TANZIA Brother Peter Lyimo, aliyekuwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Majengo-Moshi amefariki Dunia

TANZIA Brother Peter Lyimo, aliyekuwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Majengo-Moshi amefariki Dunia

Mwl Mkubwa alinifanya kujua Physics na Kemia Olevel maana nilikuwa natia timu MJSS at any time napita kwa mzee Ally baba yake na mshkaji wangu wa kipindi kile Miraji napiga pindi la hatari then narudi zangu Boarding yule moja ya kitata ila ilikuwa mjini
 
Alivyohamishwa kuna siku akatembelea MJ niliona video wanafunzi wakiandamana kumtaka asiondoke & arudi kuwa mkuu wao, Ilibidi Polisi waje kumsaidia aondoke maana wanafunzi walizingira gari lake pande zote.

Hakika amepokelewa mbinguni na baba muumba.
Ulisoma wapi mtu akifa anaenda mbinguni

Poleni kwa msiba
 
Da aisee huyu mwalimu ndo alinifanya leo kuwa baba mzuri wa familia pia na huu mkate ninao upata kwa sasa ni matunda ya usimamizi wake mzri. Mwl mwingine ni MKUMBWA KICHAWELE', SENDORO,SAFARI Kuna mmoja anaitwa TERITERI. RIP brother
RIP brother mkumbwa naye alishafariki hata mwaka haujapita
 
Nilikua Sisomi mjss ila sifa zake niliziskia plus alikua anakaa mabrother mtaani kwangu pale soweto na brothers wengine....enzi ya kina kisa kisa...na dagi pwaaa
 
New form 2 Student as per joining instructions 🙏🏽
Nakumbuka nilienda ofisini kwake mimi mwenyewe kumuomba nafasi ya kujiunga na kidato cha pili, alinipokea kama wageni wengine bila kujali umri wangu. Aliniuliza maswali kadhaa kwa upole na mwisho akanipa kibali cha kujiunga na shule.

R.I.P BROTHER.View attachment 1643918
 
Mbele yake nyuma yetu R.I.P bro Peter Lymo hyu jamaa alikua n mtu poa sana niseme tu ukweli ndgu zangu walishasamehewa ada kutokana na hali ya kifamilia kuyumba Bro.Peter Lymo aliagiza madeni yao kufutwa na wakapewa na vyeti vyao [emoji25][emoji24][emoji24][emoji24]apumzike kwa Aman
 
Apumzile kwa amani. Majengo ni kati ya shule zilozokua na wanafunzi wengi sana Moshi na bado ufaulu wake ukawa uko vizuri.
Kwenye ufaulu kaa kimya. Zero 100 ni ufaulu mzuri????
 
Majengo sec kulikuwa na mwalimu 1 anamiliki pikiliki aina ya Honda 110 aliitwa Mwl Miraba hivi bado yupo pale?
 
Moyo wangu umehuzunika sana kwa kifo cha Mwlm wangu mpendwa Bro. Peter Lyimo, pumzika kwa amani mwalimu. Ntabaki nakumbuka usemi wako mkubwa wa "Punctuality in the morning" nawaza pia kama mzee Rama naye (mlinzi wa getini) angekuwa hai vile ambavyo angelia kwa uchungu kwa jinsi ulivyokuwa kipenzi chake
 
Moyo wangu umehuzunika sana kwa kifo cha Mwlm wangu mpendwa Bro. Peter Lyimo, pumzika kwa amani mwalimu. Ntabaki nakumbuka usemi wako mkubwa wa "Punctuality in the morning" nawaza pia kama mzee Rama naye (mlinzi wa getini) angekuwa hai vile ambavyo angelia kwa uchungu kwa jinsi ulivyokuwa kipenzi chake
Duuuh Kwan na Mzee Rama Alifariki ?
 
Back
Top Bottom