Bunda: Lissu atangaza kubadili Sheria ya madini, kwamba atajayeyagundua kwenye ardhi yake yatakuwa yake

Bunda: Lissu atangaza kubadili Sheria ya madini, kwamba atajayeyagundua kwenye ardhi yake yatakuwa yake

Mkuu, wakati wa Nyerere,tulikuwa na mfumo wa Uchumi wenye kufuata siasa za Ujamaa na Kujitegemea ambapo mali ya asili kama ardhi nk ni mali ya Umma. Conversely, tulipoanza kuachana na siasa hizo,tuk a ingiza vichwa vyetu kwenye mfumo tofauti ambao hata kwenye katiba yetu haupo, ndipo shida ilipoanzia.
Watu hasa viongozi wa juu wakaanza kujimegea ardhi na maliasili kwa kigezo cha Soko huria na uwekezaji. Wanaharakati wa kuutetea huu mfumo zaidi ni viongozi wa ngazi za juu,wenye nafasi n zaidi mafisadi.
Wananchi wa kawaida wenye nchi wameachwa solemba wakabaki wakiambiwa tunawajengea shule zahanati,barabara nk.
Swali kwako, ni kosa kuwaambia wananchi ukweli kuwa hii dahabu ni mali yenu? Kuwa, mnshitaji kuwa sehemu ya uwekezaji na siyo kusubiri "vimatunda" vya uwekezaji?
Mkuu, inaonekana unahitaji elimu zaidi. Lisu yuko sahihi pamoja na kuwa mimi siyo wa Chama chake
Kwani saizi Mali zipi sio za Umma? Na ni za nani? Ardhi ni Mali ya Umma haid keshokutwa na uelewe neneo Ardhi kwanza , mengine hayo ni blaa blaa zako
 
Lissu kachanganyikiwa. Hicho anachokisema ni ujinga mtupu. Bora hata angesema kwamba madini yakigunduliwa kwenye ardhi yako na wewe unakuwa shareholder wa kampuni itakayochimba uwe unapata mrabaha.
Lkn mmiliki wa ardhi yenye uoto wa bangi sio mali ya serikali sio 🤣🤣🤣🤣
 
toka kipindi cha lowasa mlisema hivyohivyo nyie makuwadi ya warabu koko lakin 2020 yule mbwa wa chato akaona chadema mziki mnene akasanda.
Hujaelewa,

Nachosema ni kuwa bila kuwapo Tume huru na Katiba mpya kabla ya Uchaguzi,

CDM kushinda uchaguzi ni ndoto ya mchana, maana Katiba hii haitoi nafasi ya kukata Rufaa mahakamani, na akishatangazwa, ametangazwa.

Jambo hili amekuwa akisisitiza zaidi Mnyika na Lissu, msisituzo unahitajika zaidi Ili kuhamasisha vijana kushiriki uchaguzi.
 
Uko sahihi Lakini shida itakuja kwenye kujua kiasi Cha madini kilichopatikana Ili upate mrabaha wako.
Mpaka serikali yenyewe imekwama inapigwa Kila kukicha
Mkuu hili suala la madini ni zito mno. Lina mikono michafu mingi kuanzia serikalini, wanasiasa, watu binafsi hadi viongozi wa dini. Ni suala tete mno kwenye nchi zetu hizi. Fikiria kiongozi wa dini kama Prophet Bushiri na Uegbert Angel nao huwa wanapiga madili haramu ya dhahabu na mawe mengine ya thamani..!!
 
Hakuna sheria ya kimataifa inayozipangia nchi jinsi kumiliki au kutumia rasilimali zake, ni uongo mtupu.
C6429A47-A205-4B7E-A2BB-5647075FDB00.jpeg

Mnatabia ya kupenda kubishaga tu, natural resources ni mali ya nchi husika.
 
Lissu kachanganyikiwa. Hicho anachokisema ni ujinga mtupu. Bora hata angesema kwamba madini yakigunduliwa kwenye ardhi yako na wewe unakuwa shareholder wa kampuni itakayochimba uwe unapata mrabaha.
Wewe na Lissu nani kachanganyikiwa.
 
Wewe umekielewa? Unajua maana ya neno Ardhi?Lisu anasema mwenye plot ndio aje a bargain na mwekezaji au serikali Sasa hatujafikia kuweka Ardhi Mali binafsi.
Ni wewe na nani hamjafikia? Na ni kwa nini hamfikii? Jitahidi kumuelewa Lissu anachokiongea. Tuachane na sheria tata za wakoloni na ambazo baadhi tumejitia kurithi bila kuelewa.
Nikiwa na kipande cha ardhi (eneo), ikagundulika kuna madini, automatically mimi ninapaswa kuwa shareholder kwa uwekezaji wowote ule whether govt au mwekezaji yoyote. For each unit of valuable resource extracted,natakiwa kupata % share ya ile total value. Na serikali kama msimamizi Mkuu, atapata siyo kwa niaba yangu ila share yake.
Hicho ndicho anachoongea Lissu. Ilivyo hivi sasa, naambiwa ili ninufaike na madini yanayochimbwa kwenye eneo langu,nifungue mgahawa wa chai niwauzie wachimbaji na wawekezaji.
 
