BoT yatahadharisha wananchi kuhusu utapeli wa fedha mitandaoni

BoT yatahadharisha wananchi kuhusu utapeli wa fedha mitandaoni

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imewataka Watanzania kuwa makini na utapeli mpya unaofanyika kwa njia ya barua pepe unaoelekeza kulipa kiasi fulani cha fedha kuwezesha kupata fedha nyingi.

BOT katika taarifa yake imebaini kuongezeka kwa udanganyifu wa fedha nchini unaohusisha mwananchi kupokea taarifa (hati au barua pepe) inayodai kuwa ni uthibitisho wa malipo kupitia SWIFT na/au mifumo mingine ya uhamishaji fedha.

“Mpokeaji anafahamishwa kuwa fedha zimeingizwa kwenye benki au akaunti katika taasisi ya fedha nchini Tanzania; wakati mwingine, mpokeaji fedha anaelekezwa kulipa kiasi fulani cha fedha kuwezesha kupata fedha hizo nyingi,” imeeleza taarifa ya BoT.

Matukio mengi ya taarifa hizo yanahusisha kiasi kikubwa cha pesa kinachodaiwa kuletwa kwa ajili ya ufadhili wa mradi au matumizi binafsi.

Benki Kuu imesema taarifa hizo ni za kughushi na za kubuni na kusema “wananchi mnashauriwa kuwa waangalifu na kuacha kujihusisha na miamala hiyo ambayo kwa kawaida inalenga kuwatapeli fedha.”
FlyeIGKXgAAylc0
 
Hakuna hela ya bure. Hakuna hela rahisi. Toa thamani, dai malipo. Ukizingatia hili hutapigwa, ila ukipenda slope....
 
Hizo kampuni zimepitaje kwenye idara za serikali kama tatu mzuka mfano
 
Huo utapeli utakuwa unawahusu watu wachache sana wenye tamaa. Sisi wengine tunadunda tu.
 
Waangalia pia namna ya kushugulika nalo maana licha ya taarifa bado watu watapigwa sana tu
 
Back
Top Bottom