Boti la uokoaji limefika Morogoro, Dereva aelezea changamoto anazokumbana nazo barabarani

Boti la uokoaji limefika Morogoro, Dereva aelezea changamoto anazokumbana nazo barabarani

Sasa mzee nimeamka asubuhi, nimeenda shamba, nikapalilia nyanya/vitunguu/viazi nk hadi saa nane mchana, nikaenda kijiweni kupumzika.
Boti likapita, nisishangaee??

Mimi ni bodaboda, nipo kijiweni sina abiria, boti linapita na sijawahi kuliona nisishangae??

Mimi ni mwalimu boti linapita, na ni kipindi cha likizo hiki, nisilishangae na sijawahi kuliona??

Mimi ni mwanafunzi wa kidato cha 1,2,3,4,5,6 au yata mwanachuo, nimesoma maeneo ambayo hayana bahari wala ziwa zaidi ya mito midogo, boti linapita karibu yangu na nisishangaeee??

Mimi ni mfanyabiashara ambae niko hapahapa miaka nenda rudi, sijawahi kuona boti zaidi ya kwenye picha tu , leo linapita karibu kabisa nisiende kulishangaa kweeeliii??

Mzee sio jambo baya kuangalia kitu kipya maishani mwako na ni kitu kizuri mnoo maana unaongeza maarifa.

Leo wewe ukienda kwa wahdazbe utawashangaa, ila kwao hawaoni ajabu maisha wanayoishi.
Umetisha sana.

Lakini kuna vitu vinaudhi sana nchi hii, kama hayo mabango yaliyowekwa kwa hiyo boti.
 
Back
Top Bottom