Boti la uokoaji limefika Morogoro, Dereva aelezea changamoto anazokumbana nazo barabarani

Boti la uokoaji limefika Morogoro, Dereva aelezea changamoto anazokumbana nazo barabarani

Bado sijaelewa kwanini hili suala linamake headlines na purukushani za bodaboda na wananchi.

Hiyo ni transportation ya kawaida sana tena kwangu bado ni wrong movie.
Njia sahihi ni Mombasa - Kisumu( barabara)- Mwanza (via ziwa Victoria)
Huu mlolongo wote usingekuwepo.
Kuna bango la mama lazima lipate airtime
 
Kwenye Kila tatizo hapakosi fursa wenye makampuni wana feli wapi? angetokea mmoja akabandika tangazo lake hapo kwenye hilo boti Kwa udhamini Wa pesa ndogo sana ila lingesomwa na watu wengi zaidi kama ndo hivi boti lenyewe linasubiriwa kama mwenge Wa uhuru
 
Dereva wa gari linalosafirisha boti maalumu ya uokoaji katika Ziwa Victoria (Ambulance Mwanza), Hamidu Mshamu ameeleza changamoto anazokumbana nazo akiwa katika safari ya siku 14 kutoka Mtwara hadi Mwanza.

Akizungumza akiwa mkoani Morogoro leo Alhamisi Juni 19, 2025, Mshamu amesema tayari ametembea zaidi ya kilomita 1,100 tangu kuanza safari hiyo na kwa siku huweza kusafiri kati ya kilomita 100 hadi 110 kutokana na hali ya miundombinu na mazingira ya barabara. “Maeneo mengine tunalazimika kusimama kukata miti ili isiathiri mzigo wetu mkubwa,” amesema.

Boti hiyo baada ya kuwasili eneo la Msamvu, Morogoro, imepokewa na mamia ya wananchi.

Ofisa Mahusiano wa Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (Tasac), Mariamu Mwayera amesema boti hiyo imenunuliwa kupitia mradi wa kikanda wa usafirishaji na mawasiliano Ziwa Victoria.



Chanzo: Mwananchi_official
Bonge la adventure ataingia kwenye vitabu vya kumbukumbu.. Wachukue na video za matukio yote wake kutengeneza documentary
 
Hivi sisi Watanzania ni jamii ya kijinga au? Tunapenda sana kushangaa vitu, sasa hapa kuna nini cha kushangaa kama si ujinga tu?
Hakuna jamii ya watu duniani ambayo haipendi kushangaa vitu ambavyo hawajawahi kuviona. Hata wewe ukiwaona wamasai unaona kawaida ila wazungu wakija huku wanawashangaa utafikiri wameona nini sijui
Hilo sio kosa la Watanzania ni nature ya binadamu. Sio kila muda uwe unajiona smart na kutukana Watanzania, mmeshawatukana sana Watz wenzenu inatosha sasa. Kila kitu Watanzania this Watanzania that. So pathetic!
 
Nimetoka kutizama kipande cha serie ya POWER saa hii niko napepea pureweed yangu...nikitoka hapo am going to find my lost believable 10,000 then narudi nyumbani....ila mwaka huu ni NO REFORM NO ELECTION....Na hapo ndio watakapojua kunavijana wako timamu kiakili ila sio viherehere.
 
Hakuna jamii ya watu duniani ambayo haipendi kushangaa vitu ambavyo hawajawahi kuviona. Hata wewe ukiwaona wamasai unaona kawaida ila wazungu wakija huku wanawashangaa utafikiri wameona nini sijui
Hilo sio kosa la Watanzania ni nature ya binadamu. Sio kila muda uwe unajiona smart na kutukana Watanzania, mmeshawatukana sana Watz wenzenu inatosha sasa. Kila kitu Watanzania this Watanzania that. So pathetic!
Unalia nini? acha kutetea ujinga.

Hiyo kitu ni ushamba wa hali ya juu.
Mbona hatushangai au kujitokeza kudai na kupigania mambo ya msingi?
 
Hii boti labda ipo kimkakati ya kimaonyesho , lakini hakuna faida ya kitembeza kwa mwezi mzima kwenda Mwanza. Kwanza inaleta hasara hizi
1. Uharibifu wa barabara kwa aijli ya uzito
2. Gharama ya kuasafirisha kigezo cha muda namafuta
3. Inaleta foleni njiani kwa ajili ya eneo inalochukua na spidi inayotembea
Hii boti ilitakiwa iwe itenganishwe vipande na kwenda kuungwa Mwanza, aliyeamua hivi kuna wasiwasi wake kitaakuma
 
Watu hawajawahi kuiona boti, acha waishangae, kuna makosa gani mtu kushangaa??
Sio kushangaa, sema Watanzania hatuna kazi za msingi za kufanya.

Tungekuwa na maisha mazuri au tunajitambua, ni suala la kwenda boti zilipo kama kusafiri kutoka huko vijijini mlipo muende Dar, Mtwara, Mwanza na sehemu zingine ikiwezekana nje ya nchi.
 
Bado sijaelewa kwanini hili suala linamake headlines na purukushani za bodaboda na wananchi.

Hiyo ni transportation ya kawaida sana tena kwangu bado ni wrong movie.
Njia sahihi ni Mombasa - Kisumu( barabara)- Mwanza (via ziwa Victoria)
Huu mlolongo wote usingekuwepo.
We bado haujaelewa michezo kumbe,hao bodaboda wenyewe uikifuatilia utakuta wamekula posho kila mmoja
 
Bado sijaelewa kwanini hili suala linamake headlines na purukushani za bodaboda na wananchi.

Hiyo ni transportation ya kawaida sana tena kwangu bado ni wrong movie.
Njia sahihi ni Mombasa - Kisumu( barabara)- Mwanza (via ziwa Victoria)
Huu mlolongo wote usingekuwepo.
Limeletwa kimkakati mkuu. Nchi inaenda kwa trending na kiki hii.
NO REFORMS NO ELECTION
 
Ina maana likitoka morogoro linaelekea dodoma, singida, shinyanga na kufika mwanza?
Nimejiuliza na mm hivi hivi why Iringa wasingepitia ile njia ya kuingia dodoma then waendelee na safari yao unawaza kuta watalipeleka Dar Tanga Kilimanajaro Arusha
 
Back
Top Bottom