Boxer yangu katika chumba cha mpangaji mwenzangu

Boxer yangu katika chumba cha mpangaji mwenzangu

Kwahiyo mkuu wewe huwa unaiachia mishuzi kwa nguvu zote?😂 haya baba
sio hivyo madam, hii nimekutaka wewe ujambe kwa nguvu.
Yaani kwa lolote unalolitoa ama chochote unachokitoa Moyoni mwako kwaajili ya jamii, hakikisha unakitoa kwa nguvu zote hadi jamii yote isikie. yamkini ikaleta matokeo fulani ktk jamii.
 
sio hivyo madam, hii nimekutaka wewe ujambe kwa nguvu.
Yaani kwa lolote unalolitoa ama chochote unachokitoa Moyoni mwako kwaajili ya jamii, hakikisha unakitoa kwa nguvu zote hadi jamii yote isikie. yamkini ikaleta matokeo fulani ktk jamii.
Vitu vya jamii ndiyo uvifananishe na vijambo vya nguvu mkuu? Aah hii ulimanisha mashuzi tu😂so wewe huwa unaijambia jamii kwa nguvu?😂
 
Habari wana JF.

Ninaomba ufahamu ili niiokoe ndoa ya watu.
Wiki iliyopita nilimtembelea dada yangu anayeishi Dodoma mjini - Chang'ombe Extension.
Yeye na MR. wake na watoto 2 wana chumba na sebule.

Kwakuwa nilikuwa na majukumu binafsi mbali na kuitembelea familia hii na kutokana na ufinyu wa nyumba yao, ilinilazimu kuchukua room guest.
Siku ya tatu, dada na shemeji yangu wakanitaarifu kuwa kuna chumba kimoja pale kwao ambacho bado hakina mpangaji hivyo nikilipie 20,000/= kwa wiki 2 za kuishi kwangu Dom.

Chumba kilikuwa na changamoto 1 tu, juu palikuwa wazi kabisa.

Tatizo lilitokea siku mbili kabla ya mimi kuondoka Dom. wakati wa usiku wa saa mbili, nimetoka kuoga bafu la nje, wamama wa pembeni mwa chumba changu walikuwa wakiendelea na mapishi jirani na milango yao.

Walizoea kuniita Uncle kwasababu ya vile watoto wa sister wanavyoniita
Nikiwa chumbani nikung'uta bukta niliyotokanayo bafuni, ghafla ile bukta ikagusa kamba ya net na kuniponyoka mkononi na kuangukia chumba cha pili.
Muda si mrefu jamaa wa chumba hicho akawa anaingia ndani kwake na moja kwa moja akaelekea kuwasha TV.

Hapo ndipo alipoikuta bukta yangu nyuma ya TV penye switch ya ukutani. Bukta ya mtu mzima tena bado inamajimaji,,,,,,,,,,,Duh!
Alimuita mkewe aliyekuwa anapika, na hapo ndipo malumbano ya kuwa mwanamke huwa anaingiza wanaume ndani yakakolea.

Kichapo kikatembea,,,,,,hakika moyo uliniuma ila nilikaa kimya.
Kesho yake niliwaeleza wenyeji wangu, ila walinionya nisiingilie wala nisiseme uhalisia. wakiamini kuwa yataisha tu.
Wana miaka 2 ktk mahusino yao ila mdada hajawahi kushika mimba.

ukijumlisha na hili,,,, jamaa kaamua kumuacha mkewe na yuko mbioni kuoa mwingine.
Nimejulishwa kuwa mdada ameanza kwenda kwenye maombi kwaajili ya ndoa yake.
Mimi tayari nimeisha ondoka.
Ila naomba ufahamu kwenu wana JF, jinsi ninavyoweza kuwa msaada wa kurejesha ndoa ya hawa jamaa.
Mkuu
Siku hizi wanaume hatuvai boxer.

Joto la Dar utaunguza watoto kwenye mifuko ya mbegu.
 
Vitu vya jamii ndiyo uvifananishe na vijambo vya nguvu mkuu? Aah hii ulimanisha mashuzi tu😂so wewe huwa unaijambia jamii kwa nguvu?😂
😅😅😅😅ahahaha!!!!! haya Financial S.
acha tusali kisha tukalale japo kwa saa kadhaa.
 
Mkuu
Siku hizi wanaume hatuvai boxer.

