndio wameamua kusambaza picha yake.

Au alkkopa kwa kutumia majina na taarifa za watu wengine?
Kiufupi hawa ni matapeli na wanafanya kublack mail watu. Kuna kesi nyingi tu za watu ambao ukimaliza kulipa wanaendelea kukuzingua wanasingizia malipo hayakuingia uwatumie wao pesa kisha wao walipe. Na unakuta mtu alishalipa
 
Wakuu,

Kwa muda mrefu sasa, wakopaji wengi wa mitandaoni wamekuwa wakilalamika kuhusu kitendo cha baadhi ya apps za mikopo ku-access list ya mawasiliano ya wateja na kisha kuwatumia message baadhi ya contacts iwapo mteja ameshindwa kulipa.

Soma pia: Serikali ipitie upya Sheria ya 'Mikopo ya Mtandaoni (Online)'

Tabia hiyo ilifika hatua mbaya zaidi kiasi cha baadhi ya kampuni kuanzisha magroup ya Whatsap na kuadd baadhi ya contacts unaowaheshimu na kuweka picha za wadeni wao ili kuwapa presha za kulipa madeni wanayodaiwa.



Siku ya jana BOT walitoa muongozo rasmi kujibu vilio vya wananchi ambapo katika muongozo huo, BOT umeweka miongozo ifuatayo (Nime-summarize)
  • Hairuhusiwi kwa kampuni moja kumiliki apps mbili au zaidi za mikopo
  • Kampuni za mikopo haziruhusiwi kushare taarifa za mteja kwa watu au makampuni za nje ya nchi
  • Hairuhusiwi kwa kampuni za mikopo mitandaoni kukusanya namba za simu, meseji, picha, email au taarifa nyingine zozote kwenye simu yako
  • Mdhamini wa mteja ni lazima afahamishwe kuwa amechaguliwa kuwa mdhamini na akubali
  • Watu wa huduma kwa wateja hawaruhusiwi kutumia lugha chafu na kejeli kwa wateja
  • Ni marufuku kuchapisha taarifa za mteja mtandaoni iwapo atafeli kulipa deni
  • Ni marufuku kwa kampuni kumtaka mteja kulipa riba au pesa yote anayodaiwa kabla ya tarehe ya makubaliano
  • Ni marufuku kutuma meseji kwa contacts za mteja ili kumuonesha kuwa anadaiwa
Hayo ni machache tu wakuu.

Ningependa kuwapongeza BOT kwa kusikiliza kilio cha watanzania wengi.

Unaweza kupata taarifa zaidi kupitia website ya BOT

Nawasilisha
Hakuna lolote hapa. Hizi ni sinema
 
Mimi natafuta mwanasheria ambaye yuko tayari tufungue kesi kuhusu hawa jamaa kutumia taarifa zangu kunidhalilisha.
 
ebana leo ndo nimejua serikali kweli inaafanya kazi nilishaanza kusumbuliwa leo na pdf ndo linatoka.
Serikali ilitakiwa iyajue yote haya na kuweka masharti yote kwenye leseni zao wanapotoa
Ila sisi tunasubiri janga litokee ndio tuweke sheria.
Hizi sheria zingetumika zamani kwenye mikataba na wataalamu lazima walijue hili
 
Siku ya kulipa ni kesho tarehe ishirini lakini wao wanani lazimisha kulipa leo japo nimewataarifu kuhusu tarehe sahihi ya malipo lakini wameanza kuwapigia na kuwatumia watu kwenye contact zangu kama wananidai na huondo uthibitisho hivi vilio tuvipeleke wapi ili sheria itufute haya machozi ya kudhalilishwa
Screenshot_20241119-202028.png
 
Back
Top Bottom