Dr Matola PhD
JF-Expert Member
- Oct 18, 2010
- 60,050
- 104,466
Mnadanganya sana, ukitaka kuelewa zunguka kwenye mabucha bei za nyama hazifanani unajuwa kwa nini?Karibu mjini mkuu..hizo ni nyama za ng'ombe waliokufa,ukanda huo wa buguruni mpaka gongo la mboto ndio biashara yao kubwa..
Nyama zina grade, grade one kwa Dar buchani kilo moja bei haiwezi kupunguwa shilling 10,000/=
Grade ya kawaida unaweza kuuziwa kilo kwa shilling 7000/= sasa imagine mtu anayekwenda machinjioni atapata kwa shilling ngapi?
Halafu isitoshe wauza supu za bei kitonga wengi wanauza bandama, mapupu na makolomelo, hivyo vitu machinjioni havina bei.
Binafsi naelewa vizuri bei za machinjioni unakuta tumbo lote la mbuzi umeshasafishwa kila kitu unauziwa kwa shilling 15,000/= tu, halafu ukienda bar eti unauziwa supu ya utumbo kwa shilling 2000 ni wizi mtupu.