Bukoba: Ndege ya Precision Air yapata ajali Ziwa Victoria, watu 19 wafariki dunia

Bukoba: Ndege ya Precision Air yapata ajali Ziwa Victoria, watu 19 wafariki dunia

So wengine ilikua vipi wasipite pale? au unapitwa KWa viza ? Mpaka inasemekana mapilot wamekufa , acheni zungumzia Mambo mepesi kwenye Mambo muhim, mfano ajali imeisha tokea unaficha Ili iweje, hamjui kuficha kitu ni kurutubisha tatizo,?

Waliofariki wanasema ni wale waliokuwa mbele

Wa nyuma waliwahi kutolewa na wananchi
 
Kwa maelezo hayo, unahitajika uchunguzi wa kina sana
Shida naiona hapa ni kwa response unit. Kuna fire brigade (kikosi cha Zimamoto) kipo muda wote standby (tayar) kwa uokozi. Inakuwaje................. hadi wavuvi pekee waokoe wote wale......

Kitu kingine, Huu uwanja mara nyingi umekuwa na changamoto ya hali ya hewa. Kwann usipewe kipaombele kufungiwa taa za kuongoza ndege kutua na kuruka muda wote.
 
So ndege ilikuwa itoke Bukoba iende mwanza then Tabora. Too sad. Maana hawa watumishi hawakuwa na haja ya kwenda Bukoba. Mzunguko usio na Maana na umecost maisha yao.
Mzunguko huo hauna tatizo kabisa kwenye hili. Kuna direct flights na kuna roaming flights. Wao kama waliona hiyo ya kuzunguka still kwao ni option nzuri huwezi kuwalaumu. Imekuwa ikitokea hivyo na all is well.
Tatizo kubwa lipo kwenye emergency preparedness and response mechanisms!

Nakumbuka kuna ndege ya Ethiopian iliwahi kuanguka pale Arusha airport. Rubani did everything right ndege ikafika ardhini Salama nje ya runway lakini control unit walimwambia kwa kuwa ndege yake ni kubwa, ndeefuuu kwenda juu uwanja hauna ngazi asubirie iletwe from KIA ndo waje washushwe. KIA to Arusha unazungumzia 50+Kms... Nahisi ushaanza kuona tatizo lipo!
1996 mkasa mkubwa wa MV BUKOBA hadi leo miaka 26 baadae bado hatujajipanga kikamilifu kukabiliana na dharura, ajali na majanga.
Serikali imejisahau sana imebaki kuwekeza kwenye vitu vya fahari badala ya kuimarisha mifumo ya kulinda usalama wa wananchi.

Factors za route na mizunguko ingekuja kwenye equation kama ndege ingekosa uwezo au mafuta ya kuzunguka kukamilisha ratiba zake!
Tusifumbie macho wala kunyamaza. Serikali imefanya uzembe.
Tuishurutishe ibadilike!
 
So ndege ilikuwa itoke Bukoba iende mwanza then Tabora. Too sad. Maana hawa watumishi hawakuwa na haja ya kwenda Bukoba. Mzunguko usio na Maana na umecost maisha yao.
Lakini kwenye Maelezo hayo, hajasema hiyo ndege ilikuwa ifuate huo mzunguzuko ( Mwanza - Bukoba- Tabora.
Ila watumishi wa MDH ndio walikuwa na Safari hiyo.
 
Serikali pia hiangalie huduma la shirika hili wana route nyingi kuliko idadi ya ndege, mara nyingi ndege ikitoka mbeya iyo iyo inaenda mwanza tena ndege iyo iyo jioni inaenda kilimanjalo hii hali inafanya shirika kuangalia pesa zaidi kuliko usalama wa ndege zao.

Sent from my Nokia G10 using JamiiForums mobile app
Umesahau Nairobi.
Ndege zimetengenezwa kukaa angani kuliko ardhini
 
Kwa haraka ukisikiliza maelezo ya huyu abiria na manusura wa ajali kuna points muhimu kaziongea zinatoa picha ya nini kimejiri.

