BRUSSELS, UBELGIJI: Rais Samia akutana na Tundu Lissu na kufanya mazungumzo mafupi

BRUSSELS, UBELGIJI: Rais Samia akutana na Tundu Lissu na kufanya mazungumzo mafupi

Na wengi ambao hawajafurahishwa na kutaniko hili la Rais Samia na gwiji la siasa ambaye pia ni makamu mwenyekiti Chadema mhe. Lissu ni wahafidhina wa CCM.

Kwa nini hawataki siasa za maridhiano nchini? Hilo ni swali la kujiuliza kwa nguvu zote.

Ona hata wakati vyombo vya habari hilo ni jambo kubwa kwenye front page zao lakini magazeti yanayomilikiwa na ccm na wahafidhina wao wamepotezea habari kubwa kwao kama hiyo jambo ambalo sio la kawaida. Nikama wamemchukia mama kwa alichofanya.


View attachment 2122574

View attachment 2122573
Halafu si unajua hili gazeti na chief sio kivile?
 
Elewa jambo, Lissu kaomba kuonana na Samia akakubaliwa, Chadema Tz licha ya kumuandikia barua Samia ya kuonana nae walijibiwa watapangiwa siku lakini hiyo siku haikuwahi kufika, usikurupuke tafakari kwanza ndio uandike.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia, amekutana na kufanya Mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Tundu Lissu.

Ni baada ya Lissu kuomba kuonana naye.

Walizungumzia mambo mbalimbali kuhusu ustawi wa Tanzania.

Pia, soma

1). Makamu wa Rais, Samia Suluhu amtembelea Tundu Lissu hospitalini Nairobi

2). Tundu Lissu afutiwa kesi zote za uchochezi

3). Summary ya Maongezi ya Rais Samia na Tundu Lissu

View attachment 2121534
View attachment 2121277
View attachment 2121284View attachment 2121285
View attachment 2121326
Picha: Rais Samia alipokutana na Tundu Lissu nchini Ubelgiji


UPDATES: LISSU AELEZA MAMBO SABA (7) ALIYOZUNGUMZA NA RAIS SAMIA
1. Ajenda ilikuwa "hali ya siasa ya nchi yetu." mazungumzo yamechukua takribasi saa moja, na mojawapo ya mambo niliyozungumza nae ni juu ya mwenendo wa kesi ya Mbowe

2. Ajenda ya pili ni suala na la vyama vya upinzani kufanya shughuli za kisiasa kwa mujibu wa sheria.

3. Jambo la tatu ni suala la Katiba Mpya na nimemwambia Mh. Rais ana nafasi ya kuhakikisha tunapata Katiba Mpya na anatengeneza mfumo wa kidemokrasia.

4. Ajenda ya nne, ni inayonihusi mimi na wenzangu tuliolazimika kuikimbia nchi yetu sababu ya vitisho. Nimemwambia Rais kwa mamlaka yake, nina haki ya kupatiwa matibabu kwa mujibu wa sheria, na mazingira yanayohusu kuondolewa kwangu Tundu A. Lissu bungeni na kutokulipwa mafao yangu.

5. Nimemwambia Mh. Rais kuwa mimi Tundu A. Lissu ninahitaji kurudi nyumbani na ninahitaji atoe kauli ya kunikaribisha nyumbani na nitakuwa salama, nimehakikishiwa nitapata hati ya kusafiria, kwa kuwa yangu iliibiwa Ujerumi. Nimewaongelea pia wenzangu Wenje Ezekiah na Godbless Lema

6. Nimemweleza mh. Rais sisi Chadema hatuna wabunge Bungeni kwa kuwa wale wabunge tumewafukuza uanachama. Nimemwomba Mh. Alishughulikie hilo.

7. Ajenda ya mwisho nimemwomba Mh. Rais atuongoze katika kuliponya Taifa kutokana na majeraha tuliyonayo, kwa kutekeleza ahadi yake ya kukutana na viongozi wa vyama vya upinzani.

Pia soma: Summary ya Maongezi ya Rais Samia na Tundu Lissu yaliyofanyika Ubelgiji
Good,

Yule shetani alikuwa na roho mbaya Sana, picha yake ya mwisho karibia na siku chache au mwezi mmoja kabla ya kifo chake Mungu alimbadilisha Hadi sura lake likawa Kama iblis,

Hile picha alipiga akiwa somewhere kwenye uzinduzi wa kituo Cha usafiri sijui wanini
 
Good,

Yule shetani alikuwa na roho mbaya Sana, picha yake ya mwisho karibia na siku chache au mwezi mmoja kabla ya kifo chake Mungu alimbadilisha Hadi sura lake likawa Kama iblis,

Hile picha alipiga akiwa somewhere kwenye uzinduzi wa kituo Cha usafiri sijui wanini
Sukumagangs na Mataga ni wanafiki sana. Hivi walishindwa kabisa kumwambia kuwa zile picha zake hasa za kampeni hazikufaa kuwa public!
 
Back
Top Bottom