TANZIA Brother Peter Lyimo, aliyekuwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Majengo-Moshi amefariki Dunia

TANZIA Brother Peter Lyimo, aliyekuwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Majengo-Moshi amefariki Dunia

Nakumbuka nilienda ofisini kwake mimi mwenyewe kumuomba nafasi ya kujiunga na kidato cha pili, alinipokea kama wageni wengine bila kujali umri wangu. Aliniuliza maswali kadhaa kwa upole na mwisho akanipa kibali cha kujiunga na shule.

R.I.P BROTHER.View attachment 1643918
Aisee you are a wonderful archiver. Such a clean kept note🤣🤣😂😂😀😃😃😃. Happy that your former Headmaster was such a kind man. May his soul Rest In Eternal Peace. Amen
 
Inasikitisha na kuhuzunisha sana kwa kifo chake. Ametutoka mapema leo 07/12/2020. Taarifa zaidi kuhusu chanzo cha kifo chake zitakujia hivi karibuni.

Nafahamu kuna wana MJSS wengi sana hapa Jukwaani walio ndani na nje ya nchi. Karibuni tumuenzi mkuu wetu mpendwa kwa maneno ya faraja.

MAY HIS SOUL REST IN ETERNAL LIFE.
Pole sana ndugu yangu
 
Kabisa mkuu. Watu wengi sana wamepitia mikononi mwake wengi saaana Ikiwemo Jamal Sambeke rubani TPDF
IMG00253-20110114-1431_400x400.jpg

Yule kijana wa Peter Malya?
 
Dah unanikumbusha mbali sana Majengo secondary. Maeneo hayo ndio homu.

R. I. P
 
Majengo ilikua bora zaidi kwa ajili yake, imebaki kuwa miongoni mwa sehemu bora sana zilizowahi kutokea katika maisha yangu..
Mungu anajua zaidi mioyo yetu kuliko tunavofahamiana, lakini katika akili zangu za kibinadam Mungu amevuna kilicho bora, hakika Brother Peter Lymo alikua ni Mzazi, mwalim na mlezi wangu katika miaka yangu pale majengo, Mungu amrehem na ampe pumziko la amani...
 
Dah soo sad...alikuwa anapenda wanafunzi sana,
Alikuwa ni mtu wa watu.
nakumbuka alikuwa hapendi mwanafunzi kuwa Na ndefu...A K.A mzuzu...RIP legend....
 
Majengo secondary School taasisi ambayo watumishi wake hawakuwahi kuwa na wazo la kuacha kazi wala kutafuta kazi sehemu nyingine.
Management iliyowajali sana watumishi na watumishi wakawajali sana wateja wao wanafunzi

Mungu awapumzishe kwa amani, Tutawakumbuka daima🙏
Brother Peter Lyimo RIP
Brother Pius Kihuru RIP
Mr Mgimwa RIP
Mr Nyindo RIP
Mr Sendoro RIP
Mr Almas RIP
Mr Mkumbwa RIP
Chef mkuu Mr James RIP
 
Back
Top Bottom