Boxer yangu katika chumba cha mpangaji mwenzangu

Kwahiyo mkuu wewe huwa unaiachia mishuzi kwa nguvu zote?πŸ˜‚ haya baba
sio hivyo madam, hii nimekutaka wewe ujambe kwa nguvu.
Yaani kwa lolote unalolitoa ama chochote unachokitoa Moyoni mwako kwaajili ya jamii, hakikisha unakitoa kwa nguvu zote hadi jamii yote isikie. yamkini ikaleta matokeo fulani ktk jamii.
 
sio hivyo madam, hii nimekutaka wewe ujambe kwa nguvu.
Yaani kwa lolote unalolitoa ama chochote unachokitoa Moyoni mwako kwaajili ya jamii, hakikisha unakitoa kwa nguvu zote hadi jamii yote isikie. yamkini ikaleta matokeo fulani ktk jamii.
Vitu vya jamii ndiyo uvifananishe na vijambo vya nguvu mkuu? Aah hii ulimanisha mashuzi tuπŸ˜‚so wewe huwa unaijambia jamii kwa nguvu?πŸ˜‚
 
Mkuu
Siku hizi wanaume hatuvai boxer.

Joto la Dar utaunguza watoto kwenye mifuko ya mbegu.
 
Vitu vya jamii ndiyo uvifananishe na vijambo vya nguvu mkuu? Aah hii ulimanisha mashuzi tuπŸ˜‚so wewe huwa unaijambia jamii kwa nguvu?πŸ˜‚
πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…ahahaha!!!!! haya Financial S.
acha tusali kisha tukalale japo kwa saa kadhaa.
 
Mkuu
Siku hizi wanaume hatuvai boxer.

Joto la Dar utaunguza watoto kwenye mifuko ya mbegu.
Ok,
actually, ilikuwa ni bukta laini ama tuiite pensi nyanya.
nilikosea kutumia neno boxer.
ingawaje huwa nazitumia ila siishi Dar Mkuu.
 

Kama story yako ni ya kweli; kwa maumivu anayo pitia huyo dada, Hakuna namna unaweza kuyaelezea!
Nakushauri uende tena bila kupoteza muda ukaongee na huyo Mume wake; Unaweza kwenda na kumuomba muende out kwa chakula/kinjwaji ( hii haitaji tena kuendelea kuomba ushauri)
Muelezee hilo tukio mwanzo mwisho, jinsi ulivyo andika hapo juu na kwa kuwa ilikuwa ni kweli, utakuwa umempa huyo mwanamme nafasi ya kufikiria maamuzi yake upya. Muombe msamaha kuwa ulikuwa mgeni hivyo ulipata woga kumjulisha
Tofauti na hapo, hayo machozi ya huyo mwanamke yatakufuata.....
 
Namshauri afuate alichoambiwa na nduguze.

Huo msala asiuingie. Seems huyo bwege anaweza hata kuua
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MREJESHO.
Habari wana JF.,
Siku chache nyuma niliweka andiko kuhusiana na changamoto niliyoisababisha mimi nilipokuwa Mkoani Dodoma.
Baada ya pensi yangu kuangukia chumba cha jirani yangu na kuleta mtafaruku kwa wanandoa vijana, Hatimaye, nilipata ushauri mzuri hapa JF. Na miongoni mwenu mlinihimiza kuwasiliana na wahusika haraka iwezekanavyo.

NAWASHUKURU sana kwa ushauri wenu maana kwa hakika nimeutendea kazi, na kwasehemu umeleta matokeo chanya.

Shemeji na dada yangu walinisaidia kupata namba za simu za Mchungaji ambapo yule dada alijiunga kwaajili ya maombezi.
Nilimpigia simu Pastor kumueleza kila kitu kilichotokea wakati huo, na madhara yake.
Majuzi, siku ya Ijumaa waliniita Dodoma pale kanisani kwao, wakanikutanisha na wahusika wote wawili pamoja na ndugu wa pande zote mbili, shemeji na dada yangu walikuwepo pia.
Mambo yalikuwa mengi, mzozo ulikuwa mkubwa, ila kilichowaaminisha kuwa ile nguo ilikuwa yangu ni picha ya hovyo kabisa ambayo alinipiga mtoto wangu siku moja ya mwezi wa 4 nikiwa bombani nabadilisha koki ya maji.
Siku hiyo ndiyo niliivaa hiyo pensi na nilikuwa na wife pembeni.
Nawashukuru wale viongozi wa lile kanisa kwa namna walivyomsihi kijana kupokea majibu.
Mimi nina AMANI baada ya hayo.
ila kijana aligoma kunipa pensi yangu kwa wakati ule.
Aliahidi atawapa ndugu zangu siku atakapoona ni salama moyoni mwake.
ASANTENI SANA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…