Boti la uokoaji limefika Morogoro, Dereva aelezea changamoto anazokumbana nazo barabarani

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Dereva wa gari linalosafirisha boti maalumu ya uokoaji katika Ziwa Victoria (Ambulance Mwanza), Hamidu Mshamu ameeleza changamoto anazokumbana nazo akiwa katika safari ya siku 14 kutoka Mtwara hadi Mwanza.

Akizungumza akiwa mkoani Morogoro leo Alhamisi Juni 19, 2025, Mshamu amesema tayari ametembea zaidi ya kilomita 1,100 tangu kuanza safari hiyo na kwa siku huweza kusafiri kati ya kilomita 100 hadi 110 kutokana na hali ya miundombinu na mazingira ya barabara. “Maeneo mengine tunalazimika kusimama kukata miti ili isiathiri mzigo wetu mkubwa,” amesema.

Boti hiyo baada ya kuwasili eneo la Msamvu, Morogoro, imepokewa na mamia ya wananchi.

Ofisa Mahusiano wa Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (Tasac), Mariamu Mwayera amesema boti hiyo imenunuliwa kupitia mradi wa kikanda wa usafirishaji na mawasiliano Ziwa Victoria.

​
Chanzo: Mwananchi_official
 
Bado sijaelewa kwanini hili suala linamake headlines na purukushani za bodaboda na wananchi.

Hiyo ni transportation ya kawaida sana tena kwangu bado ni wrong movie.
Njia sahihi ni Mombasa - Kisumu( barabara)- Mwanza (via ziwa Victoria)
Huu mlolongo wote usingekuwepo.
 
Hivi hilo boti limeshushwa mtwara
Au limetengenezwa mtwara!
Ndiyo safari ikaanzia huko

Ova
 
Bado sijaelewa kwanini hili suala linamake headlines na purukushani za bodaboda na wananchi.

Hiyo ni transportation ya kawaida sana tena kwangu bado ni wrong movie.
Njia sahihi ni Mombasa - Kisumu( barabara)- Mwanza (via ziwa Victoria)
Huu mlolongo wote usingekuwepo.
Kwani we kuna usumbufu umeupata? Kafanye mambo yako.
 
Bado sijaelewa kwanini hili suala linamake headlines na purukushani za bodaboda na wananchi.

Hiyo ni transportation ya kawaida sana tena kwangu bado ni wrong movie.
Njia sahihi ni Mombasa - Kisumu( barabara)- Mwanza (via ziwa Victoria)
Huu mlolongo wote usingekuwepo.
Unajua kwanini ina picha ya mama,ukijua hili hupati taabu
 
Bado sijaelewa kwanini hili suala linamake headlines na purukushani za bodaboda na wananchi.

Hiyo ni transportation ya kawaida sana tena kwangu bado ni wrong movie.
Njia sahihi ni Mombasa - Kisumu( barabara)- Mwanza (via ziwa Victoria)
Huu mlolongo wote usingekuwepo.

Boti ya mama
 
Msimu wa uchaguzi
 
Hiyo ni sehemu ya kampeni inabidi wananchi waione
 
Bado sijaelewa kwanini hili suala linamake headlines na purukushani za bodaboda na wananchi.

Hiyo ni transportation ya kawaida sana tena kwangu bado ni wrong movie.
Njia sahihi ni Mombasa - Kisumu( barabara)- Mwanza (via ziwa Victoria)
Huu mlolongo wote usingekuwepo.
CCM utawaweza?
utakuta kampeni zinapigiwa humo humo!!😂
 
Dereva wa gari linalosafirisha boti maalumu ya uokoaji katika Ziwa Victoria (Ambulance Mwanza), Hamidu Mshamu ameeleza changamoto anazokumbana nazo akiwa katika safari ya siku 14 kutoka Mtwara hadi Mwanza.

Akizungumza akiwa mkoani Morogoro leo Alhamisi Juni 19, 2025, Mshamu amesema tayari ametembea zaidi ya kilomita 1,100 tangu kuanza safari hiyo na kwa siku huweza kusafiri kati ya kilomita 100 hadi 110 kutokana na hali ya miundombinu na mazingira ya barabara. “Maeneo mengine tunalazimika kusimama kukata miti ili isiathiri mzigo wetu mkubwa,” amesema.

Boti hiyo baada ya kuwasili eneo la Msamvu, Morogoro, imepokewa na mamia ya wananchi.

Ofisa Mahusiano wa Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (Tasac), Mariamu Mwayera amesema boti hiyo imenunuliwa kupitia mradi wa kikanda wa usafirishaji na mawasiliano Ziwa Victoria.

Chanzo: Mwananchi_official
Hivi sisi Watanzania ni jamii ya kijinga au? Tunapenda sana kushangaa vitu, sasa hapa kuna nini cha kushangaa kama si ujinga tu?
 
Back
Top Bottom