Boti la uokoaji limefika Morogoro, Dereva aelezea changamoto anazokumbana nazo barabarani

Boti la uokoaji limefika Morogoro, Dereva aelezea changamoto anazokumbana nazo barabarani

Bado sijaelewa kwanini hili suala linamake headlines na purukushani za bodaboda na wananchi.

Hiyo ni transportation ya kawaida sana tena kwangu bado ni wrong movie.
Njia sahihi ni Mombasa - Kisumu( barabara)- Mwanza (via ziwa Victoria)
Huu mlolongo wote usingekuwepo.
They want to make attention
 
Sasa mkuu kushangaa na kazi ya kufanya vinahusiana vipi??

Kwahiyo akisafiri toka Moro kuja dar kuona boti ndio anakua kapata kazi ya kufanya??
Binafsi sioni tatizo juu ya hili na ukizingatia hilo boti linapita kwa siku moja au masaa kadhaa tu.
Unaandika as if hao watu ni mwaka mzima kazi yao ni kushangaa boti.

Watu wenye mawazo kama yako huwa tunawaita LIMBUKENI..
Haya mawazo uliyoandika wewe ndio yanathibitisha ulimbukeni wako.

Ukiwa sio limbukeni huwezi kuja na hoja nyepesi kama hii, eti wanashangaa siku/ saa moja?

Kwa sababu hauna ratiba wala mipango yoyote ndio maana unaona kawaida.

Watanzania tuna kazi kubwa sana ya kuitoa Tanzania gizani, kama akili zetu ndio kama hizi zako.
 
We akili yako unafikiri ualimu ni tusi? Pamoja na kwamba mm si mwl. Ningefurahi sn kuwa mwl. Maana ni fungu jema. Ualimu ni kutekeleza takwa la mwenyenzi Mungu kuwapatia binadamu elimu. Nikiona watoto wadogo wa shule ya msingi asubuhi natamani ningekuwa nawafundisha. Kwako ww ni fimbo ya kuwatukania wenzio? We umepotoka
Sasa ndio nakutukana, wewe ni hamnazo.
Yaani mimi kukuita mwalimu ni kukutukana!!!???
"mm" na "ww" ni lugha ya wapi!!??
Ukilaza ni janga kubwa sana nchini.
 
Ingekuwa awamu ya JPM akiwa hai hii kelele zingekua nyingi sana
 
Bado sijaelewa kwanini hili suala linamake headlines na purukushani za bodaboda na wananchi.

Hiyo ni transportation ya kawaida sana tena kwangu bado ni wrong movie.
Njia sahihi ni Mombasa - Kisumu( barabara)- Mwanza (via ziwa Victoria)
Huu mlolongo wote usingekuwepo.
Angalia pembeni Ina bango la picha ya nani
 
Dereva wa gari linalosafirisha boti maalumu ya uokoaji katika Ziwa Victoria (Ambulance Mwanza), Hamidu Mshamu ameeleza changamoto anazokumbana nazo akiwa katika safari ya siku 14 kutoka Mtwara hadi Mwanza.

Akizungumza akiwa mkoani Morogoro leo Alhamisi Juni 19, 2025, Mshamu amesema tayari ametembea zaidi ya kilomita 1,100 tangu kuanza safari hiyo na kwa siku huweza kusafiri kati ya kilomita 100 hadi 110 kutokana na hali ya miundombinu na mazingira ya barabara. “Maeneo mengine tunalazimika kusimama kukata miti ili isiathiri mzigo wetu mkubwa,” amesema.

Boti hiyo baada ya kuwasili eneo la Msamvu, Morogoro, imepokewa na mamia ya wananchi.

Ofisa Mahusiano wa Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (Tasac), Mariamu Mwayera amesema boti hiyo imenunuliwa kupitia mradi wa kikanda wa usafirishaji na mawasiliano Ziwa Victoria.



Chanzo: Mwananchi_official
Kwani wametokea wapi?
 
Kuna fly over ambayo ule mzigo haupiti..? Pale njia ya chini magufuli mzigo ule haupiti?? Unaijua dar kweli..