1. Kutoka Dar hadi Mwanza.
Hali ya hewa ilikuwa nzuri na wamesafiri vizuri. Hii inathibitisha ndege haikuwa na tatizo.

2. Kutoka Mwanza hadi Bukoba.
Hali ya hewa ziwani haikuwa nzuri kwani kulikuwa na mawingu na mvua. Hadi Bukoba hali ilikuwa sio nzuri. Walishindwa kutua wakazunguka Misenyi huku Rubani akiwajulisha atajaribu tena kutua akishindwa watarudi Mwanza. Hii inaondoa dhania kwamba ndege haikuwa na mafuta ya kufika Mwanza. Baada ya kutoka Misenyi abiria anasema waliambiwa wajiandae ndege inatua na ghafla wakajikuta wapo majini na mbele maji yameanza kuingia. Hapa unaona ni kwa nini hakuna rubani aliepona na wengi waliofariki ni waliokuwa mbele. Ni milango ya nyuma pekee ilifunguliwa na wengi waliokuwa nyuma walitoka.

3. Ruban alishusha ndege.
Uwanja wa ndege Bukoba hauna taa za kuongoza ndege wakati wa giza, ukungu au mawingu. Ukitafakri maelezo ya huyu abiria rubani atakuwa ameshusha ndege sehemu isiyo sahihi kutokana na hali isiyo nzuri ya hewa (kutoona) hivyo kusababisha kujikita kwenye maji. Tambua unamaliza ziwa unaanza uwanja wa ndege Bukoba, Mwanza na Entebbe Uganda.

Kwa ufupi.
1. Ndege ya PA iliyopata ajali haikuwa mbovu wala kuwa na tatizo.
2. Ndege ya PA haikuwa na upungufu wa ziada ya mafuta kwani ruban alitangaza kurudi Mwanza akishindwa kutua mara ya pili.
3. Hali ya hewa kutokuwa rafiki kwa zoezi la kutua.
4. Rubani kudhani anaweza kutua katika hali hiyo ya hewani kitu ambacho hakikuwezekana na ikawa kinyume na matarajio yake.
5. Maji yalianza kuingia mbele ndio maana haikuwa rahis marubani kusalimika
6.nk...... nisimalize yote niachie wengine waendelee kuchambua maelezo ya abiria
All in all Cockpit Voice Recorder zitasema ukweli....

Yawezekana kabisa alijaribu shusha ndege ila visibility ilikuwa mbaya na ule uwanja hauna ILS, hivyo akajikuta tayari kwenye maji
 
Hizi taa za kuongezea ndege huwa ni shillingi ngapi?? Kwa nini baadhi ya viwanja havina hizi taa?!
Shida naiona hapa ni kwa response unit. Kuna fire brigade (kikosi cha Zimamoto) kipo muda wote standby (tayar) kwa uokozi. Inakuwaje................. hadi wavuvi pekee waokoe wote wale......

Kitu kingine, Huu uwanja mara nyingi umekuwa na changamoto ya hali ya hewa. Kwann usipewe kipaombele kufungiwa taa za kuongoza ndege kutua na kuruka muda wote.
 
usembassytz~p~Cknnn_CtXmx~1.jpg
 
My take.Kuna technical faults za uendeshaji wa ndege na TCAA na TAA hawana pa kujifichia(wao being the cause)
1.Runway length ya BK ni fupi sana--being 1325metres-hii ni distance ya kutua na kupaa kwa vindege vidogo kama grand caravan--marubani wetu huwa wanajitahidi sana hasa wakati wa kutua kutokana na eneo uwanja ulipo---1 mistake unapita na fence.
2.Runway lights-Pale BKZ hakuna taa za kuongozea ndege--hivyo hali ya hewa ikiwa mbaya ni ngumu mno kukadiria--the same kwenye vingine vingi.

Aftermath baada ya ajali
Zimamoto na uokoaji(useless).
Coast guard na police(mafuta ya kukimbizana na wavuvi wanayo--ila ya kuokoa hawana)
Wananchiii(Very useful)
 
Lakini kwenye Maelezo hayo, hajasema hiyo ndege ilikuwa ifuate huo mzunguzuko ( Mwanza - Bukoba- Tabora.
Ila watumishi wa MDH ndio walikuwa na Safari hiyo.
Jiongeze na wewe. Safari yao ni Tabora imekuwaje wamefia Bukoba ?Kwa akili zako no wonder CCM mpaka leo inatawala. Akili zako na akili za watanzania majority.
 
