Buguruni kunalemaza sana wakuu, hebu angalia nguvu ya 500!

Karibu mjini mkuu..hizo ni nyama za ng'ombe waliokufa,ukanda huo wa buguruni mpaka gongo la mboto ndio biashara yao kubwa..
Mnadanganya sana, ukitaka kuelewa zunguka kwenye mabucha bei za nyama hazifanani unajuwa kwa nini?

Nyama zina grade, grade one kwa Dar buchani kilo moja bei haiwezi kupunguwa shilling 10,000/=

Grade ya kawaida unaweza kuuziwa kilo kwa shilling 7000/= sasa imagine mtu anayekwenda machinjioni atapata kwa shilling ngapi?

Halafu isitoshe wauza supu za bei kitonga wengi wanauza bandama, mapupu na makolomelo, hivyo vitu machinjioni havina bei.

Binafsi naelewa vizuri bei za machinjioni unakuta tumbo lote la mbuzi umeshasafishwa kila kitu unauziwa kwa shilling 15,000/= tu, halafu ukienda bar eti unauziwa supu ya utumbo kwa shilling 2000 ni wizi mtupu.
 
Nakupa chimbo sasa ndani ya City center, mtaa wa Samora pale jengo la daily news nyuma kuna mama anaitwa mama Zai, hapo ni mapishi ya nazi, bei ya juu haizidi shilling 3000/=

Maboss wanaojiona status zao ni shida kwenda pale wanafanyiwa delivery maofisini, ukienda saa 8 mchana hupati chakula kimeisha.

Kipindi cha nyuma holiday inn ya kuelekea occean road kuna mama yupo jirani alisababisha mpaka wazungu wanalala hotelini wanakwenda kula pale mpaka holiday wakafanya fitina yule mama akafukuzwa pale.

Watu hawana taarifa tu.
 
Duh hiyo mia tatu (300) mwaka gani mkuu? Kikombe cha chai? Holiday inn napapata sana, tumepiga sana misosi. Ila hawa akina mama zai wanapepo yao kwenye chakula 😂.
 
Huu ni zaidi ya uongo!
yaani 300 upate sahani ya Chakula? mtakuwa mnalishwa mashudu nyinyi
 
Duh hiyo mia tatu (300) mwaka gani mkuu? Kikombe cha chai? Holiday inn napapata sana, tumepiga sana misosi. Ila hawa akina mama zai wanapepo yao kwenye chakula 😂.
Ni shilling 3000/= nilikosea dígit, nimeshaedit.

Wao na holiday inn, sisi chimbo letu tukaliita holiday out, wamefanya fitina na kuhonga pesa Jiji mpaka yule mama akafukuzwa pale.
 
cha muhimu kujua ni supu hiyo ni ya nini, na ni supu kweli au kitu kingine. nyama hiyo imetoka bushani au ndio yale mavibudu yanakufa peke yake wakaona wasiyatupe, au ni yale mabaki ya nyama kule machinjioni, au ni.........
 
cha muhimu kujua ni supu hiyo ni ya nini, na ni supu kweli au kitu kingine. nyama hiyo imetoka bushani au ndio yale mavibudu yanakufa peke yake wakaona wasiyatupe, au ni yale mabaki ya nyama kule machinjioni, au ni.........
Hakuna mama muuza supu mtaani anayenunuwa buchani, bucha ni kwa ajili ya matumizi ya nyumbani au wachoma mishikaki.

Kule machinjioni kuna serikali na kuna madaktari wa mifugo, msidanganyane mkadhani hii serikali imefeli kila eneo.

Jipe nafasi siku tembelea machinjio usiku au afajiri utajionea mengi usiyoyajuwa na utaanza kupuuza uzushi unaousikia.
 
Dogo nilijua umerudi Kigoma kumbe bado upo jijini inapambania life, hongera sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…