Boxer yangu katika chumba cha mpangaji mwenzangu

Ni sawa ndugu. Tatizo langu lilikuwa ni hofu iliyonijaa mala baada ya vichapo kutembezwa na kutotokea mpangaji hata mmoja aliyejitokeza kuamulia.
pili, niliingiziwa hofu na wenyeji wangu.
hakika sikuwa na ujasiri wa kulivalia njuga tatizo hilo kwa wakati ule.
 
Kuna ukweli ktk usemalo.
ila sikupenda kuubeba ukweli huo ambao niliusikia ktk majibizano yao.
mimi najihisi kuwa na hatia tu.

Kama ni hivyo
Pale pale bukta ilipoanguka ilikuwa uende kuiomba na kumwambia mshkaji
Oya bukta imedondokea kwako

Ila ukauchuna na kutoa kiti nje na kufurahia movie likiendelea [emoji12]
Ila sitaki kuamini sana hii ya pili
Lakini wapo wa hivyo pia

Dunia Ina mambo hii
 
ni kweli usemalo. ila sikupata solution kwa haraka. Ni kama ganzi tu ilinishika hata nisijue chakufanya kwa haraka.
na haikuchukua hata dakika 5 jamaa akaingia ndani.
hakika nawaza hilo lingetendwa nyumbani kwangu, hata kama ni baba yangu ama kaka yangu nisingelipokea kwa wepesi.
 
Kwamba bukra ikiwa imelowana inakuwa nzito kwa kg ngap? Hadi ishindwe ruka chumba cha pili
Zipompa,,,,,,,,,,ilikuwa accidentally tu ndugu yangu.
Ni kama unakunywa maji wewe mwenyewe alafu yanakupalia.
Utafanyaje sasa?
Utamshika uchawi nani?
 
Uncle umezingua...ilitakiwa wakati uleule ilipodondoka utoke kuwaeleza wenyeji

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
hakika nimezingua. Ndio maana linanisumbua kwasasa. ningeweza ku mute, tatizo moyo unanisuta.
ni kama nimemgonga mtu kwa gari alafu nikakimbia bila kumpa msaada wowote. amani haipo kabisa.
 
Duh, nimesema kweli ila umeninyima ushirikiano.
hata hivyo nashukuru kwa kustaajabu hilo.
 
yaani kwa issue yako ilivyo kuwa sensitive hukutakiwa kuchukua muda wa kuomba ushauri...
Ungemuita yule mwanamme huku umevalia taulo yako muombe msamaha kuwa kuna ngua yako imerukia kwake kwa bahati mbaya wakati unaikunguta. Mambo mengine hayataki kuomba ushauri kwani yanataka maamuzi ya haraka; sasa hivi ni vigumu kuaminika...
 
nilikuwa kama nimebutwaa hivi, na ghafla nikasikia mdada akiitwa na kuulizwa " mala ngapi umekuwa ukifanya uchafu wako humu ndani ya chumba changu na kujifanya mtakatifu.......niambie haraka, hii nguo ni yanani?"
Hapo ndipo hofu iliponishika.
hakika sikuweza kufanya lolote zaidi ya kwenda kuwaeleza wenyeji wangu ambao waliniambia nikae kimya.
 
Iyo bukta yako mkuu nmemuona nayo jamaa kwenye basi la Saratoga sijui anaenda nayo kigoma kukufanyaje

Sent from my SM-G960U1 using JamiiForums mobile app
sijui kama watafanikiwa, maana sikushiriki uchafu wowote zaidi ya kosa hili la ghafla.
mala nyingi ubaya humpata mtu aliyetenda kosa/dhambi kwa makusudi, hasa dhambi ya zinaa huwa haimuachi mtu salama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…