BullDoza Mwamposa Ana Powers za Mvuto wa Ajabu, Aleta Balaa Kubwa Kawe na Maeneo ya Jirani, Mkesha Wake, Kawe, Mikocheni, Mbezi Beach, Wote Tumekesha!

BullDoza Mwamposa Ana Powers za Mvuto wa Ajabu, Aleta Balaa Kubwa Kawe na Maeneo ya Jirani, Mkesha Wake, Kawe, Mikocheni, Mbezi Beach, Wote Tumekesha!

Hata wewe ushaingia huko, unajuaje kama mahubiri yameponya watu wasiotaka kiyasikia??

Mke ana nguvu sana.
 
Kwa watumiaji wa Tigo Pata GB za bure kwa kufuta maelekezo haya.



1. Ingia TigoPesa app (Kama hauna download play store)

2. Ingia Invite & Earn

3. Bonyeza Redeem

4. Weka hii code 2ZJVO8ZK

Baada ya hapo utapata 2GB na DK kibao bure kabisa!!
 
Kakaa hatareer nimetokaaa saa 0620am nilichomwomba Mungu niwe na nguvu kama zake za kuombaa aisee mwamba ana stamina hatareee yaaan kipindi chapilii alivyorudi kama pakomeeeeee wayaa nkaanza onaa majiran zangu pemben smart wanagalagala nkajua kumekucha ngoja niweke na mie miguu sawa hataree
Pole sana mkuu
 
Wanabodi,

Huyu Pasta Bulldoser, Mwamposa.. sio mchezo...
1. Nyomi!.
Kiukweli kabisa watu ni wengi ajabu, sijui hata walitoka wapi, mabasi yote yalijaa, watu kwa makundi wanatembea kwa miguu, tumekaa foleni masaa 3!.

Hii maana yake Bulldozer Mwamposa, ana nguvu za upako wa mvuto wa watu kwenye mikutano yake!, nisichokijua ni the source of those powers if they are the powers of light, or the powers of darkness, hivyo, wanachofanyiwa hao the multitudes is nothing but hypnosis, watu wanafanyiwa hypnotism, wanakuwa hypnotized, hivyo huwaambii kitu kuhusu Mchungaji wao.
Mimi pia japo ni Mkristo wa lile kanisa moja Kuu, Takatifu la Mitume, ambao tunaamini kwenye Utatu Mtakatifu na asili ya binadamu ni dhambi hivyo tunaamini kwenye ubatizo mmoja, kuungama na maondoleo ya dhambi, hivyo hapa duniani hatuamini imani za wokovu.

Ila Maza wangu (RIP), alikuwa mlokole na kunichagulia wife aliyeokoka, hivyo wife ni mlokole fulani hivi, from time to time huwa namsindikiza, na kuwafuatilia wahubiri mahubiri yao kwenye TV, na humu nimeisha wahi kupandisha threads zaidi ya 10 kuwahusu wahubiri mbalimbali na miongoni mwake ni hizi
- Kauli ya Kakobe "Magufuli atubu", yaibua mambo! Je asili halisi ya Rais Magufuli ni Msukuma, Mhaya au Muha wa Kakonko?

Faida na Hasara ya Mkesha wa Mwamposa.

Hiki ndicho kilichotokea, PA iliotumika ilikuwa too powerful kwa usiku mkubwa hivyo kuleta noise pollution na nuisance trespass kwa majirani na maeneo ya karibu.

Mimi naishi Mbezi Juu, Goba Rd. Usiku sikulala kwa kelele za mahubiri.

Itambidi Mwamposa awatumie watu wa sound technician wamashauri PA ya kufunga na sound set up ya speaker za aina moja, na zikae equal distance kwa kuangaliana at 90 degree angles ili sauti zigongane at the centre na kusambaa hapo watu wanapokesha bila kuwakera majirani.

Mkesha wa jana, wafuasi wake wamekesha, majirani wote, Wakristo na Waislamu wamekesha watake wasitake!.

Hasara za mkesha wa kuwahubiri watu, wakusikilize watake wasitake ni kero kwa waumini wa dini nyingine ambao nao lazima wakeshe watake wasitake!.

