TANZIA Brother Peter Lyimo, aliyekuwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Majengo-Moshi amefariki Dunia

TANZIA Brother Peter Lyimo, aliyekuwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Majengo-Moshi amefariki Dunia

Majengo secondary School taasisi ambayo watumishi wake hawakuwahi kuwa na wazo la kuacha kazi wala kutafuta kazi sehemu nyingine.
Management iliyowajali sana watumishi na watumishi wakawajali sana wateja wao wanafunzi

Mungu awapumzishe kwa amani, Tutawakumbuka daima🙏
Brother Peter Lyimo RIP
Brother Pius Kihuru RIP
Mr Mgimwa RIP
Mr Nyindo RIP
Mr Sendoro RIP
Mr Almas RIP
Mr Mkumbwa RIP
Chef mkuu Mr James RIP
Mkumbwa mzee wa kemia nae alishatutangulia kumbe?
 
Woooi kumbe hivyo tuu😂😂 Haya pole kwa kubeba hilo zigo chuki kwenye moyo wako, utakua unachoka sana. Mimi Mmwenzio hata sikuwahi kukujua ndio leo naona hii ID
Lay down woman ohoooo!
 
Da aisee huyu mwalimu ndo alinifanya leo kuwa baba mzuri wa familia pia na huu mkate ninao upata kwa sasa ni matunda ya usimamizi wake mzri. Mwl mwingine ni MKUMBWA KICHAWELE', SENDORO,SAFARI Kuna mmoja anaitwa TERITERI. RIP brother
Wazazi wako walikushindwa?
 
Aisee you are a wonderful archiver. Such a clean kept note[emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23][emoji3][emoji2][emoji2][emoji2]. Happy that your former Headmaster was such a kind man. May his soul Rest In Eternal Peace. Amen
Aamen.

Kuanzia nimeanza shule nimetunza documents zangu zote hadi leo tena kwa hali ya usafi.

Check receipt niliyofanyia malipo term moja baada ya kupewa kibali na Brother PL.
IMG_20201207_154546_062~2_1.jpg
 
Majengo ilikua bora zaidi kwa ajili yake, imebaki kuwa miongoni mwa sehemu bora sana zilizowahi kutokea katika maisha yangu..
Mungu anajua zaidi mioyo yetu kuliko tunavofahamiana, lakini katika akili zangu za kibinadam Mungu amevuna kilicho bora, hakika Brother Peter Lymo alikua ni Mzazi, mwalim na mlezi wangu katika miaka yangu pale majengo, Mungu amrehem na ampe pumziko la amani...
Aaamen.
 
Dah soo sad...alikuwa anapenda wanafunzi sana,
Alikuwa ni mtu wa watu.
nakumbuka alikuwa hapendi mwanafunzi kuwa Na ndefu...A K.A mzuzu...RIP legend....
Alivyohamishwa kuna siku akatembelea MJ niliona video wanafunzi wakiandamana kumtaka asiondoke & arudi kuwa mkuu wao, Ilibidi Polisi waje kumsaidia aondoke maana wanafunzi walizingira gari lake pande zote.

Hakika amepokelewa mbinguni na baba muumba.
 
RIP Brother Peter Lyimo,nakumbuka ukiapisha viongozi waliochaguliwa na wanafunzi ulikua unasema "Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu"
 
Back
Top Bottom