Maneno ya huyu ni kwamba walijiokoa wenyewe.
View attachment 2408639
Kwa haraka ukisikiliza maelezo ya huyu abiria na manusura wa ajali kuna points muhimu kaziongea zinatoa picha ya nini kimejiri.
1. Kutoka Dar hadi Mwanza.
Hali ya hewa ilikuwa nzuri na wamesafiri vizuri. Hii inathibitisha ndege haikuwa na tatizo.
2. Kutoka Mwanza hadi Bukoba.
Hali ya hewa ziwani haikuwa nzuri kwani kulikuwa na mawingu na mvua. Hadi Bukoba hali ilikuwa sio nzuri. Walishindwa kutua wakazunguka Misenyi huku Rubani akiwajulisha atajaribu tena kutua akishindwa watarudi Mwanza. Hii inaondoa dhania kwamba ndege haikuwa na mafuta ya kufika Mwanza. Baada ya kutoka Misenyi abiria anasema waliambiwa wajiandae ndege inatua na ghafla wakajikuta wapo majini na mbele maji yameanza kuingia. Hapa unaona ni kwa nini hakuna rubani aliepona na wengi waliofariki ni waliokuwa mbele. Ni milango ya nyuma pekee ilifunguliwa na wengi waliokuwa nyuma walitoka.
3. Ruban alishusha ndege.
Uwanja wa ndege Bukoba hauna taa za kuongoza ndege wakati wa giza, ukungu au mawingu. Ukitafakri maelezo ya huyu abiria rubani atakuwa ameshusha ndege sehemu isiyo sahihi kutokana na hali isiyo nzuri ya hewa (kutoona) hivyo kusababisha kujikita kwenye maji. Tambua unamaliza ziwa unaanza uwanja wa ndege Bukoba, Mwanza na Entebbe Uganda.
Kwa ufupi.
1. Ndege ya PA iliyopata ajali haikuwa mbovu wala kuwa na tatizo.
2. Ndege ya PA haikuwa na upungufu wa ziada ya mafuta kwani ruban alitangaza kurudi Mwanza akishindwa kutua mara ya pili.
3. Hali ya hewa kutokuwa rafiki kwa zoezi la kutua.
4. Rubani kudhani anaweza kutua katika hali hiyo ya hewani kitu ambacho hakikuwezekana na ikawa kinyume na matarajio yake.
5. Maji yalianza kuingia mbele ndio maana haikuwa rahis marubani kusalimika
6.nk...... nisimalize yote niachie wengine waendelee kuchambua maelezo ya abiria