Raymanu KE
JF-Expert Member
- Jan 20, 2022
- 8,611
- 16,118
Matango pori
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
We jamaa kila kitu unataka kuprove watu unakiweza?[emoji23][emoji23]Huyo bro wako ni zoba sipendi mwanaume mwoga ambaye changamoto kidogo anaufyata na hawa ndo wanaume wa Tanzania wanatakiwa wapiganie bandari tunasafari ndefu sana kama nchi
Kwenye maisha mtu anaweza kukuambia jambo ambalo ili akupime uwezo wako wa akili na hii inapnyesha uwezo wa kukabiliana na changamoto ni mdogo sana kwa bro wako
Jambo lolote kwenye maisha unalipigania haliji kirahis lazima tuwafundishe watoto wetu hiki kitu mwanaume jasiri huwez mkuta ana zirazira
Hata kama story yakutunga ila wewe BICHWA lako zito SANA kauze Skrepa tuMahari mmetoka kutoa last week,leo wana 2kids,,ni chizi pekee atakaeisoma hii utumbo yako,,,,chizi wa hed
Daaaah huo ndo uanaume. Binafsi nachukia sana familia inayowafanya mabinti zao kuwa kitega uchumi. Kuoana ni kitendo cha kuunganisha familia sasa unapanga mahari ili kuikomoa halafu siku mnapata shida mnakimbilia wapi?Last week bro ilikuwa anaenda kutoa mahari kwa kabila moja huko Kanda ya Kaskazinu. Ni bro wangu wa damu kabisa baada ya yeye ndo mimi. Hivyo tukachukuana kwenye usafiri hao mpaka huko. Mimi, bro, uncle, rafiki na mshenga tuliambiwa tungempata kule kule.
Tukaenda Ukweni. Siku ya kwanza ikabidi tuonane na mshenga tuyajenge kwanza na tufahamiane. Bro wangu naye ni mpole sana kama mimi. Huwa mnaweza kaa hata masaa 3 hamjaongea kitu. Hapendi kabisa kuongea ongea.
Basi kesho yake tukaenda ukweni. Tumefika harakati nyingi zinaendelea. Watu wana mishe mishe za kumwaga. Ikafika wakati wa msosi. Tukaona tu wakwe wanaitana wanaenda wanakula wakifurahia. Tukasubiri sana muda umeenda saa 10 hiyo.
Wale ndugu ukweni wamekula wameshiba ndo wanatuita nasi tukale. Bro aligoma. Akadai amefunga. Tukashangaa amefunga masaa ya mchana tu? Maana bfast tuligonga naye vizuri tu soup na chapati.
Anyway sisi wengine tukaenda kizushi tu maana chakula chenyewe walishapakua mapande makubwa ya nyama n.k wamebakiza mifupa tu. Mi nikachukua ndizi chache sana.
Tumekula sasa tumekaa. Tumalize kilichotupeleka. Na mipango ni kuwa tumalize mahari pale pale siku ile ile. Basi yakatajwa mambo kadhaa ikafika kwenye mahari. Mjomba mtu anasema mahari ni tsh mil 8. Haipungui hata sent tano. Mshenga akabembeleza sana. Wakagomea hapo. Sisi tulijipanga mahari halisi isizidi Mil 5.
Jamaa wakagoma. Bro muda wote huo yupo kimya ila mimi nlisha mwona hayupo sawa. Maana alishaanza kufinya finya macho. Namjua akianza hivyo maana yake amekasirika.
Basi akasimama ghafla na kusema haina shida. Pale center kuna ATM au Mawakala wa kutoa pesa. Wale wakwe wakajibu kwa haraka sana wapo. Kwa Assey wanatoa hadi Mil 10.
Bro akaniambia twende dogo akamwita na mshenga na mjomba. Wakaja nje akasema twendeni tukatoe pesa. Mshenga akasema wao wasubiri mle ndani. Sisi tuende. Basi tukaingia garini na kuanza kuelekea center. Nikamwona bro anakanyaga mafuta mpaka hotel tuliyofikia.
Akamtumia mshenga tsh 100, 000. Akamtuma dereva taxi mmoja aende kule ukweni akamchukue Mjomba. Akazima simu. Shughuli akaniambia ndo kamaliza.
Bro wala hakutaka kuongea. Nami namjua. So sikutaka muuliza. Huwa akiamua anakuwa ameshaamua. Kule wakachanganyikiwa. Mjomba akaja amefura hasira. Bro alimwambia tu kwa sasa hata Mil 2 ya mahari halipi ameghairi. Kesho tunarudi Dar. Akaingia room.
Mshenga alinitafuta kesho nikamwambia jamaa ameghairi. Wakwe wakaanza kumwambia mshenga amrudishe kijana wakayajenge ni mila tu. Bro akatuambia tupande garini na mizigo maana hatutarudi tena Hotelin. Tukapanda na akaanzisha safari kurudi Dar. Simu kazima.
Shem alikuja mwenyewe Dar. Bro alimwambia safari hii wakitaka mahari waifuate Dar. Akamtia mimba wanaishi wote kwa sasa na two kids. Wakwe walitumiwa tu pesa za zawadi n.k ila hawana hamu kabisa na bro.