Ratiba
 
Attachments

  • 314A08A4-3DAF-4213-8DFD-F84036E2C62A.jpeg
    314A08A4-3DAF-4213-8DFD-F84036E2C62A.jpeg
    64.4 KB · Views: 5
All in all Cockpit Voice Recorder zitasema ukweli....

Yawezekana kabisa alijaribu shusha ndege ila visibility ilikuwa mbaya na ule uwanja hauna ILS, hivyo akajikuta tayari kwenye maji
Kaangalie Global online tv .Yule Majaliwa muokoaji mvuvi kaeleza. Alishuhidia na mpaka aliongea kwa ishara na mapilot wakimwambia avunje dirisha la cockpit. Afisa mmoja akamzuia eti wanafanya mawaliano na pilot.What a stupid idea. Yule dogo Majaliwa ana akili sana yaani ikiwezekana apate ajira jeshi la uokoaji.
 
Serikali pia hiangalie huduma la shirika hili wana route nyingi kuliko idadi ya ndege, mara nyingi ndege ikitoka mbeya iyo iyo inaenda mwanza tena ndege iyo iyo jioni inaenda kilimanjalo hii hali inafanya shirika kuangalia pesa zaidi kuliko usalama wa ndege zao.

Sent from my Nokia G10 using JamiiForums mobile app
Kama ndio hivyo basi basi tutegemee nyingine kutokea
 
Precision air yapata ajali Bukoba ziwa Victoria

View attachment 2408224
View attachment 2408189
View attachment 2408195

===
NDEGE YA PRECISION YAANGUKA ZIWA VICTORIA MJINI BUKOBA

Ndege ya Shirika la Ndege la Precision, imeanguka ziwani mjini Bukoba, Mkoani Kagera asubuhi ya leo Novemba 6, 2022

Taarifa za awali zinaonesha ndege hiyo imeanguka ziwani, uokoaji wa abiria unaendelea.

Taarifa kwa kina zinafuata

=====

NDEGE YA PRECISION AIR ILIKUWA IKIJIANDAA KUTUA
Mmoja wa abiria wa Precision Air, Simon Mkina amesema tukio hilo limetokea asubuhi ya leo Novemba 6, 2022 Saa mbili kasoro dakika 10 wakati ndege ikiwa inajiandaa kutua.

Amesema “Nipo eneo la tukio, nilikuwa naisubiri hiyo ndege kurudi Dar es Salaam, ghafla tukaona ndege imepitiliza, rubani ikashindwa kutua kwenye njia yake, inawezekana amekosa mawasiliano au kuna hitilafu ilitokea.

Ameongeza “Mpaka sasa hatujajua nini hasa ni chanzo kwa kuwa rubani mwenyewe bado hajatolewa ndani ya ndege na uokoaji unaendelea.”

ABIRIA waliokuwa katika ndege ya shirika la ndege la Precision Air iliyoanguka katika Ziwa Victoria kabla ya kutua uwanja wa ndege wa Bukoba wameokolewa, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kagera, William Mwampaghale amethibitisha.

Akitoa taarifa ya awali kuhusu ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 2:35 asubuhi ikiwa ni mita 100 kabla ya kutua katika uwanja wa ndege wa Bukoba, Mwampaghale amesema manusura wote wamepelekwa katika hospitali ya rufaa mkoa wa Kagera kwa ajili ya matibabu.

“Ndege ilipata ajali mita 100 kabla ya kutua uwanja wa ndege. Abiria wameokolewa na jitihada zinaendelea,” amesema nakuongeza “tukio lipo ‘under control.’”

Mwampaghale amewataka wananchi kupunguza taharuki na kuondoka eneo la tukio ili kuruhusu vyombo husika kuendelea na shughuli za uokozi.

Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokozi Zabron Muhuma amesema jeshi linaendelea na uokoaji ili kuhakikisha ndege hiyo inatolewa majini.

