BullDoza Mwamposa Ana Powers za Mvuto wa Ajabu, Aleta Balaa Kubwa Kawe na Maeneo ya Jirani, Mkesha Wake, Kawe, Mikocheni, Mbezi Beach, Wote Tumekesha!

Ana mzidi wingi wa watu Babu wa Loliondo? make na yule ni alikuwa tapeli wa karine ya 21.
 
Jana nilikaa kwenye foleni imeanzia mikocheni A mpk kawe yaani masaa matatu hakuna kusogea hata kidogo daaaah...leo naona toka asubuhi mpk sasa watu wanaendelea kutembea kwenda majumbani kwao baada ya kukosa usafiri
 
Watu wanatakiwa kuibana serikali iboreshe uchumi na hali ya maisha zikiwemo huduma bora za afya, maji, barabara, umeme, mishahara stahiki kwa watumishi, ajira kwa vijana badala ya kuishia kukata tamaa kwa kutegemea kutoboa kwa miujiza ya manabii feki.

Tukisema kuna ajenda nyuma ya kuongezeka kwa hawa manabii feki tutakuwa tumekosea?
 

Hypnotizing the society for political authorities! Regretfull to be Tansanian
 
Kwa mantiki hio Watanzania wana matatizo mengi sana ambayo yamekosa utatuzi wa kiserikali na kukimbilia kwenye Imani, Nadhani pia viongozi wasishangae kujaza kwa Mwamposa bali watumie kusanyiko hilo kama evaluation ya kinachoendelea kwa ground.
Uko sahihi kabisa kuna wenye shida ambazo ukifatilia kwa makini utagundua ni maswala ya kisheria tu yangemsaidia, kuna wenye shida ambazo msaada wa matibabu ungemsaidia lakini yote hayo yanabebwa kama uko na uchumi mzuri je uchumi mzuri utakujaje wakati anaenda kwa mwamposa anataka muujiza wakupata kazi au hata kibarua na anadegree yake hii no ishu ya ukosefu wa ajira.
 
Hata TB Joshua alikuwa hivyo hivyo ila alichojuwa anawafanya Watumishi wake utajua haujui
 
LAKINI...
Mbili; Umesema nyote mmekesha mmekesha mliokwenda au kelele zimesababishia hata wasiohusika kukesha kwa bughudha ? Hio sio Kosher (furaha yako / yenu isiwe kero kwa wengine)
Hiki ndicho kilichotokea, PA iliotumika ilikuwa too powerful kwa usiku mkubwa hivyo kuleta noise pollution na nuisance trespass kwa majirani na maeneo ya karibu.

Mimi naishi Mbezi Juu, Goba Rd. Usiku sikulala kwa kelele za mahubiri.

Itambidi Mwamposa awatumie watu wa sound technician wamashauri PA ya kufunga na sound set up ya speaker za aina moja, na zikae equal distance kwa kuangaliana at 90 degree angles ili sauti zigongane at the centre na kusambaa hapo watu wanapokesha bila kuwakera majirani.

Mkesha wa jana, wafuasi wake wamekesha, majirani wote, Wakristo na Waislamu wamekesha watake wasitake!.

Hasara za mkesha wa kuwahubiri watu, wakusikilize watake wasitake ni kero kwa waumini wa dini nyingine ambao nao lazima wakeshe watake wasitake!.

Faida za huu mkesha, ukimsikia hata bila kuhudhuria, ukaamini anachohubiri, unaponywa!. Hivyo mahubiri hayo, yanasaidia wengi, wakiwemo ndugu zetu wa imani tofauti!. Faida ni kubwa kuliko kero!.
P
 
Kuna mtu alishasema multiracial can mix lakini multicultural can not mix..., chuki baina ya imani inaweza kutokea sio sababu watu hawapendi sura au wengine waamini tofauti bali kero zinazosababishwa na wao kwa hao wengine...,

Nadhani sheria zipo ifike wakati hawa watu wakitaka kufanya kitu waende sehemu zenye sound proof au vyovyote watakavyofanya isilete kero kwa yoyote asiyehusika....

Hizi Haki za Kuabudu ziandane na Haki ya kutokuabudu kwa wengine...
 
Hizi Haki za Kuabudu ziandane na Haki ya kutokuabudu kwa wengine...
Naunga mkono hoja, haki ya mtu mmoja kuabudu Mungu wake, isiwe kero kwa watu wengine, tena nchi nyingine, hata Adhana ya Waislamu inaratibiwa kwa viwango fulani ili isiwe kero kwa wengine, sambamba na kengele makanisani.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…