Mkaishia vipi sasa?Ana akili kama zangu mm nishakimbia ukweni mara 3 kisa mahari zao kubwa hzo
Hamna sisi watu wapole.Kadanganya uhalisia wake,afu chini kaanza kuonyesha uhalisia wake
Pole dada. Usijali ni typing error dada. Usiwe na hasira sana.Mahari mmetoka kutoa last week,leo wana 2kids,,ni chizi pekee atakaeisoma hii utumbo yako,,,,chizi wa hed
Umemjibu vizuri. Ana maumivu makubwa namfahamu huyo binti/dogo. Typing error imemfanya apate pa kutolea makasiriko yake.Hata kama story yakutunga ila wewe BICHWA lako zito SANA kauze Skrepa tu
Hawa ndio wanaume wanaotakiwa Sasa,hao wapuuzi Wakome kama walidhani mtoto wao ni asset itawatoa ndio imeshawakata hivyo..Last three years bro alikuwa anaenda kutoa mahari kwa kabila moja huko Kanda ya Kaskazini. Ni bro wangu wa damu kabisa baada ya yeye ndo mimi. Hivyo tukachukuana kwenye usafiri hao mpaka huko. Mimi, bro, uncle, rafiki na mshenga tuliambiwa tungempata kule kule.
Tukaenda Ukweni. Siku ya kwanza ikabidi tuonane na mshenga tuyajenge kwanza na tufahamiane. Bro wangu naye ni mpole sana kama mimi. Huwa mnaweza kaa hata masaa 3 hamjaongea kitu. Hapendi kabisa kuongea ongea.
Basi kesho yake tukaenda ukweni. Tumefika harakati nyingi zinaendelea. Watu wana mishe mishe za kumwaga. Ikafika wakati wa msosi. Tukaona tu wakwe wanaitana wanaenda wanakula wakifurahia. Tukasubiri sana muda umeenda saa 10 hiyo.
Wale ndugu ukweni wamekula wameshiba ndo wanatuita nasi tukale. Bro aligoma. Akadai amefunga. Tukashangaa amefunga masaa ya mchana tu? Maana bfast tuligonga naye vizuri tu soup na chapati.
Anyway sisi wengine tukaenda kizushi tu maana chakula chenyewe walishapakua mapande makubwa ya nyama n.k wamebakiza mifupa tu. Mi nikachukua ndizi chache sana.
Tumekula sasa tumekaa. Tumalize kilichotupeleka. Na mipango ni kuwa tumalize mahari pale pale siku ile ile. Basi yakatajwa mambo kadhaa ikafika kwenye mahari. Mjomba mtu anasema mahari ni tsh mil 8. Haipungui hata sent tano. Mshenga akabembeleza sana. Wakagomea hapo. Sisi tulijipanga mahari halisi isizidi Mil 5.
Jamaa wakagoma. Bro muda wote huo yupo kimya ila mimi nlisha mwona hayupo sawa. Maana alishaanza kufinya finya macho. Namjua akianza hivyo maana yake amekasirika.
Basi akasimama ghafla na kusema haina shida. Pale center kuna ATM au Mawakala wa kutoa pesa. Wale wakwe wakajibu kwa haraka sana wapo. Kwa Assey wanatoa hadi Mil 10.
Bro akaniambia twende dogo akamwita na mshenga na mjomba. Wakaja nje akasema twendeni tukatoe pesa. Mshenga akasema wao wasubiri mle ndani. Sisi tuende. Basi tukaingia garini na kuanza kuelekea center. Nikamwona bro anakanyaga mafuta mpaka hotel tuliyofikia.
Akamtumia mshenga tsh 100, 000. Akamtuma dereva taxi mmoja aende kule ukweni akamchukue Mjomba. Akazima simu. Shughuli akaniambia ndo kamaliza.
Bro wala hakutaka kuongea. Nami namjua. So sikutaka muuliza. Huwa akiamua anakuwa ameshaamua. Kule wakachanganyikiwa. Mjomba akaja amefura hasira. Bro alimwambia tu kwa sasa hata Mil 2 ya mahari halipi ameghairi. Kesho tunarudi Dar. Akaingia room.
Mshenga alinitafuta kesho nikamwambia jamaa ameghairi. Wakwe wakaanza kumwambia mshenga amrudishe kijana wakayajenge ni mila tu. Bro akatuambia tupande garini na mizigo maana hatutarudi tena Hotelin. Tukapanda na akaanzisha safari kurudi Dar. Simu kazima.
Shem alikuja mwenyewe Dar. Bro alimwambia safari hii wakitaka mahari waifuate Dar. Akamtia mimba wanaishi wote kwa sasa na two kids. Wakwe walitumiwa tu pesa za zawadi n.k ila hawana hamu kabisa na bro.
Bro huwa namkubali sana... Mnaweza mkawa mnajadiliana kitu akawa kimya.... Wana ndugu mtajadiliana weeeeee. Akiona hamfikii hitimisho anaamka zake anaenda fanya maamuzi aliyoona yeye yanafaa.Hawa ndio wanaume wanaotakiwa Sasa,hao wapuuzi Wakome kama walidhani mtoto wao ni asset itawatoa ndio imeshawakata hivyo..
Kwanza Mimi nilishasema siwezi toa magari zaidi ya mil.2.
Kabisaanaimani kwenye safari hiyo ulienda kama wifi
Sana jamaa me nilikuwa naye nimepiga chini wa Arusha halafu mmbuluWanaushenzi sana huko kati wanadhani pesa zinachumwa hapo kwenye miti.
Hio ndio dawa yao
Kingole kwa bro wako.
Hata Mimi ninaye mmoja wa pande hizo tutaenda kwa formula hio tu
Ilikuaje?Sana jamaa me nilikuwa naye nimepiga chini wa Arusha halafu mmbulu
Huenda walioana sogea tukae so hapo walienda wakiwa wameshaoana kienyejiStori nzuri.... Ila last week mlienda kutoa mahari na sasa hivi bro wako ana 2 kids, serious[emoji23][emoji23][emoji23]
Yeaaah... Na wewe ndo kaka amekuzalisha watoto wawili. Habari za siku wifi yangu mpendwa?naimani kwenye safari hiyo ulienda kama wifi