Imeandaliwa na Diana Deus

====

UPDATE: WATU 26 WAMEOKOLEWA KATI YA 43 KATIKA AJALI YA NDEGE
Ndege ya Precision Air iliyopata ajali wakati wa kutua Bukoba ilibeba watu 43 na tayari waliookolewa ni 26 ambao wamepelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kagera.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila ametoa taarifa hiyo kuhusu ndege hiyo ATR 42 yenye namba za usajili 5H BWF ambayo ilikuwa ikitokea Dar es Salaam kuelekea Bukoba na ilikuwa na safari ya kurudi Dar.

Aidha, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera, William Mwampaghale amesema zoezi la uokoaji la ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 2:35 asubuhi ikiwa ni mita 100 kabla ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Bukoba linaendelea kwa kuivuta ndege kuelekea ufukweni.

===============

UPDATE: WATU WATATU WAMEPOTEZA MAISHA KWENYE AJALI

Mganga Mkuu Mkoa wa Kagera Dkt. Isesanda Kaniki amesema hadi kufikia saa 9 alasiri wamepokea maiti za watu 3 waliofariki katika ajali

Amebainisha kuwa wamepokea jumla ya watu 26, Wanaume 17, Wanawake 9, huku Wanaume 2 na Mwanamke 1 wakipokelewa wakiwa wamefariki dunia.

UPDATE: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza uchunguzi ufanyike ili kubaini watu wawili wanaozidi kwenye idadi iliyoainishwa mwanzo ya watu 43. Hatua hiyo imekuja baada ya kupatikana kwa miili 19 ya waliofariki huku wengine 26 kuokolewa hivyo kufanya idadi ya watu kuwa 45.

UPDATE: WATU 19 WAMERIPOTIWA KUFARIKI MPAKA SASA
Vikosi vya Uokoaji na Wananchi wanakaribia kuifikisha nchi kavu Ndege ya Precision iliyopata ajali Ziwa Victoria, Bukoba takribani mita 100 kutoka Kiwanja cha Ndege ilikotakiwa kutua, ajali hiyo imeua Watu 19 na wengine 26 wameokolewa.

WALIOFARIKI AJALI YA NDEGE KUAGWA UWANJA WA KAITABA
Miili ya Watu 19 waliofariki katika ajali ya ndege ya Precision Air inatarajiwa kuagwa leo Novemba 7, 2022 kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila amesema utaratibu wa zoezi la kuaga unatarajiwa kukuanza Saa 4 asubuhi ukiongozwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Toka enzi za MV Bukoba hatujawahi kua na boti/meli ya uokoaji kweli? Labda hii kitu itabadilisha mtazamo wa umuhimu wakua nayo maana dah aise hapana. Mungu atupe busara kama nchi kuzingatia hivi vitu kabla hayajatokea.

Ingekuwa nchi ya wenzetu kuna kiongozi angejiuzulu kutokana na maafa ya aina hii.
 
Kaangalie Global online tv .Yule Majaliwa muokoaji mvuvi kaeleza. Alishuhidia na mpaka aliongea kwa ishara na mapilot wakimwambia avunje dirisha la cockpit. Afisa mmoja akamzuia eti wanafanya mawaliano na pilot.What a stupid idea. Yule dogo Majaliwa ana akili sana yaani ikiwezekana apate ajira jeshi la uokoaji.
 
We mnduku nimekuuliza wewe hili swali? Na hata kama ningekuuliza huwezi kujibu bila kutukana?

Mav.i kabisa[emoji57][emoji57]
Unaona ufahari gani kujinadi kama mwanamke? Unataka kumtapeli nani hapa? Mas.hoga mmekuwa huru sana nchi hii
 
Kaangalie Global online tv .Yule Majaliwa muokoaji mvuvi kaeleza. Alishuhidia na mpaka aliongea kwa ishara na mapilot wakimwambia avunje dirisha la cockpit. Afisa mmoja akamzuia eti wanafanya mawaliano na pilot.What a stupid idea. Yule dogo Majaliwa ana akili sana yaani ikiwezekana apate ajira jeshi la uokoaji.
Sahihi kabisa naunga mkono hoja.
 
Back
Top Bottom