Boxer yangu katika chumba cha mpangaji mwenzangu

Angetoka huyo mwanaume aseme mwenye boxer yake ajitokeze.
 
Hao majirani uliowaeleza ni wachawi tu!
Hiyo ishu mbona ndogo sana, ungemwambia tu aamue alivyotaka!
Halafu huo uwazi wa chumba vipi yani, yaani kilikuwa wazi kiasi kwamba hakikuwa na paa ma vipi aiseeh…?[emoji23][emoji23]
 
Huu uzi utumike kufungia mwaka huu wa mauzauza na mwaka wa matendo makuu ya Mungu.
Hapo jiandae kumwoa huyo mwanamke
 
Habari wana JF.

Ninaomba ufahamu ili niiokoe ndoa ya watu.
Wiki iliyopita nilimtembelea dada yangu anayeishi Dodoma mjini - Chang'ombe Extension.
Yeye na MR. wake na watoto 2 wana chumba na sebule.

Kwakuwa nilikuwa na majukumu binafsi mbali na kuitembelea familia hii na kutokana na ufinyu wa nyumba yao, ilinilazimu kuchukua room guest.
Siku ya tatu, dada na shemeji yangu wakanitaarifu kuwa kuna chumba kimoja pale kwao ambacho bado hakina mpangaji hivyo nikilipie 20,000/= kwa wiki 2 za kuishi kwangu Dom.

Chumba kilikuwa na changamoto 1 tu, juu palikuwa wazi kabisa.

Tatizo lilitokea siku mbili kabla ya mimi kuondoka Dom. wakati wa usiku wa saa mbili, nimetoka kuoga bafu la nje, wamama wa pembeni mwa chumba changu walikuwa wakiendelea na mapishi jirani na milango yao.

Walizoea kuniita Uncle kwasababu ya vile watoto wa sister wanavyoniita
Nikiwa chumbani nikung'uta bukta niliyotokanayo bafuni, ghafla ile bukta ikagusa kamba ya net na kuniponyoka mkononi na kuangukia chumba cha pili.
Muda si mrefu jamaa wa chumba hicho akawa anaingia ndani kwake na moja kwa moja akaelekea kuwasha TV.

Hapo ndipo alipoikuta bukta yangu nyuma ya TV penye switch ya ukutani. Bukta ya mtu mzima tena bado inamajimaji,,,,,,,,,,,Duh!
Alimuita mkewe aliyekuwa anapika, na hapo ndipo malumbano ya kuwa mwanamke huwa anaingiza wanaume ndani yakakolea.

Kichapo kikatembea,,,,,,hakika moyo uliniuma ila nilikaa kimya.
Kesho yake niliwaeleza wenyeji wangu, ila walinionya nisiingilie wala nisiseme uhalisia. wakiamini kuwa yataisha tu.
Wana miaka 2 ktk mahusino yao ila mdada hajawahi kushika mimba.

ukijumlisha na hili,,,, jamaa kaamua kumuacha mkewe na yuko mbioni kuoa mwingine.
Nimejulishwa kuwa mdada ameanza kwenda kwenye maombi kwaajili ya ndoa yake.
Mimi tayari nimeisha ondoka.
Ila naomba ufahamu kwenu wana JF, jinsi ninavyoweza kuwa msaada wa kurejesha ndoa ya hawa jamaa.
Je ungesikia jamaa anasema siwezi mwachia Mungu bukta hii lazima ifike kwa sangoma na mara unasikia jamaa anaongea na mganga wake anamwambia ili kuondoa lawama waulize kwanza majirani wako. Ungeulizwa ungejitokeza?
 
Muda uleule mm ningetoka mbio mpaka nje ningewaambia"jamani eeh nimekungu'ta boksa yangu imegonga chandarua imeruka huko juu imedondokea huko chumbani nami nina haraka nina safar nataka nivae nimuwahi jamaa hebu nipeni nisije nikachelewa".

Lkn jamaa ulijua yatakayotokea kabla hayajatokea ndio maana ulikaa kimya.Wewe ni muharibifu hivyo pambana urudishe ndoa ya watu uliyoharibu kwa jambo lako la kijinga.
 
Habari wana JF.

Ninaomba ufahamu ili niiokoe ndoa ya watu.
Wiki iliyopita nilimtembelea dada yangu anayeishi Dodoma mjini - Chang'ombe Extension.
Yeye na MR. wake na watoto 2 wana chumba na sebule.

Kwakuwa nilikuwa na majukumu binafsi mbali na kuitembelea familia hii na kutokana na ufinyu wa nyumba yao, ilinilazimu kuchukua room guest.
Siku ya tatu, dada na shemeji yangu wakanitaarifu kuwa kuna chumba kimoja pale kwao ambacho bado hakina mpangaji hivyo nikilipie 20,000/= kwa wiki 2 za kuishi kwangu Dom.

Chumba kilikuwa na changamoto 1 tu, juu palikuwa wazi kabisa.

Tatizo lilitokea siku mbili kabla ya mimi kuondoka Dom. wakati wa usiku wa saa mbili, nimetoka kuoga bafu la nje, wamama wa pembeni mwa chumba changu walikuwa wakiendelea na mapishi jirani na milango yao.

Walizoea kuniita Uncle kwasababu ya vile watoto wa sister wanavyoniita
Nikiwa chumbani nikung'uta bukta niliyotokanayo bafuni, ghafla ile bukta ikagusa kamba ya net na kuniponyoka mkononi na kuangukia chumba cha pili.
Muda si mrefu jamaa wa chumba hicho akawa anaingia ndani kwake na moja kwa moja akaelekea kuwasha TV.

Hapo ndipo alipoikuta bukta yangu nyuma ya TV penye switch ya ukutani. Bukta ya mtu mzima tena bado inamajimaji,,,,,,,,,,,Duh!
Alimuita mkewe aliyekuwa anapika, na hapo ndipo malumbano ya kuwa mwanamke huwa anaingiza wanaume ndani yakakolea.

Kichapo kikatembea,,,,,,hakika moyo uliniuma ila nilikaa kimya.
Kesho yake niliwaeleza wenyeji wangu, ila walinionya nisiingilie wala nisiseme uhalisia. wakiamini kuwa yataisha tu.
Wana miaka 2 ktk mahusino yao ila mdada hajawahi kushika mimba.

ukijumlisha na hili,,,, jamaa kaamua kumuacha mkewe na yuko mbioni kuoa mwingine.
Nimejulishwa kuwa mdada ameanza kwenda kwenye maombi kwaajili ya ndoa yake.
Mimi tayari nimeisha ondoka.
Ila naomba ufahamu kwenu wana JF, jinsi ninavyoweza kuwa msaada wa kurejesha ndoa ya hawa jamaa.
Hapo kwenye bukta yako kurukia chumba cha jirani wakati wa kukung'uta sijaelewa vizuri,huo ukuta unaotenganisha hivyo vyumba ni mfupi kiasi gani?
 
Back
Top Bottom