Faida za huu mkesha, ukimsikia hata bila kuhudhuria, ukaamini anachohubiri, unaponywa!. Hivyo mahubiri hayo, yanasaidia wengi, wakiwemo ndugu zetu wa imani tofauti!. Faida ni kubwa kuliko kero!.
inaendelea...

Paskali
Nashukuru umeng'ata ukapuliza halafu ukafanya peaceful landing.Mimi pia nilikuwa mji fulani hivi off Goba rd,nilisikia vizuri na nilifurahia zile nguvu za Mungu zilizonifuata pale kitandani nilipolala.
Faida zilikuwa nyingi kuliko hasara
 
Hizi ni dalili za umasikini, maana raia wengi wanaamini katika miujiza kuliko kufanya ibada, kutenda mema na kuacha mabaya na mwisho kufanya kazi kwa bidii.

Hakuna Taifa duniani watu wake wameendelea kwa miujiza baadala yake kufanya kazi kwa bidii na kulinda rasirimali.
Saudia na Uarabuni na Hata Israeli kwenye chimbuko la dini watu hufanya kazi kwa bidii na viongozi kusimamia kwa uaminifu rasirimali za nchi ili zinufaishe kila mtu.

Ni rahisi huo umati wa watu kukusanyika kwa Mwamposa na sio kuwaambia tuandamane kupinga wizi kwenye mifumo, kupambania rasirimali zetu zitunufaishe watanzania wote, kuandamana kupambania elimu Bora Kwa watu wote na huduma Bora za Afya pia.
 
Unabaki unatabasamu au kuchekea chooni..ukishaona una jamii kama hii yetu wewe cheza na fantasies zao tu, alafu uone kitakachotokea, utafurahi...ni rahisi kupata pesa TZ kama ukiamua kujifyatua.
 
Hiyo nyomi inaonesha watanzania umaskini ni mkubwa sana na watu wanatafuta mafanikio kwenye kukanyaga mafuta au kutafuta mafanikio kwa mtu..na nyie socialites badala mkemee watu wafanye kazi kama wachina nchi mwao, mmekaa mmekalisha matako yenu mnahamasisha tu..shenzi kabisa.
Waache 2 si wanachunguza jua☀️☀️☀️ kwa torch 🔦🔦
 
Hata Gwajima na kakobe walianza hivyo so hapa alipo huyu ndipo pale tunasema jua la utosi sasa, ambapo anachuma na kuwekeza nje ya hiyo biashara ya kanisa.

Baadaye anajenga jengo la kanisa na baadaye sana ubunge au anaachana na kila kitu anatulia kwenye kimbweta kama kakobe.

Never trust hawa wa kizazi hiki ni wanakusanya pesa na serikali ikiwa upande wake haiwezi kumpinga au vyovyote sababu wanakula na kipofu.
 
Watu wamekata tamaa na hawasomi maandiko kwa ufasaha!Biblia inajitafsiri yenyewe.Watu wangu waangamia kwa kukosa maarifa.
 
Ukombozi upi? wiki ijayo akiandaa tamasha jingine wataenda hao hao, anacheza na akili za mazezeta, pale hutasikia Bible inasomwa, pale ni shuhuda za wale watu walio pangwa watoe shuhuda tena kwa nyanja tofauti.

Kuna shuhuda za Biashara, mikopo, ndoa, Ugumba, Matatizo ya familia, kupata kazi,Magonjwa sugu.
.Hapo ndio abako wakamatia wajinga
Niliwahi kumuona mtu ninayemfahamu sana , na changamoto alizokuwa anapitia. Siku hiyo namuona ETV anatoa ushuhuda kwa Mwamposa. Yaani walikodi basi zima kwenda Dar, alichokuwa anakishuhudia na ukweli tuliokuwa tunaufahamu vilikuwa vitu viwili tofauti kabisa. Alivyorudi tumekaa grocery tunakula bia namuuliza kwa nini ulienda kushuhudia uongo. Ameishia kukimbia mji na urudi kwao vijijini huko pamoja na ushuhuda wake wa uongo uliopitiliza.
Alijua kuwa kilichomtoa kwenye madeni ni kuuza nyumba yake, lakini siku ile ya ushuhuda anadai ni upako wa mafuta ulimpatia 35M ghafla, ilihali ni mauzo ya nyumba na bado kakimbia madeni lukuki, yuko maporini huko anachoma mkaa.
 
Back
Top Bottom