Daktari W Sindabhalla
JF-Expert Member
- Jan 29, 2017
- 600
- 580
Habari wana JF.
Ninaomba ufahamu ili niiokoe ndoa ya watu.
Wiki iliyopita nilimtembelea dada yangu anayeishi Dodoma mjini - Chang'ombe Extension.
Yeye na MR. wake na watoto 2 wana chumba na sebule.
Kwakuwa nilikuwa na majukumu binafsi mbali na kuitembelea familia hii na kutokana na ufinyu wa nyumba yao, ilinilazimu kuchukua room guest.
Siku ya tatu, dada na shemeji yangu wakanitaarifu kuwa kuna chumba kimoja pale kwao ambacho bado hakina mpangaji hivyo nikilipie 20,000/= kwa wiki 2 za kuishi kwangu Dom.
Chumba kilikuwa na changamoto 1 tu, juu palikuwa wazi kabisa.
Tatizo lilitokea siku mbili kabla ya mimi kuondoka Dom. wakati wa usiku wa saa mbili, nimetoka kuoga bafu la nje, wamama wa pembeni mwa chumba changu walikuwa wakiendelea na mapishi jirani na milango yao.
Walizoea kuniita Uncle kwasababu ya vile watoto wa sister wanavyoniita
Nikiwa chumbani nikung'uta bukta niliyotokanayo bafuni, ghafla ile bukta ikagusa kamba ya net na kuniponyoka mkononi na kuangukia chumba cha pili.
Muda si mrefu jamaa wa chumba hicho akawa anaingia ndani kwake na moja kwa moja akaelekea kuwasha TV.
Hapo ndipo alipoikuta bukta yangu nyuma ya TV penye switch ya ukutani. Bukta ya mtu mzima tena bado inamajimaji,,,,,,,,,,,Duh!
Alimuita mkewe aliyekuwa anapika, na hapo ndipo malumbano ya kuwa mwanamke huwa anaingiza wanaume ndani yakakolea.
Kichapo kikatembea,,,,,,hakika moyo uliniuma ila nilikaa kimya.
Kesho yake niliwaeleza wenyeji wangu, ila walinionya nisiingilie wala nisiseme uhalisia. wakiamini kuwa yataisha tu.
Wana miaka 2 ktk mahusino yao ila mdada hajawahi kushika mimba.
ukijumlisha na hili,,,, jamaa kaamua kumuacha mkewe na yuko mbioni kuoa mwingine.
Nimejulishwa kuwa mdada ameanza kwenda kwenye maombi kwaajili ya ndoa yake.
Mimi tayari nimeisha ondoka.
Ila naomba ufahamu kwenu wana JF, jinsi ninavyoweza kuwa msaada wa kurejesha ndoa ya hawa jamaa.