TANZIA Brother Peter Lyimo, aliyekuwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Majengo-Moshi amefariki Dunia

TANZIA Brother Peter Lyimo, aliyekuwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Majengo-Moshi amefariki Dunia

Dah! Mola ampumzishe kwa amani. Alifanya kazi kubwa sana kuibadilisha Majengo - shule iliyokuwa na kila aina ya wanafunzi unaoweza kuwadhania hapa dunia. Nilipojiunga na Majengo, yeye na Mr Minja ndio waalimu walionielewa toka awali. Nitaendelea kumshukuru na kumuombea pumziko la amani.
 
Da aisee huyu mwalimu ndo alinifanya leo kuwa baba mzuri wa familia pia na huu mkate ninao upata kwa sasa ni matunda ya usimamizi wake mzri. Mwl mwingine ni MKUMBWA KICHAWELE', SENDORO,SAFARI Kuna mmoja anaitwa TERITERI. RIP brother
Dah,umenikumbusha mbali sana. Kuna Mr James wa English alikuwa na mikwara yake...Kichawele na usemi wake wa "jampu kifrogi frogi"...Teriteri alivyokuwa hapendi wanafunzi wa kike...Mkumbwa na tukio la trench town..! Kweli Majengo kulikuwa hakuboi, ni tukio baada ya tukio😅
 
Aamen.

Kuanzia nimeanza shule nimetunza documents zangu zote hadi leo tena kwa hali ya usafi.

Check receipt niliyofanyia malipo term moja baada ya kupewa kibali na Brother PL.View attachment 1643975

Hongera sana mkuu. Wengine sisi hata documents za jana tu hatujui tumetupa wapi. Naona umeficha mwaka nilitamani nijue walau umezitunza kwa makadirio ya miaka mingapi.
 
Moyo wangu umehuzunika sana kwa kifo cha Mwlm wangu mpendwa Bro. Peter Lyimo, pumzika kwa amani mwalimu. Ntabaki nakumbuka usemi wako mkubwa wa "Punctuality in the morning" nawaza pia kama mzee Rama naye (mlinzi wa getini) angekuwa hai vile ambavyo angelia kwa uchungu kwa jinsi ulivyokuwa kipenzi chake
Rama yupo,mzee Ali ndo alifariki
 
Nimesikitika zaidi kujua pia Mr Almas na Mkumbwa hatupo nao tena, Mr Almas mbobezi ya Somo LA Biolojia, Mkumbwa mbobezi wa Kemia, wote nimepita mikononi mwao. Wapumzike kwa amani
Mr Almas alikua akitibiwa muhimbili hadi alipofarika. Alikua mpole sana yule baba. Mkubwa mwenye chemistry yake🙏
 
Brother Lyimo alikua akitukuta tunajisomea madarasani weekend anampigia sim brother anayehusika na maakuli kule brothers centre tunaletewa vyuku.
Alale salama kazi aliyotumwa aliifanya sawasawa
Kuku moshi ni kile cha arusha,maana watoto wengi wa majengo walikua wanakitumia
 
Comment zote za kistaarabu.
Kweli teaching is a noble profession. Ingekua polisi au yule asiyependwa na wengi ingekua sio msiba bali kibali cha beer, kitimoto yaani Xmas ingeshaanza.
Tujifunze kutenda mema. Haina maana kuwaumiza watu kisa tu una madaraka. Dunia yenyewe tunapita tu.
Ukweli Mtupu
 
Wanakuja wajuvi
Tayari walishajibu hapa kwenye post #94

 
Majengo secondary School taasisi ambayo watumishi wake hawakuwahi kuwa na wazo la kuacha kazi wala kutafuta kazi sehemu nyingine.
Management iliyowajali sana watumishi na watumishi wakawajali sana wateja wao wanafunzi

Mungu awapumzishe kwa amani, Tutawakumbuka daima[emoji120]
Brother Peter Lyimo RIP
Brother Pius Kihuru RIP
Mr Mgimwa RIP
Mr Nyindo RIP
Mr Sendoro RIP
Mr Almas RIP
Mr Mkumbwa RIP
Chef mkuu Mr James RIP
Duuh!!!!mkubwa alifarik lin tena??
 
Back
Top Bottom