Uchaguzi 2020 Bulembo: Taratibu za CCM haziruhusu mwanachama mwingine kuchukua fomu ya kugombea urais zaidi ya John Magufuli

Mkuu, hebu muwe mnatumia akili hata kidogo na kuacha propaganda na utapeli wa wazi. Hivi Membe anachukuaje fomu huko CCM ikiwa alifukuzwa uanachama na sasa si mwanachama wa CCM?
Mdau..kwani kuna mahali kamtaja Membe..? Au mie sijaelewa hapa...
 
Baada ya Mheshimiwa raisi kuvunja Bunge na wagombea mbali mbali kujitokeza kuchukua fomu za kugombea uraisi!hadi sasa kachero mbobezi Benard Membe hajajitokeza hadi sasa!kwani uko wapi? ulituahidi utanuka mbona harufu sisikii???

Tupe matumaini kama upo mbioni au ndio basi tena!!kwa maana mwenyekiti ameshachukua fomu sisi wakulima wa korosho wa huku mtwara tunakusubiri kwa hali na mali tukuunge mkono!!!

Kama kuna mwakilishi wake au yeye mwenyewe humu jukwaani aje atuambie kulikoni!ukimya wako unatutisha sisi ambao tunasubiria kunuka kwako tena kwa hamu ili tunuse!!!!!!Jitokeze!tuambie ili tuondoe duku duku letu!!
 
Kusoma na kuandika tu ndiyo shida ya bunge letu kuwa na watu wa aina ya Bulembo
 
Mbona wakati wa kina Mkapa na kina Kikwete na Mwinyi wanachama wengi walijitokeza kuchukua form?
 
Atachukua form tu ingawa nasikia katibu anakimbia ofisi kama wale ma DED wanavyo kimbiaga wagombea wa cdm wakati wa kurudisha form kwenye chaguzi za marudio
 
Wanajisikia aibu kubwa sana mbele ya umma wa watanzania na nje ya mipaka ya nchi yetu.

Ila sema hawana jinsi ya kulisemea maana midomo yao imepigwa kufuli
 
Alifukuzwa kwenye kikao kipi? Unamfukuzaje mtu kwa maneno tu bila ya kumkabidhi barua?

Membe hakuwa mwana chama kama ulivyo wewe huko kwenu mbwinde, Membe alikuwa ni kiongozi wa ngazi za juu ndani ya ccm. Hawezi kufukuzwa kama utakavyo fukuzwa wewe.
Mkuu, hebu muwe mnatumia akili hata kidogo na kuacha propaganda na utapeli wa wazi. Hivi Membe anachukuaje fomu huko CCM ikiwa alifukuzwa uanachama na sasa si mwanachama wa CCM?
 
Ndiyo kisheria bado ni mwana ccm maana hakuna barua mliyo mpatia ya kumfukuza
Mkuu kadri siku zinavyozidi kwenda wana CDM mnachanganyikiwa na kupoteza kumbu kumbu,

Agombee uraisi kwani Membe ni mwanachama wa CCM ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…