Kuna fly over ambayo ule mzigo haupiti..? Pale njia ya chini magufuli mzigo ule haupiti?? Unaijua dar kweli..?
Duuuh
1.kivuko cha treni pale mtongani
2.Daraja la watembea kwa miguu vingunguti kama akisema apite Tazara flyover
3.Vile vivuko ukipita Magufuli Terminal...nahisi pale ni kibamba kuna U-turn ya kivuko cha juu
 
Mkuu inaonekana ww kidogo una chuki na Uislamu kwa mujibu wa sentence yakoyamwisho.
Halafu inaonekana huna uelewa wowote na masuala ya ships construction.
Meli au boat kukatwa vipande na ku-assemble upya haimaanishi kuwa itakatwa yote kama vile inapokatwa kwa ajili ya scraper.
Tena kwa boat ndogo kama hiyo isiyozidi urefu wa mita 50(LengthOverall) kazi inakuwa nyepesi zaidi.
Meli au boat ndogo kama hiyo itakatwa eneo la 'forecastle,freeboard na aft mooring station'.
Eneo la 'superstructure'ambalo ndani yake kuna wheelhouse,crew's accommodation na hiyo ICU haliwezi kukatwa na linaweza kusafirishwa kwenye lorry bila shida yoyote.
Labda kama materials yaliyotumika kutengeneza ni fiberglass ndiyo itakuwa ngumu kidogo ku-assemble,lakini kama ni aluminum hiyo ni kazi nyepesi sana.
Kuhusu wataalamu mbona hata Bongo wapo wengi tu wala haihitaji wazungu kutoka Ulaya waje ku-assemble .
End of Thinking Capacity?

Ndugu Kafiri/Kobazi
1. Hiyo lowbed iliyobeba Boat ina mgawanyo wa gurudumu nyingi sana so uzito wa boat hauwezi kuleta madhara makubwa kwenye barabara
2. Hiyo Boat kwenda ku-assemble mwanza ni gharama kubwa zaidi kwani unahitaji kusafirisha team ya waliotengeneza Boat kutoka ulaya na pia ungehitaji gari zaidi ya 5 kusafirisha hivo vipande na ukizingatia hiyo boat ni ambulance ina mpaka ICU room so ku-assemble sio suala dogo
3. Route ya mtwara-songea ndiyo njia Sahihi kwani hakuna flyover wala vivuko vya treni wala madaraja dhaifu

Mimi yangu ni hayo tu ndugu kobazi/Kafiri
 
Haya mawazo uliyoandika wewe ndio yanathibitisha ulimbukeni wako.

Ukiwa sio limbukeni huwezi kuja na hoja nyepesi kama hii, eti wanashangaa siku/ saa moja?

Kwa sababu hauna ratiba wala mipango yoyote ndio maana unaona kawaida.

Watanzania tuna kazi kubwa sana ya kuitoa Tanzania gizani, kama akili zetu ndio kama hizi zako.
Sasa mzee nimeamka asubuhi, nimeenda shamba, nikapalilia nyanya/vitunguu/viazi nk hadi saa nane mchana, nikaenda kijiweni kupumzika.
Boti likapita, nisishangaee??

Mimi ni bodaboda, nipo kijiweni sina abiria, boti linapita na sijawahi kuliona nisishangae??

Mimi ni mwalimu boti linapita, na ni kipindi cha likizo hiki, nisilishangae na sijawahi kuliona??

Mimi ni mwanafunzi wa kidato cha 1,2,3,4,5,6 au yata mwanachuo, nimesoma maeneo ambayo hayana bahari wala ziwa zaidi ya mito midogo, boti linapita karibu yangu na nisishangaeee??

Mimi ni mfanyabiashara ambae niko hapahapa miaka nenda rudi, sijawahi kuona boti zaidi ya kwenye picha tu , leo linapita karibu kabisa nisiende kulishangaa kweeeliii??

Mzee sio jambo baya kuangalia kitu kipya maishani mwako na ni kitu kizuri mnoo maana unaongeza maarifa.

Leo wewe ukienda kwa wahdazbe utawashangaa, ila kwao hawaoni ajabu maisha wanayoishi.
 
Mbwembwe nyingi alafu uokozi sifuri
 
Back
Top Bottom