Joto la Dar utaunguza watoto kwenye mifuko ya mbegu.
Ok,
actually, ilikuwa ni bukta laini ama tuiite pensi nyanya.
nilikosea kutumia neno boxer.
ingawaje huwa nazitumia ila siishi Dar Mkuu.
 
nilikuwa kama nimebutwaa hivi, na ghafla nikasikia mdada akiitwa na kuulizwa " mala ngapi umekuwa ukifanya uchafu wako humu ndani ya chumba changu na kujifanya mtakatifu.......niambie haraka, hii nguo ni yanani?"
Hapo ndipo hofu iliponishika.
hakika sikuweza kufanya lolote zaidi ya kwenda kuwaebukta yenyewe ilikuwa imelowa na umetokea bafunileza wenyeji wangu ambao waliniambia nikae kimya

Kama story yako ni ya kweli; kwa maumivu anayo pitia huyo dada, Hakuna namna unaweza kuyaelezea!
Nakushauri uende tena bila kupoteza muda ukaongee na huyo Mume wake; Unaweza kwenda na kumuomba muende out kwa chakula/kinjwaji ( hii haitaji tena kuendelea kuomba ushauri)
Muelezee hilo tukio mwanzo mwisho, jinsi ulivyo andika hapo juu na kwa kuwa ilikuwa ni kweli, utakuwa umempa huyo mwanamme nafasi ya kufikiria maamuzi yake upya. Muombe msamaha kuwa ulikuwa mgeni hivyo ulipata woga kumjulisha
Tofauti na hapo, hayo machozi ya huyo mwanamke yatakufuata.....
 
Kwa maumivu anayo pitia huyo dada, Hakuna namna unaweza kuyaelezea!
Nakushauri uende tena bila kupoteza muda ukaongee na huyo Mume wake; Unaweza kwenda na kumuomba muende out kwa chakula/kinjwaji ( hii haitaji tena kuendelea kuomba ushauri)
Muelezee hilo tukio mwanzo mwisho, jinsi ulivyo andika hapo juu na kwa kuwa ilikuwa ni kweli, utakuwa umempa huyo mwanamme nafasi ya kufikiria maamuzi yake upya. Muombe msamaha kuwa ulikuwa mgeni hivyo ulipata woga kumjulisha
Tofauti na hapo, hayo machozi ya huyo mwanamke yatakufuata.....
Namshauri afuate alichoambiwa na nduguze.

Huo msala asiuingie. Seems huyo bwege anaweza hata kuua
 
Aisee hata mm nimeshtuka, ila nimeshtuka zaidi boxer yenye maji kuruka kwenye neti kisha ikadunda na kwenda chumba cha pili [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MREJESHO.
Habari wana JF.,
Siku chache nyuma niliweka andiko kuhusiana na changamoto niliyoisababisha mimi nilipokuwa Mkoani Dodoma.
Baada ya pensi yangu kuangukia chumba cha jirani yangu na kuleta mtafaruku kwa wanandoa vijana, Hatimaye, nilipata ushauri mzuri hapa JF. Na miongoni mwenu mlinihimiza kuwasiliana na wahusika haraka iwezekanavyo.

NAWASHUKURU sana kwa ushauri wenu maana kwa hakika nimeutendea kazi, na kwasehemu umeleta matokeo chanya.

Shemeji na dada yangu walinisaidia kupata namba za simu za Mchungaji ambapo yule dada alijiunga kwaajili ya maombezi.
Nilimpigia simu Pastor kumueleza kila kitu kilichotokea wakati huo, na madhara yake.
Majuzi, siku ya Ijumaa waliniita Dodoma pale kanisani kwao, wakanikutanisha na wahusika wote wawili pamoja na ndugu wa pande zote mbili, shemeji na dada yangu walikuwepo pia.
Mambo yalikuwa mengi, mzozo ulikuwa mkubwa, ila kilichowaaminisha kuwa ile nguo ilikuwa yangu ni picha ya hovyo kabisa ambayo alinipiga mtoto wangu siku moja ya mwezi wa 4 nikiwa bombani nabadilisha koki ya maji.
Siku hiyo ndiyo niliivaa hiyo pensi na nilikuwa na wife pembeni.
Nawashukuru wale viongozi wa lile kanisa kwa namna walivyomsihi kijana kupokea majibu.
Mimi nina AMANI baada ya hayo.
ila kijana aligoma kunipa pensi yangu kwa wakati ule.
Aliahidi atawapa ndugu zangu siku atakapoona ni salama moyoni mwake.
ASANTENI SANA.
 
Back
Top Bottom