Nchini Tanzania kwa sheria za sasa , shambani kwako kukikutwa madini , basi haraka sana madini hayo na shamba lako hilo vinageuzwa kuwa mali ya serikali , na baada ya muda mfupi wataletwa wawekezaji wa kiarabu au wa kizungu kuchimba madini hayo , huku wewe ukitimuliwa kwa mijeledi au hata bunduki bila huruma .

Lakini kwenye shamba lako hilo kukikutwa Bangi jua umekwisha , utamilikishwa bangi hiyo na kupigwa pingu .

Sasa leo Tundu Lissu amesema kwamba atakayekuta madini kwenye eneo lake hayo madini yatakuwa yake .mwenyewe , ataamua cha kuyafanya

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)-Bara, Tundu Lisu ametaja mambo manne yatakayorekebishwa kwenye sheria ya madini pindi chama hicho kitakapoingia madarakani ili kuwanufaisha wachimbaji wadogo nchini.

Lissu amesema hayo leo Jumatano, Septemba 6, 2023 wakati akihutubia mkutano wa hadhara wa Operesheni +255 Katiba mpya, eneo la Kinyambiga, Bunda mkoani Mara.

Amesema licha ya sheria ya madini kusema madini yote nchini ni mali ya umma chini ya udhamini wa Rais kwa niaba ya Watanzania lakini amedai kiuhalisia madini ni mali ya Rais.

Lissu amesema suluhisho la kwanza, Chadema itakapoingia madarakani ni kubadilisha sheria hiyo akidai madini yanatakiwa yawe mali kwanza ya wenye ardhi ambaye ataelewana na atakaye yagundua kwenye ardhi yake.

Pili, sheria iseme machimbo ambayo yanatakiwa yawe kwaajili ya wananchi wa kwetu tu na ukweli ni kwamba sheria ndivyo inavyosema ya sasa lakini shida ni CCM...hizi zinazoitwa PMR remaining licence hizi ni leseni zinazotolewa kwaajili ya watanzania," alisema Lissu akihoji wageni wanakujaje mahali hapo.

Alisema wananchi, vijiji, halmashauri na Serikali kuu wanatakiwa kunufaika na rasilimali ya madini yaliyopo kwenye maeneo yao.

Tatu, linalohitaji mabadiliko ni Serikali inapotoa leseni kwa kampuni kubwa lazima kuwe na mgawanyo wa umiliki na faida zake.

Nne, ni kushugulika na mamlaka ya Rais, akidai Katiba iliyopo sasa siyo tu inamfanya Rais amiliki rasilimali za nchi yakiwemo madini, misitu na wanyama pori bali pia inampa nguvu ya kumiliki nchi na watu wake.
Hayo ndio watu wanataka kuyasikia sio habari za mtu aliyekwisha kwenda mbele ya haki !!
 
Ni wewe na nani hamjafikia? Na ni kwa nini hamfikii? Jitahidi kumuelewa Lissu anachokiongea. Tuachane na sheria tata za wakoloni na ambazo baadhi tumejitia kurithi bila kuelewa.
Nikiwa na kipande cha ardhi (eneo), ikagundulika kuna madini, automatically mimi ninapaswa kuwa shareholder kwa uwekezaji wowote ule whether govt au mwekezaji yoyote. For each unit of valuable resource extracted,natakiwa kupata % share ya ile total value. Na serikali kama msimamizi Mkuu, atapata siyo kwa niaba yangu ila share yake.
Hicho ndicho anachoongea Lissu. Ilivyo hivi sasa, naambiwa ili ninufaike na madini yanayochimbwa kwenye eneo langu,nifungue mgahawa wa chai niwauzie wachimbaji na wawekezaji.
Subiria Lisu awe Rais wa Nchi ya kufikilika ndio atafanya huo upuuzi
 
Subiria Lisu awe Rais wa Nchi ya kufikilika ndio atafanya huo upuuzi
Upuuzi tunao sisi. Hatutaki kufungua uelewa. Anachoongea Lissu kina logic. Ni namna gani logic yake iboreshwe kuwa sheria au utaratibu kamili kwa maslahi ya wote ni kazi yetu.
 
Back
Top Bottom